Uchafu! Picha za madiva wakubwa wa filamu
Tanzania, Wema Isaac Sepetu na Aunt
Ezekiel Grayson zimebambwa na gazeti hili
hivi karibuni wakiwa katika hali ya
kimalavidavi licha ya kwamba, mmoja ni mke
wa mtu, mwingine mchumba.
Kwa mujibu wa mnyetishaji wetu, ishu hiyo
ilichukua nafasi maeneo ya Mikocheni jijini
Dar es Salaam ambako Wema na Aunt
wamepiga kambi kwa ajili ya filamu yao
mpya ya Familia.
Ilidaiwa kuwa, Wema na Aunt ambao kwa
sasa wapo ‘klozdi’ kiasi cha watu kuwa na
maswali vipi kuhusu Kajala Masanja, walipiga
picha hizo wak i dhamiria kuzifuta baada ya
kujiona lakini lililotokea si akili zao, picha
hizo zikanaswa na paparazi wetu.
Staa wa filamu Tanzania, Wema Isaac
Sepetu
Juzi, Amani liliwatafuta kwa njia ya simu
wawili hao na kuwauliza nini kiliwatia nguvu
hadi kupiga picha hizo ambapo Wema
anaonekana akibusu sehemu ya paji la uso la
Aunt huku naye akiwa amelegeza macho
kusikilizia.
Wema: “Unajua huyu Aunt ni mtu ambaye
tumezoeana kupita kiasi, tunapomaliza
kufanya kazi, tunaanza utani. Halafu kwetu
mbona mabusu ni ishu ya kawaida sana!”
Habari za ndani zinasema, baadhi ya ndugu
wa mume wa Aunt, Sunday Dimonte
wamekuwa wakimtumia meseji ‘mista’ huyo
kumweleza uchafu mbalimbali anaofanya
mume wake licha ya kutotoa tamko lolote.
Diva wa filamu za kibongo Aunt Ezekiel
Mbali na Dimonte, baadhi ya watu
waliozungumza na Amani walimtaka Nasibu
Abdul ‘Diamond’ kukaa chini na kufikiri upya
kuhusu uamuzi wake wa kumuoa Wema.
Wengi wanaamini si sahihi kwake kwa vile
haonekani ‘kutulia’ licha ya kwamba wote
‘hawajatulia’
Thursday, March 27, 2014
WEMA NA AUNT EZEKIEL WATIA KINYAA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment