Friday, April 17, 2015

WAKILI WA GWAJIMA AMEANDIKA HAYA BAADA YA KUTOKA MAHAKAMANI KISUTU LEO MCHANA AKIWA NA MTEJA WAKE ASKOFU GWAJIMA

Tumetoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Dar es Salaam iliyopo
Kisutu ambapo Askofu Josephat Gwajima ameshtakiwa kwa;
(1).Kutoa lugha ya matusi kwa Polycarp Cardinal Pengo.
Mahakama imemuachia Askofu Gwajima kwa dhamana ya
kujidhamini yeye mwenyewe.(2). Kufanya uzembe katika silaha
anayomiliki kisheria kiasi kwamba ikaangukia mikononi kwa
Askofu Yeconia Bihagaze na wenzake wawili, na kwa Askofu
Bihagaze na wenzake wawili kupatikana na silaha na risasi
wakati siyo wamiliki halali wa Silaha hiyo inayomilikwa na
Askofu Gwajima. Mahakama imewaachia washtakiwa wote kwa
kudhaminiwa na mdhamini mmoja mmoja.
Case itatajwa tarehe 4 April.
Mpaka tunakwenda Mahakamani Jeshi la Polisi halijajibu Barua
yetu ya kutaka watutajie kifungu cha Sheria kinachowapa
mamlaka ya kudai nyaraka zinazohusiana na umiliki wa
helicopter na usajili wa Kanisa la Glory of Christ Tanzania
Church/Ufufuo na Uzima na nyinginezo, na wala Askofu
Gwajima na wenzake hawajashtakiwa kwa chochote kuhusiana
na suala hilo.

Thursday, April 9, 2015

KESI YA MINJA YAPIGWA CALENDAR TENA

THURSDAY , 9TH APR , 2015

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara nchini, Johnson Minja leo amefikishwa mahakamani kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali ya kesi inayomkabili ya uchochezi, lakini upande wa serikali ulikuwa haujakamilisha kuandika maelezo hayo.

Mwendesha mashtaka mwandamizi wa serikali, Rose Shio aliiambia mahakama kuwa kesi hiyo ilifika mahakamani hapo leo kwa ajili ya kusikilizwaji wa awali lakini upande wa serikali ulikuwa bado haujakamilisha kuandika maelezo hayo ya awali.

Mweyekiti wa Shirikisho la vyama vya Wafanyabiashara nchini, Bw. Jonson Minja (aliyevaa koti jeusi) huku akiongea na katibu wake Mchungaji Kiondo

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara nchini, Johnson Minja leo amefikishwa mahakamani kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali ya kesi inayomkabili ya uchochezi, lakini upande wa serikali ulikuwa haujakamilisha kuandika maelezo hayo.

Mwendesha mashtaka mwandamizi wa serikali, Rose Shio aliiambia mahakama kuwa kesi hiyo ilifika mahakamani hapo leo kwa ajili ya kusikilizwaji wa awali lakini upande wa serikali ulikuwa bado haujakamilisha kuandika maelezo hayo ya awali.

Amesema kuwa kesi hiyo leo imekuja mahakamani kwa ajili ya usikilizwaji wa awali lakini kwa bahati mbaya upande wa serikali umeshindwa kuandika maelezo ya awali kwa hiyo akaomba ipangwe tarehe nyingine kwa ajili ya kusikiliza maelezo ya awali ya kesi hiyo.

Wakili wa mshtakiwa huyo Godfrey Wasonga amesema hana kipingamizi na ombi hilo la mwendesha mashtaka wa serikali na kuomba kesi hiyo ipangiwe tarehe nyingine kwa ajili ya usikilizwaji wa awali.

Baada ya maelezo hayo, hakimu mfawidhi wa mahakama ya Wilaya ya Dodoma, Rhoda Ngimilanga alisema kesi hiyo itatajwa tena Mei 7 mwaka huu na mshtakiwa ameendelea kuwa nje kwa dhamana.