Sunday, April 13, 2014

DAH!! MAJANGA MZEE GURUMO AFARIKI DUNIA

BreakingNews, Ent. , stori kubwa
Tweet 20 418 Like
0
Breaking: Kuhusu mwanamuziki
mkongwe mzee Gurumo kufariki
dunia.
Ni mzee wa siku nyingi sana kwenye muziki
Tanzania ambae aliwahi kuingia kwenye
vichwa vya habari mara nyingi hasa kutokana
na kuugua kwake kuliko mfanya aache hata
muziki aliokua anaufanya.
Taarifa zilizothibitishwa na hospitali ya Taifa
Muhimbili kwa millardayo.com zimesema Mzee
huyu amefariki dunia akiwa hospitalini hapo leo
April 13 2014 saa nane mchana baada ya
kuletwa jana asubuhi na kulazwa kwenye wodi
namba 6 ya Mwaisela kutokana na kuzidiwa.
Tayari mwili wake umepelekwa kwenye chumba
cha kuhifadhia maiti ambapo taarifa zaidi
kuhusu chanzo cha kifo na taratibu za mazishi
millardayo.com itaendelea kuzitoa kupitia
@millardayo kwenye twitter instagram na
facebook.

No comments:

Post a Comment