Video mpya ya H-Baba
imemgharimu Laki na Nusu tu
Star mwenye vipaji vingi nchini Tanzania H-
Baba amesema ukweli kuhusiana na gharama
zilizomgharimu katika video yake mpya ya
"Tubebane" itakayotoka hivi karibuni.
H amesema haina haja ya kuongea uongo ama
kudanganya Mashabiki wake kwa swala la
gharama. Amefafanua kuwa Video Production
amepewa bure. Pia ameoneshwa kukerwa na
wasanii wengine wanaodanganya kuwa
wamefanya video kwa gharama kubwa sana
kumbe wamefanyiwa bure, amekiri kuwa video
za gharama zipo hata ukitazama zinaonekana ila
wengi ni waongo.
Kwa hiyo mashabiki wote wa H-Baba muipokee
video hiyo ya "Tubebane"
Friday, July 18, 2014
Lol!! VIDEO YA H-BABA IMEMGHARIMU LAKI NA NUSU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment