Tuesday, June 30, 2015

Watch Ali kiba _chekecha official video

Watch "Alikiba - Chekecha Cheketua (Official Video)" on YouTube - https://youtu.be/ZbCmbWktYh4

Sunday, June 14, 2015

AJALI MBAYA YATOKEA IRINGA



Basi la abiria la Another G limepata ajali eneo la Kinyanambo Mafinga wilaya ya Mufindi katika mkoa wa Iringa. Gari hilo limegongana usokwa uso na lori aina ya Scania ambapo taarifa za awali zinaeleza kwamba kutoka kwenye gari hilo la abiria wamefariki watu 23 wakati kutoka kwenye lori amepona mtu mmoja pekee na wengine wote wamefariki akiwemo dereva wa lori hilo.

Aidha wakazi wa maeneo jirani ambapo ajali hiyo imetokea wameeleza kwamba ajali hiyo ni mbaya sana.

Ndugu msomaji wa mtandao huu endelea kufuatilia mtandao huu kwa habari zaidi juu ya ajali hii.

Saturday, June 13, 2015

WASHINDI WA TUZO ZA KILIMANJARO MUSIC AWARDS 2015

ENTERTAINMENT

Orodha kamili ya washindi wa Kilimanjaro Music Awards 2015.

Hii ni orodha kamili ya washindi wa tuzo za muziki Tanzania Kilimanjaro Music Awards 2015 zilizofanyika 13 June 2015 Mlinani City jijini Dar es salaam.

#FahamuKTMA2015 Tuzo ya Mtumbuizaji Bora wa Muziki wa Kiume wa Mwaka ameshinda>Ali Kiba.

#FahamuKTMA2015 Tuzo ya Mwimbaji bora wa kike Bongo Fleva ameshinda> Vanessa Mdee aka V Money

#FahamuKTMA2015 Tuzo ya Msanii Bora wa Kiume Taarab ameshinda >Mzee Yusuph

#FahamuKTMA2015 Tuzo ya Mwimbaji Bora wa Kike Taarab ameshinda> Isha Mashauzi.

#FahamuKTMA2015 Tuzo ya Mwimbaji Bora wa Kiume Kutoka Bendi ameshinda >Jose Mara

#FahamuKTMA2015 Tuzo ya Wimbo Bora wa Mwaka wa Muziki wa Taarab imeshinda >Mapenzi Hayana Dhamana Yake Isha Mashauzi

#FahamuKTMA2015 Tuzo ya Wimbo Bora wa Mwaka imeshinda ‘Mwana‘ Ya Ali Kiba

#FahamuKTMA2015 Tuzo ya Wimbo Bora wa Kiswahili Kutoka Bendi imeshinda >’ Walewale ‘ ya FM Academia

#FahamuKTMA2015 Tuzo ya Wimbo Bora wa Muziki wa R&B imeshinda single ya Jux >‘Sisikii’

#FahamuKTMA2015 Tuzo ya Wimbo Bora wa Hip Hop imeshinda single ya Profesa Jay> Kipi Sijasikia Ft Diamond @diamondplatnumz

#FahamuKTMA2015 Tuzo ya Wimbo Bora wa Reggae&Dance Hall ameshinda > Maua Sama

#FahamuKTMA2015 Tuzo ya Rapa Bora wa Mwaka Muziki wa Bendi ameshinda> Ferguson

#FahamuKTMA2015 Tuzo ya Msanii Bora wa Hip Hop Ameshinda >Joh Makini

#FahamuKTMA2015 Tuzo ya Wimbo Bora wa Afrika Mashariki wameshinda Kenya >Sauti Sol Kupitia wimbo wao wa Sura Yako

#FahamuKTMA2015 Tuzo ya Mtunzi Bora wa Mwaka Taarab ameshinda >Mzee Yusuph
go
#FahamuKTMA2015 Tuzo ya Mtunzi Bora wa Mwaka Muziki wa Bongo Fleva ameshinda> Ali Kiba.

#FahamuKTMA2015 Tuzo ya Mtunzi Bora wa Mwaka muziki wa Bendi ameshinda > Jose Mara

#FahamuKTMA2015 Tuzo ya Msanii Bora Chipukizi ameshinda >Baraka Da Prince

#FahamuKTMA2015 Tuzo ya Mtunzi Bora wa Mwaka Hip Hop imeshindwa na >Joh Makini

#FahamuKTMA2015 Tuzo ya Bendi Bora ya Mwaka wameshinda> FM Academia

#FahamuKTMA2015 Tuzo ya Mtayarishaji Bora wa Nyimbo wa Mwaka Muziki wa Bongo Fleva ameshinda > Nahreel

#FahamuKTMA2015 Tuzo ya Mtayarishaji Bora wa Nyimbo wa Mwaka Taarab ameshinda> Enrico

#FahamuKTMA2015 Tuzo ya Mtayarishaji Bora wa Nyimbo wa Mwaka Bendi ameshinda> Amoroso

#FahamuKTMA2015 Tuzo ya Wimbo Bora Wenye Vionjo vya Asili ya Kitanzania ameshinda> Mrisho Mpoto

#FahamuKTMA2015 Kikundi Bora cha Mwaka Muziki wa Taarab wameshinda  >Jahazi Modern Taarab

#FahamuKTMA2015 Kikundi Bora cha Mwaka Muziki Wa Bongo Fleva Wameshinda >Yamoto Band

Friday, June 5, 2015

SAMWEL SITTA ACHUKUA FOMU, ATAKA MIAKA 5 TU KUWANG'OA WATU HAWA




Waziri wa Uchukuzi Samweli Sitta akionesha fomu ya kugombea urais mara katika ukumbi wa NEC makao makauu Dodoma.

  

Waziri wa Uchukuzi Mh. Samweli Sitta akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kuchukua fomu leo.

Waziri wa Uchukuzi  Mh. Samweli Sitta leo  amechukua fomu ya kugombea urais kwa tiketi ya  chama cha Mapinduzi makao makuu ya CCM yaliyopo White House  Dodoma  mjini. Sitta ameambatana na Mke wake pamoja na wapambe wake.

Akizungumza mara baada ya kupokea fomu Sitta amesema kwamba  anaomba   miaka mitano tu sio zaidi ili aweze kuwashughulikia ipasavyo mafisadi na kumaliza kabisa tatizo la ufisadi  unao onekana kukwamisha maendeleo ya ya  nchi Hivisasa.

Aidha, ametaja vipaumbele vyake kuwa ni;

(i) Kuulinda muungano
(ii)  Kumalizia mchakato wa katiba Pendekezwa
(iii)  Kumaliza kabisa suala la Rushwa
(iv) Kuleta mahusiano mazuri kati ya  Wafanyabiashara na Serikali
(v) Kuimarisha Chama