Saturday, June 21, 2014

NJEMBA YAFUMANIWA IKILA UNYUMBA NA MKE WA RAFIKI AKE

Na mwandishi Jk boy
Mume aliyejulikana kwa jina moja la Ngosha,
mkazi wa Mabibo jijini Dar, amemfumania rafiki
yake aitwaye Jazira akiwa chumbani na mkewe
Jack wakiivunja amri ya sita ya Mwenyezi
Mungu.Tukio hilo lilitokea Jumanne iliyopita saa
12 alfajiri ambapo ilidaiwa kuwa Jack alikuwa
chumbani na mwanaume huyo ambaye ni
mpangaji, wenzake wakipeana maraha.
Imedaiwa kuwa, wawili hao walikuwa wakimtegea
Ngosha akitoka kwenda katika shughuli zake,
Jazira alikuwa akizama katika chumba cha rafiki
yake na kufanya mchezo wa kikubwa.
Wapangaji wenziye na Jack wamedai kuwa, mke
huyo wa mtu ambaye ana miezi miwili tangu
aolewe kutoka mkoani Tabora, amekuwa kero
katika nyumba hiyo kwani amekuwa akipiga
kelele za kimahaba nyakati za asubuhi ambapo
watu wengi wanakuwa wakielekea kazini.
“Hata sisi wanawake tunaoishi nyumba hiyo tuna
waume zetu tunawalilia lakini kinachotusikitisha
mwenzetu anamlilia Jazira badala ya mumewe
ambaye anakuwa amekwenda kazini,” alisema
mmoja wa wapangaji wa nyumba hiyo.
Imeelezwa kuwa, siku hiyo mlinzi wa msikiti
alikwenda kumwamsha Ngosha kwenda kusogeza
gari lake ili watu wapite na alipofika katika
chumba chake, alikuta mlango wa sebuleni ukiwa
wazi lakini hakukuwa na mtu, ila chumbani kwake
kulisikika redio ikizungumza kwa sauti kubwa.
Jirani mmoja aliyedai kuchoshwa na tabia hiyo,
alimshauri mlinzi huyo kwenda kusikiliza kwenye
dirisha la chumba hicho na waliposikia sauti za
kimahaba wakakubaliana wamtonye mjumbe wa
Serikali ya Mtaa wa Kanuni, Mabibo aliyetajwa
kwa jina la Asha ambaye alifika na kusikia
‘mchezo’ ukiendelea chumbani
Wakati huohuo, Ngosha akapigiwa simu kuja
kushuhudia mchezo huo mchafu wa mkewe
alioufanyia ndani ya chumba chake.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema, alipofika
Ngosha nyumbani na kutonywa kilichotokea
alipandwa na hasira na kuangusha varangati kwa
rafiki yake lakini baadaye akatulizwa, akamtaka
Jazira amlipe shilingi milioni 1.2 ili amuachie mke
moja kwa moja.
JAZIRA ANA LAKI 2
Jazira alisema hakuwa na kiasi hicho isipokuwa
anaweza kulipa shilingi laki mbili tu, jambo
lililomfanya Ngosha kuomba msaada wa askari
mgambo na kumpeleka mgoni wake Kituo cha
Polisi cha Urafiki kwa ajili ya hatua zaidi za
kisheria.

Saturday, June 7, 2014

DIAMOND PLATNUMZ AMEHUDHURIA TUZO ZA MTV MAMA 2014

Diamond Platinumz amehudhuria tuzo za MTV MAMA2014 akiwa na kampani ya watu kadhaa kutoka Tanzania na mchumba wake Wema Abraham Sepetu, katika ukumbi wa ICC Arena, hapa Durban Afrika Kusini.
Diamond anawania tuzo mbili, Best Male na Best Collaboration (Number One Remix ft Davido).
Utaratibu ulianzia kwenye zuria jekundu aka Red Carpet na kupoz kwa ajili ya picha na waliungana na watu mbalimbali maarufu.
Kuhusu tuzo alizokuwa akiwania Diamond, Tuzo ya Best Collabo kupitia wimbo wa Number One Rmx imechukuliwa na Uhuru Ft DJ Bucks, Oskido, Professor, Yuri Da Cunha -Y-tjukutja, na tuzo ya Best Male Artist ilichukuliwa na Davido.
Hongera kwa Diamond kwa hatua kubwa kwenye muziki wa Kimataifa na kuwakilisha Tanzania Vizuri.