Wednesday, May 20, 2015

MAPAMBANO YATOKEA MKOANI NJOMBE KATI YA POLISI NA RAIA

Mapigano makali yanaendelea sasa mjini Njombe kati ya wananchi
na polisi tangu asubuhi.
Mtangazaji wa Kings FM ya Njombe, King David, ametutumia taarifa
ifuatayo:
Jana usiku wa saa 3 polisi wa doria walikua mtaani wakapita mtaa
mmoja unaitwa Nzenge kuna kilabu cha pombe za kienyeji
wakawakuta watu mle ndani. Sasa katika kuwauliza kwanini wapo
eneo hilo mpaka muda wa usiku, wananchi wakajibu kuwa muda wa
kufunga ni saa 4 na ndio utaratibu ofcoz (Kufunga saa 4) wale polisi
hawakuridhishwa na majibu na kuamua kuwatimua wananchi pale
ndani lakini jamaa hawakutii. Polisi wakafyatua risasi ambayo
ilimpata mwananchi mmoja na kumuua pale pale huku mmoja
akijeruhiwa.
Then polisi wakaondoka baada ya tukio hilo bila msaada wowote.
Wananchi wakapanic na ilipofika asubuhi leo wananchi wa mtaa ule
pamoja na vijana wa boda boda wakaanza maandamano kwenda
kituo cha polisi cha mkoa wakiwa wanatamka maneno makali sana
ikiwa ni pamoja na kuwataka polisi wachukue mwili wa marehemu
na kuuzika wao pamoja na kutoa sababu za kufanya mauaji hayo.
Polisi wakaanza kuwatimua tena lakini wananchi wakagoma ndo
hapo polisi walipoamua kutumia nguvu ya ziada ikiwa ni pamoja na
kupiga mabomu ya machozi na risasi hewani. Bado wananchi
walikua wagumu kuelewa mpaka walipoamua kuanza kuwapigwa
kwa virungu, fimbo na mateke.
Polisi wametoa tahadhari ya watu kutotoka nje na kuna dereva
mmoja amepigwa risasi tena mchana huu kauawa pia kuna baadhi
ya polisi wamejeruhiwa kwa mawe na mapanga kutoka kwa
wananchi.
Kwasasa hakuna mtu anaruhusiwa kutoka nje.

Monday, May 4, 2015

WAZIRI MKUU AUNDA KAMATI KUSHUGHULIKIA USAFIRI

WAZIRI MKUU AUNDA KAMATI KUSHUGHULIKIA
USAFIRI

Waziri Mkuu , Mizengo Peter Pinda ameunda kamati maalumu ya
kudumu ya kusimamia Usafiri wa barabarani nchini ili kutatua
changamoto zinazoikabali sekta ya Usafiri .
Katika kamati hiyo mwenyekiti wake atakuwa katibu mkuu wa
wizara ya chukuzi, Katibu akiwa kamishna wa polisi barabarani
na Mkurugenzi wa SUMATRA huku wajumbe wakiwa ni pamoja
na katibu mkuu wizara ya kazi ya na ajira , katibu mkuu ujenzi,
mwanasheria mkuu wa serikali na naibu katibu mkuu ofisi ya
waziri mkuu .
Mkuu wa ratibu wa idara ya maafa toka ofisi ya waziri mkuu ,
mwenyekiti wa TABOA na TATOA , CHAKUA na wanatakiwa
kuanza kufanya vikao leo na kila mwezi watakutana kujadili na
kutatua changamoto zote kasoro zile za kisheria ambazo
zitapelekwa serikalini kwa mchakato zaidi wa kuzirekebisha.
Wakati huo huo umoja wa vyama vya madereva nchini Tanzania
umesema hauna taarifa juu ya wao kutakiwa kukutana na waziri
mkuu Mh . Mizengo Pinda kwa ajili ya mazungumzo kama
inavyozungumzwa na kusisitiza kuwa wao wataendelea na
mgomo wao ulioanza leo mpaka masuala yao yatapofanyiwa
kazi .
Akizungumza na East Africa Radio leo Makamu Mwenyekiti wa
Muungano wa vyama vya Madereva Abdallah Lubala amesema
kauli ya kuwa wamekubaliana kukutana na Mh. Pinda ni za
kisiasa na hazina ukweli wowote hivyo wataendelea na mgomo
wao.
Wakati huo huo mgomo huo ambao umetangazwa kwa nchi
nzima athari zake zimejitokeza katika mikoa mingine tofauti
ambapo madereva wa mabasi ya abiria wamegoma huku
wasafiri wakitumia usafiri mbadala wa bajaji pamoja bodaboda .
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wakazi wa jiji la
Mbeya , Arusha na Mwanza wamesema kuwa wanalazimika
kutembea umbali mrefu kwenda makazini na wangine wakitumia
gharama kubwa kutokana na vyombo hivyo wanavyotumia
kupandisha bei za nauli kuliko kawaida .
( CHANZO : EAST AFRICA RADIO )

Saturday, May 2, 2015

FLOYD MAYWEATHER AMDUNDA PACQUIAO

Floyd Mayweather amemdunda Manny Pacquiao kwa
points baada ya pambano la dunia lililokuwa
likisubiriwa kwa hamu kumalizika huko jijini Las
Vegas.
Pacquiao kama ilivyokuwa ikitarajiwa alirusha ngumi
nyingi zaidi kuliko mpinzani wake lakini Mayweather
aliweza kurusha ngumu zenye faida zaidi
zilizowafanya majaji wanne wampe ushindi.
Mayweather ameshinda kwa point 118-110, 116-112,
116-112. Kwa ushindi huo, Mayweather ameendelea
kushikiliza rekodi yake ya kutowahi kushindwa katika
mapambano yake 48 aliyowahi kupigana.
Tazama picha za pambano hilo.