Saturday, July 26, 2014

DIAMOND ASHINDA TUZO MBILI

Wanaziita African Muzik Magazine Awards
ambapo za mwaka huu 2014 zimetolewa huko
Eisemann center Texas Marekani na
kuhudhuriwa na mastaa mbalimbali akiwemo
Diamond wa Tanzania ambae pia alikua
mmoja wa wanaowania tuzo.
Good news kwa mujibu wa meneja Babu Tale
ni kwamba Diamond ameshinda tuzo mbili
moja ya Msanii bora wa Afrika Mashariki na
nyingine ni wimbo bora wa kushirikiana ambao
ni ‘number one rmx’ alioufanya na Davido wa
Nigeria.
Stori zaidi na pichaz vitafata baadae hivyo
endelea kukaa karibu na millardayo.com mtu
wangu ili ujue kilichotokea kwenye tukio hili
ambalo limewahusisha wakali wengine kama
Davido, 2Face, Fally Ipupa, Iyanya, Flavour,
Wyre, Miriam Chemmoss na wengine ambao ni
sehemu ya watu kutoka nchi 17 za Afrika.

No comments:

Post a Comment