Je? Huyu mwalimu yupo sahihi
Monday, April 28, 2014
Tuesday, April 22, 2014
KOCHA MKUU WA KLABU YA MANCHESTER UNITED DAVID MOYES ATIMULIWA
Kocha mkuu na meneja wa wa klabu
ya Manchester United David Moyes
ametimuliwa.
Meneja wa klabu ya Manchester
United David Moyes amefutwa kazi
baada ya kushikilia usukuni wa
klabu hiyo kwa miezi kumi tu.
Klabu hiyo hapo awali ilikuwa
imekataa kuzungumzia udaku wa
magezti kuwa Moyes atafutwa kazi
kabla ya msimu kumalizika.
Moyes, mwenye umri wa miaka 50,
aliteuliwa na Ferguson kumrithi
alipostaafu mwaka jana baada ya
kuwa na klabu hiyo kwa miaka 26.
HABARI KAMILI KUHUSU MOYES
KUTIMULIWA MAN U.. SOMA HAPO
CHINI..
Mkufunzi mkuu na meneja wa klabu
ya Manchester United David Moyes
ametimuliwa.
David Moyes amefutwa kazi baada
ya kushikilia usukuni wa klabu hiyo
kwa miezi kumi tu.
Klabu hiyo hapo awali ilikuwa
imekataa kuzungumzia udaku wa
magezti kuwa Moyes atafutwa kazi
kabla ya msimu kumalizika.
Moyes, mwenye umri wa miaka 50,
aliteuliwa na Ferguson kumrithi
alipostaafu mwaka jana baada ya
kuwa na klabu hiyo kwa miaka 26.
Taarifa kutoka kwa klabu hiyo
imemshukuru Moyes kwa bidii,
uaminifu na hekima aliyoonyesha
kocha huyo akiwa mkufunzi wa
Manchester United.
Moyes alichukuwa usukani wa
kuifunza Manchester United mwaka
uliopita baada ya aliyekuwa kocha
wa siku nyingi Sir. Alex Ferguson
kustaafu.
Huku zikiwa zimesalia mechi nne
pekee msimu wa ligi kukamilika
Mancheseter united inashikilia
nafasi ya saba kwenye jedwali la
msimamo wa ligi hiyo alama ishirini
na tatu nyuma ya viongozi Liverpool.
Klabu hiyo imeshindwa kufuzu
kushiriki michuano ya ligi ya
mabingwa ulaya kwa mara ya
kwanza katika kipindi cha takriban
miaka ishirini.
Sunday, April 20, 2014
SASA HUKU KUFURU WAZIMIA
KAMA NI USHABIKI SASA HUU UMEZIDI NI
KWENYE PAMABANO LA WATANI WA JADI
HIVI HAPA...!! HATARI SANA TAZAMA PICHA
AKINA DADAHAWA WA YANGA W
KUZIMIA WAKATI WA PAMBANO
JADI..
Friday, April 18, 2014
BREAKING NEWZ: MELI YAZAMA ZIWA VICTORIA HIVI PUNDE
BREAKING NEWS: MELI YAZAMA
ZIWA VICTORIA HIVI PUNDE
Meli ya mizigo ya Kampuni ya FB Matara
iliyokuwa inatoka Bukoba kwenda Mwanza ikiwa
na wafanyakazi kumi na shehena ya sukari
imezama ziwa victoria katikati ya visiwa vya
Kerebe na Bumbile.
Taarifa kamili itakujia baadaye
Sunday, April 13, 2014
DAH!! MAJANGA MZEE GURUMO AFARIKI DUNIA
BreakingNews, Ent. , stori kubwa
Tweet 20 418 Like
0
Breaking: Kuhusu mwanamuziki
mkongwe mzee Gurumo kufariki
dunia.
Ni mzee wa siku nyingi sana kwenye muziki
Tanzania ambae aliwahi kuingia kwenye
vichwa vya habari mara nyingi hasa kutokana
na kuugua kwake kuliko mfanya aache hata
muziki aliokua anaufanya.
Taarifa zilizothibitishwa na hospitali ya Taifa
Muhimbili kwa millardayo.com zimesema Mzee
huyu amefariki dunia akiwa hospitalini hapo leo
April 13 2014 saa nane mchana baada ya
kuletwa jana asubuhi na kulazwa kwenye wodi
namba 6 ya Mwaisela kutokana na kuzidiwa.
