Saturday, March 29, 2014

MAMA SHARO AMVAA KITALE KWA TUHUMA NZITO ZA AIBU

MAKUBWA NA MAZITO HAYA....MAMA
SHARO MILIONEA AMVAA KITALE KWA
TUHUMA NZITO NA ZA AIBU...!
Mama yake na marehemu Hussein Mkieti
aka ‘Sharo Milionea’ . Makubwa! Mama
mzazi wa aliyekuwa nyota wa filamu na
muziki, marehemu Hussein Mkieti ‘Sharo
Milionea’ amemtuhumu msanii wa vichekesho
ambaye alikuwa rafiki wa mwanaye, Musa
Kitale kuwa alikula michango ya
kumbukumbu ya kifo cha mwanaye, mwaka
jana.
Kwa mujibu wa chanzo makini, Mama Sharo
amekuwa akimlalamikia Kitale kwa watu
kwamba alikula fedha za mchango wa
mwanaye hivyo kupigwa marufuku kwamba
kitu chochote kinachomhusu Sharo asipewe.
Ilidaiwa kwamba, chanzo cha mama Sharo
kutaka Kitale asipewe kitu chochote
kinachomhusu marehemu ni baada ya hivi
karibuni Klabu ya Bongo Movie Unity
kutangaza kuwa litatoa Tuzo kwa Sharo
Milionea kama kumbukumbu kwani alikuwa ni
mwenzao katika tasnia ya filamu.
Ilisemekana kuwa mama huyo alielezwa
kwamba tuzo hiyo itapokelewa na Kitale
ndipo alipokataa na kusema hataki kabisa
kitu chochote kipitie kwa msanii huyo kwa
sababu huwa hamfikishii.
Msanii wa vichekesho Musa Kitale.
“Mama Sharo amekuwa akilalamika kwa
muda mrefu sana kwamba Kitale anatumia
vitu vya mwanaye, eti alichangisha michango
ya kumbukumbu hakumfikishia hivyo kwa
sasa ameamua kupiga marufuku asikabidhiwe
kitu chochote,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kupata habari hizo, wanahabari
wetu walimtafuta Kitale ambapo kabla hata
ya kujibu tuhuma hizo, alinyanyua simu na
kumpigia mama Sharo kumuuliza kama kweli
amezungumza madai hayo.
Mama Sharo alikiri kuwa ni kweli
alizungumza akidai alifikia uamuzi huo baada
ya kutonywa na watu kuwa Kitale amekuwa
‘akichikichia’ fedha za marehemu mwanaye.
Kitale, baada ya kujiridhisha, alitoa ufafanuzi
kuwa madai hayo hayana ukweli na
kudadavua kwamba wakati wa kumbukumbu
ya Sharo mwaka mmoja (Novemba) tangu
alipofariki dunia, hakuna michango yoyote
iliyotolewa.
“Inaniuma sana kwa sababu enzi za uhai wa
Sharo hatukuwahi kugombana hata siku moja
na mama Sharo alikuwa analitambua hilo,
tuliishi kama ndugu na mimi ndiye
niliyemsaidia mpaka akapata umaarufu lakini
sasa namshangaa huyu mama kunishutumu
vitu vya uongo,” alisema Kitale kwa huzuni
huku jasho likimtiririka.

Thursday, March 27, 2014

HUU NI MZIGO MPYA WA PRO-JAY AKIMSHIRIKISHA DIAMOND PLATNUMZ

Hapo awali mtu mzima Daddy (Prof. Jay) aliwahi kutoa picha akiwa studio kwa P-funk Majani akiwa pamoja na Diamond Platnumz, katika maelezo ya picha hizo Prof alisema tukae mkao wa kusikiliza "kolabo" kali kati yake na Diamond Platnumz ingawa hakusema jina la wimbo utaitwaje,

Hatimaye Prof. Jay ameachia Official Cover litalohusika katika track yake mpyaaaaa itayokujia hivi karibuni katika masikio yako akiwa kashirikiana na Diamond Platumz. wimbo uliyoandikwa kwenye Cover hilo unakwenda kwa jina la "KIPI SIJASIKIA"

WEMA NA AUNT EZEKIEL WATIA KINYAA

Uchafu! Picha za madiva wakubwa wa filamu
Tanzania, Wema Isaac Sepetu na Aunt
Ezekiel Grayson zimebambwa na gazeti hili
hivi karibuni wakiwa katika hali ya
kimalavidavi licha ya kwamba, mmoja ni mke
wa mtu, mwingine mchumba.
Kwa mujibu wa mnyetishaji wetu, ishu hiyo
ilichukua nafasi maeneo ya Mikocheni jijini
Dar es Salaam ambako Wema na Aunt
wamepiga kambi kwa ajili ya filamu yao
mpya ya Familia.
Ilidaiwa kuwa, Wema na Aunt ambao kwa
sasa wapo ‘klozdi’ kiasi cha watu kuwa na
maswali vipi kuhusu Kajala Masanja, walipiga
picha hizo wak i dhamiria kuzifuta baada ya
kujiona lakini lililotokea si akili zao, picha
hizo zikanaswa na paparazi wetu.
Staa wa filamu Tanzania, Wema Isaac
Sepetu
Juzi, Amani liliwatafuta kwa njia ya simu
wawili hao na kuwauliza nini kiliwatia nguvu
hadi kupiga picha hizo ambapo Wema
anaonekana akibusu sehemu ya paji la uso la
Aunt huku naye akiwa amelegeza macho
kusikilizia.
Wema: “Unajua huyu Aunt ni mtu ambaye
tumezoeana kupita kiasi, tunapomaliza
kufanya kazi, tunaanza utani. Halafu kwetu
mbona mabusu ni ishu ya kawaida sana!”
Habari za ndani zinasema, baadhi ya ndugu
wa mume wa Aunt, Sunday Dimonte
wamekuwa wakimtumia meseji ‘mista’ huyo
kumweleza uchafu mbalimbali anaofanya
mume wake licha ya kutotoa tamko lolote.
Diva wa filamu za kibongo Aunt Ezekiel
Mbali na Dimonte, baadhi ya watu
waliozungumza na Amani walimtaka Nasibu
Abdul ‘Diamond’ kukaa chini na kufikiri upya
kuhusu uamuzi wake wa kumuoa Wema.
Wengi wanaamini si sahihi kwake kwa vile
haonekani ‘kutulia’ licha ya kwamba wote
‘hawajatulia’

Tuesday, March 25, 2014

UJUMBE MKALI

Ukiona unatumia nguvu nyingi kumchafua mtu kwa kumpakazia mambo, kumsengenya, kumfitanisha, na kumsingizia ujue ye ni bora kuliko wewe
Kichafu chaonekana hata bila kuambiwa.

Monday, March 24, 2014

Friday, March 21, 2014

KARIBU JK BOY BLOG

Kwa habari mbalimbali zinazotokea ndani na nje ya nchi tembelea JK BOY BLOG.
Huku utapata kujua matukio mbalimbali ya kusisimua pamoja na matangazo mbalimbali ya kibiashara.
Kuwa wa kwanza kupata habari kwa kutembelea JK BOY BLOG!...
                                                     By
                                                      Admin!