Saturday, July 26, 2014

DIAMOND ASHINDA TUZO MBILI

Wanaziita African Muzik Magazine Awards
ambapo za mwaka huu 2014 zimetolewa huko
Eisemann center Texas Marekani na
kuhudhuriwa na mastaa mbalimbali akiwemo
Diamond wa Tanzania ambae pia alikua
mmoja wa wanaowania tuzo.
Good news kwa mujibu wa meneja Babu Tale
ni kwamba Diamond ameshinda tuzo mbili
moja ya Msanii bora wa Afrika Mashariki na
nyingine ni wimbo bora wa kushirikiana ambao
ni ‘number one rmx’ alioufanya na Davido wa
Nigeria.
Stori zaidi na pichaz vitafata baadae hivyo
endelea kukaa karibu na millardayo.com mtu
wangu ili ujue kilichotokea kwenye tukio hili
ambalo limewahusisha wakali wengine kama
Davido, 2Face, Fally Ipupa, Iyanya, Flavour,
Wyre, Miriam Chemmoss na wengine ambao ni
sehemu ya watu kutoka nchi 17 za Afrika.

Sunday, July 20, 2014

DUH! DUNIA HII HATARI ONA MWENYEWE

Bora uwe na hamsini nzima kuliko mia mbovu. Vijana hawa walikua wakiiba wakakamatwa na wananchi wenye hasira kali na kuwekwa taili za gari na kuchomwa moto.

Friday, July 18, 2014

Lol!! VIDEO YA H-BABA IMEMGHARIMU LAKI NA NUSU

Video mpya ya H-Baba
imemgharimu Laki na Nusu tu
Star mwenye vipaji vingi nchini Tanzania H-
Baba amesema ukweli kuhusiana na gharama
zilizomgharimu katika video yake mpya ya
"Tubebane" itakayotoka hivi karibuni.
H amesema haina haja ya kuongea uongo ama
kudanganya Mashabiki wake kwa swala la
gharama. Amefafanua kuwa Video Production
amepewa bure. Pia ameoneshwa kukerwa na
wasanii wengine wanaodanganya kuwa
wamefanya video kwa gharama kubwa sana
kumbe wamefanyiwa bure, amekiri kuwa video
za gharama zipo hata ukitazama zinaonekana ila
wengi ni waongo.
Kwa hiyo mashabiki wote wa H-Baba muipokee
video hiyo ya "Tubebane"