Tayari mwili wake umepelekwa kwenye chumba
cha kuhifadhia maiti ambapo taarifa zaidi
kuhusu chanzo cha kifo na taratibu za mazishi
millardayo.com itaendelea kuzitoa kupitia
@millardayo kwenye twitter instagram na
facebook.
Friday, April 11, 2014
JOHARI ATEMA CHECHE" SIJAWAHI SINA NA WALA SIWEZI KUWA NA UHUSIANO NA MPUUZI MKUBWA
JOHARI ATEMA
CHECHE.."SIJAWAHI ,SINA NA
WALA SIWEZI KUWA NA
UHUSIANO NA MTU MPUUZI
KAMA YULE...."NI SHIDAAA
AISEEE....!
NI mtafutano! Staa mkubwa wa sinema
za Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’
ameingia kwenye vita ya maneno na
bosi wa Mtanashati Entertainment,
Ostaz Juma Namusoma ikiwa ni siku
chache tangu jamaa huyo alipotangaza
kumuoa mwanadada huyo.
Staa mkubwa wa sinema za Bongo,
Blandina Chagula ‘Johari’.
Wakizungumza na Risasi Jumamosi kwa
nyakati tofauti, kila mmoja alitoa la
moyoni huku Johari akionekana
kukasirishwa mno na ishu hiyo.
KILICHOMPONZA JOHARI
Ilidaiwa kuwa baada ya Ostaz
kutangaza kwamba atafunga ndoa na
Johari, vyombo mbalimbali vya habari
na mitandao ya kijamii vililichukulia
jambo hilo kwa ukubwa wake kwani
mwanadada huyo hakufunguka
sawasawa.
WENGINE WADAI KULIPA KISASI
Habari zinasema baada ya ishu hiyo
kugeuka habari ya mjini ilidaiwa
kwamba labda Johari aliamua kufanya
hivyo kwa kuwa mkurugenzi mwenzake
wa RJ Film Production ‘RJ’, Vincent
Kigosi ‘Ray The Greatest’ naye alidaiwa
‘kuchepuka’ na Chuchu Hans.
Bosi wa Mtanashati Entertainment, Ostaz
Juma.
Kuenea kwa habari za Johari kuolewa
na Ostaz kulimsababishia usumbufu
mkubwa mwanadada huyo kutoka kwa
ndugu, jamaa na marafiki wakihoji
ukweli wa ishu hiyo ili kujiandaa na
cherekochereko.
MADAI YA AWALI YA OSTAZ
Katika maelezo yake ambayo yapo
kwenye rekodi zetu, Ostaz alidai kuwa
Johari anajua kila kitu kwani
walifahamiana kitambo hata kabla ya
mrembo huyo kujuana na Ray.
Hakuishia hapo, Ostaz alidai kuwa
tayari amemfungulia Johari kampuni ya
kutengeneza sinema pamoja na vifaa
vyote hivyo yupo kwenye mishemishe
za kumuoa.
JOHARI SASA
Ili kuondoa utata huo, gazeti hili
lilimtafuta Johari kwa udi na uvumba
na kutaka kujua undani wa ishu hiyo
ambayo imezua maswali mengi hasa
kwa mashabiki wake.Johari: Sijawahi,
sina na wala siwezi kuwa na uhusiano
na mtu mpuuzi kama yule (Ostaz Juma).
Mwanzoni nilidhani utani, nashangaa
imekuwa ishu kubwa.
Risasi Jumamosi: Kwani hufahamiani
na Ostaz? Mbona anasema anakujua
tangu unaishi Mburahati, Dar na enzi
ukiwa Kaole?
Johari: Ni kweli Ostaz alikuwaga
anakuja pale Kaole tulipokuwa
tunafanya mazoezi lakini si yeye
waliokuwa wanakuja ni wengi.
Risasi Jumamosi: Je, hajawahi kuleta
maombi ya kukuoa?
Johari: Hakuwahi kunitongoza ila kila
nilipokutana naye nilikuwa najua kwa
kumwangalia tu machoni. Alikuwa
anaonesha kabisa ananitaka lakini
hakuwahi kunitamkia.
