NI AIBU! Jamaa mmoja anayejulikana kwa
jina la Iddi Mgosi anashikiliwa na Polisi wa
Kituo cha Wazo jijini Dar es Salaam kwa
tuhuma za kumbaka mtoto mwenye umri wa
miaka minne (jina linahifadhiwa) huko
Mivumoni, Madale Machi 18, mwaka huu.
Mtoto wa miaka minne aliyefanyiwa unyama
huo.
Mgosi, ambaye umri wake haukuweza
kupatikana mara moja, anadaiwa kumrubuni
mtoto huyo kutoka nyumbani kwao na
kumpeleka kwake, ambako alimuingilia kwa
nguvu na baadaye kumtisha kutosema lolote
kwa wazazi wake.
Mama mzazi wa mtoto huyo, aligundua
mwanaye kuwa na maumivu makali wakati
akimuogesha, kwani alipomshika sehemu
zake za siri, binti huyo alipiga kelele za
maumivu na alipoulizwa kilichomsibu ndipo
alipoelezea alichofanyiwa.
Akizungumza kwa masikitiko makubwa,
mama huyo aitwaye Hadija, alisema alikuwa
akimuogesha mtoto wake huyo bila kugundua
kwamba alikuwa amebakwa na kuharibiwa
vibaya sehemu zake za siri. Alipomshika kwa
ajili ya kumsafisha, mtoto huyo akaanza kulia
na kulalamika kwamba alikuwa akimuumiza.
Bi Hadija alisema mara baada ya kuambiwa
hivyo, akawaita ndugu zake na kuwasimulia
alichoambiwa hivyo wote kwa pamoja
wakachukua jukumu la kumfuata Mgosi,
kumkamata na kumpeleka katika Kituo cha
Polisi Wazo.
Baada ya kumuogesha binti yake,
wakampeleka katika hospitali ya
Mwananyamala alikochukuliwa vipimo
kadhaa na kuambiwa wampeleke mtoto huyo
katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
“Hospitalini walituambia kwamba sehemu
zake za siri zimeharibiwa sana na hata kibofu
chake cha mkojo pia kimeharibiwa kwani
wametoa uchafu mwingi. Kwa sasa
amelazwa hospitalini huku akiendelea
kupatiwa matibabu na hawajajua ni siku gani
ataruhusiwa.”
MTOTO AFUNGUKA
Waandishi wetu hawakuishia hapo,
walimfuata mtoto na kumuuliza maswali
kadhaa kwa lengo la kujiridhisha ambapo
alisema:
“Mgosi alinichukua, akaniambia twende
kwake, tulipofika huko akanivua nguo na
kunilalia…ameniumiza,” alisema mtoto huyo
huku akionekana bado kuwa kwenye
maumivu makali.
Baada ya kumpeleka Mgosi katika kituo cha
Wazo, aliwekwa rumande na kufunguliwa
jalada la mashtaka WH/
RB/1891/2014KUBAKA.
Source: GPL
Tuesday, April 8, 2014
NJEMBA YABAKA MTOTO WA MIAKA MINNE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment