Saturday, March 29, 2014

MAMA SHARO AMVAA KITALE KWA TUHUMA NZITO ZA AIBU

MAKUBWA NA MAZITO HAYA....MAMA
SHARO MILIONEA AMVAA KITALE KWA
TUHUMA NZITO NA ZA AIBU...!
Mama yake na marehemu Hussein Mkieti
aka ‘Sharo Milionea’ . Makubwa! Mama
mzazi wa aliyekuwa nyota wa filamu na
muziki, marehemu Hussein Mkieti ‘Sharo
Milionea’ amemtuhumu msanii wa vichekesho
ambaye alikuwa rafiki wa mwanaye, Musa
Kitale kuwa alikula michango ya
kumbukumbu ya kifo cha mwanaye, mwaka
jana.
Kwa mujibu wa chanzo makini, Mama Sharo
amekuwa akimlalamikia Kitale kwa watu
kwamba alikula fedha za mchango wa
mwanaye hivyo kupigwa marufuku kwamba
kitu chochote kinachomhusu Sharo asipewe.
Ilidaiwa kwamba, chanzo cha mama Sharo
kutaka Kitale asipewe kitu chochote
kinachomhusu marehemu ni baada ya hivi
karibuni Klabu ya Bongo Movie Unity
kutangaza kuwa litatoa Tuzo kwa Sharo
Milionea kama kumbukumbu kwani alikuwa ni
mwenzao katika tasnia ya filamu.
Ilisemekana kuwa mama huyo alielezwa
kwamba tuzo hiyo itapokelewa na Kitale
ndipo alipokataa na kusema hataki kabisa
kitu chochote kipitie kwa msanii huyo kwa
sababu huwa hamfikishii.
Msanii wa vichekesho Musa Kitale.
“Mama Sharo amekuwa akilalamika kwa
muda mrefu sana kwamba Kitale anatumia
vitu vya mwanaye, eti alichangisha michango
ya kumbukumbu hakumfikishia hivyo kwa
sasa ameamua kupiga marufuku asikabidhiwe
kitu chochote,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kupata habari hizo, wanahabari
wetu walimtafuta Kitale ambapo kabla hata
ya kujibu tuhuma hizo, alinyanyua simu na
kumpigia mama Sharo kumuuliza kama kweli
amezungumza madai hayo.
Mama Sharo alikiri kuwa ni kweli
alizungumza akidai alifikia uamuzi huo baada
ya kutonywa na watu kuwa Kitale amekuwa
‘akichikichia’ fedha za marehemu mwanaye.
Kitale, baada ya kujiridhisha, alitoa ufafanuzi
kuwa madai hayo hayana ukweli na
kudadavua kwamba wakati wa kumbukumbu
ya Sharo mwaka mmoja (Novemba) tangu
alipofariki dunia, hakuna michango yoyote
iliyotolewa.
“Inaniuma sana kwa sababu enzi za uhai wa
Sharo hatukuwahi kugombana hata siku moja
na mama Sharo alikuwa analitambua hilo,
tuliishi kama ndugu na mimi ndiye
niliyemsaidia mpaka akapata umaarufu lakini
sasa namshangaa huyu mama kunishutumu
vitu vya uongo,” alisema Kitale kwa huzuni
huku jasho likimtiririka.

No comments:

Post a Comment