“Hajawahi kuniambia anataka kunioa.
Kwanza mimi ni Mkristo. Sina ndoa
mbili. Siwezi kuolewa mke wa pili na
mpuuzi kama yeye.
Risasi Jumamosi: Je, zile picha
zilizosambaa ukiwa umepozi kimahaba
na Ostaz zilitoka wapi?
Risasi Jumamosi: Ilikuwa nje ya RJ,
nilipiga picha na watu wengi kama
Dogo Janja akiwemo na huyo Ostaz.
Nilipigwa na butwaa nilipoziona
mitandaoni eti nina uhusiano na Ostaz
huku naye akiulizwa na kudai ni kweli.
“Kwani kupiga picha na mtu ndiyo
tayari mmekuwa wapenzi au
wachumba? Labda yeye anachukulia
hivyo kwamba ukishapiga picha na
mwanamke tayari anakuwa mpenzi
wako.”
Risasi Jumamosi: Kuhusu dini, Ostaz
alisema atakubali uwe Mwislamu na
jina lako litakuwa Rahma. Je,
alishakuambia juu ya hilo?
Johari: Hajaniambia, hata hivyo, sina
mpango wa kubadili dini ili niolewe na
yeye.
Risasi Jumamosi: Vipi kuhusu Ostaz
kukufungulia kampuni na vifaa vya
kutengenezea sinema?
Johari: Mh! Achana na kampuni au
vifaa, hata simu tu hajawahi
kuninunulia, kwanza hana fedha.
Halafu ajue kabisa kwamba mimi ni
tofauti na hao wasanii wengine
wanaoishi kwa kutegemea kuhongwa.
Mimi ni super woman, siku hizi huwa
fedha kwangu ni makaratasi. Huyo
Ostaz ana fedha gani?
“Haniwezi, mimi siyo kama hao watoto
anaowadhalilisha kwa kuwapigisha
magoti na akome kabisa kutumia jina
langu kama daraja. Hakuna kitu
ninachochukia kama mtu kutaka
kutumia jina langu kujitafutia
umaarufu, ana hadhi gani ya kuwa na
mimi, akome kabisa, mimi nimesota,
ninyi Global mnajua.”
Risasi Jumamosi: Umekana kuwa na
uhusiano wa kimapenzi na Ostaz, je,
una mchumba au mpenzi?
Johari: Mimi ni mwanamke
niliyekamilika. Nina mchumba na
‘soon’ nitamtambulisha kwa mashabiki
wangu. Lakini ijulikane kuwa siyo Ostaz
kwani hawezi kuwa mchumba wangu.
Risasi Jumamosi: Au unataka kurudi
kwa Ray?
Johari: (mshtuko) hivi ni nani aliwahi
kutamka kwamba mimi na Ray ni
wapenzi. Hapana, siyo Ray.
Risasi Jumamosi: Kwani Ray ni nani
kwako?
Johari: Ray ni mkurugenzi mwenzangu
wa RJ. Nje ya kazi tuna maisha yetu
mengine.
Risasi Jumamosi: Je, ni mtu maarufu?
Johari: Nimeshasema nitawatambulisha
subirini. Unajua mimi siyo mtu wa
matangazo.
Baada ya kumsikia Johari, gazeti hili
lilimgeukia Ostaz ambaye hakupatikana,
lakini rafiki yake wa karibu alidai kuwa
Johari amechanganyikiwa kwani Ostaz
alikuwa amuoe kweli lakini hamuelewi
mwenendo wake wa sasa.
“Johari amechanganyikiwa,” alisema
rafiki huyo.
Tuesday, April 8, 2014
KIPI KIZURI KWA MTOTO KATI YA HAYA
(1).kulelewa na mamal.
(2).kulelewa na bibi
(3).kulelewa na baba
(4).kulelewa na mama
(5).kulelewa na mama na baba
NJEMBA YABAKA MTOTO WA MIAKA MINNE
NI AIBU! Jamaa mmoja anayejulikana kwa
jina la Iddi Mgosi anashikiliwa na Polisi wa
Kituo cha Wazo jijini Dar es Salaam kwa
tuhuma za kumbaka mtoto mwenye umri wa
miaka minne (jina linahifadhiwa) huko
Mivumoni, Madale Machi 18, mwaka huu.
Mtoto wa miaka minne aliyefanyiwa unyama
huo.
Mgosi, ambaye umri wake haukuweza
kupatikana mara moja, anadaiwa kumrubuni
mtoto huyo kutoka nyumbani kwao na
kumpeleka kwake, ambako alimuingilia kwa
nguvu na baadaye kumtisha kutosema lolote
kwa wazazi wake.
Mama mzazi wa mtoto huyo, aligundua
mwanaye kuwa na maumivu makali wakati
akimuogesha, kwani alipomshika sehemu
zake za siri, binti huyo alipiga kelele za
maumivu na alipoulizwa kilichomsibu ndipo
alipoelezea alichofanyiwa.
Akizungumza kwa masikitiko makubwa,
mama huyo aitwaye Hadija, alisema alikuwa
akimuogesha mtoto wake huyo bila kugundua
kwamba alikuwa amebakwa na kuharibiwa
vibaya sehemu zake za siri. Alipomshika kwa
ajili ya kumsafisha, mtoto huyo akaanza kulia
na kulalamika kwamba alikuwa akimuumiza.
Bi Hadija alisema mara baada ya kuambiwa
hivyo, akawaita ndugu zake na kuwasimulia
alichoambiwa hivyo wote kwa pamoja
wakachukua jukumu la kumfuata Mgosi,
kumkamata na kumpeleka katika Kituo cha
Polisi Wazo.
Baada ya kumuogesha binti yake,
wakampeleka katika hospitali ya
Mwananyamala alikochukuliwa vipimo
kadhaa na kuambiwa wampeleke mtoto huyo
katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
“Hospitalini walituambia kwamba sehemu
zake za siri zimeharibiwa sana na hata kibofu
chake cha mkojo pia kimeharibiwa kwani
wametoa uchafu mwingi. Kwa sasa
amelazwa hospitalini huku akiendelea
kupatiwa matibabu na hawajajua ni siku gani
ataruhusiwa.”
MTOTO AFUNGUKA
Waandishi wetu hawakuishia hapo,
walimfuata mtoto na kumuuliza maswali
kadhaa kwa lengo la kujiridhisha ambapo
alisema:
“Mgosi alinichukua, akaniambia twende
kwake, tulipofika huko akanivua nguo na
kunilalia…ameniumiza,” alisema mtoto huyo
huku akionekana bado kuwa kwenye
maumivu makali.
Baada ya kumpeleka Mgosi katika kituo cha
Wazo, aliwekwa rumande na kufunguliwa
jalada la mashtaka WH/
RB/1891/2014KUBAKA.
Source: GPL
Wednesday, April 2, 2014
UTAJIRI WA MASANJA NI NOMA HEBU CHEKI APA
UTAJIRI wa komediani maarufu Bongo, Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ ni kufuru! Tena unatisha na sasa anaonekana kuwa miongoni mwa wasanii wanaomiliki fedha na mali nyingi Bongo, Risasi Mchanganyiko linakupa zaidi.
Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ akiwa mbele ya usafiri na mjengo wake. HABARI MEZANI Awali, habari kuhusu utajiri wa Masanja ilitua mezani mwa gazeti hili kama kidokezo, hapo mwandishi wetu akaingia mzigoni na kuanza kuchunguza kwa kina mali anazomiliki msanii huyo na kugundua kuwa ni kati ya mastaa mabilionea Bongo.
“Masanja sio yule tena. Ana mpunga (fedha) mrefu sana. Hakuna msanii wa maigizo Bongo anayeweza kumfikia kwa sasa. Hao wengine ni mbwembwe tu, lakini pesa imelala kwa Masanja,” kilipasha chanzo chetu.
Kikaongeza: “Kwanza ana ghorofa lipo Tabata, hapo ndipo anapoishi. Pia ana magari kibao ya kifahari, mashamba ya mpunga na Kampuni ya OK Security inayolinda sehemu mbalimbali zikiwemo taasisi nyeti nchini.
Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ akiwa kwenye pozi na miongoni mwa magari yake. “Ni msanii gani mwenye kampuni kubwa kama ya Masanja? Wengi wanaishia kudai wanatayarisha filamu ambazo hata matunda yake hayaonekani.”