Tuesday, April 22, 2014

KOCHA MKUU WA KLABU YA MANCHESTER UNITED DAVID MOYES ATIMULIWA

Kocha mkuu na meneja wa wa klabu
ya Manchester United David Moyes
ametimuliwa.
Meneja wa klabu ya Manchester
United David Moyes amefutwa kazi
baada ya kushikilia usukuni wa
klabu hiyo kwa miezi kumi tu.
Klabu hiyo hapo awali ilikuwa
imekataa kuzungumzia udaku wa
magezti kuwa Moyes atafutwa kazi
kabla ya msimu kumalizika.
Moyes, mwenye umri wa miaka 50,
aliteuliwa na Ferguson kumrithi
alipostaafu mwaka jana baada ya
kuwa na klabu hiyo kwa miaka 26.
HABARI KAMILI KUHUSU MOYES
KUTIMULIWA MAN U.. SOMA HAPO
CHINI..
Mkufunzi mkuu na meneja wa klabu
ya Manchester United David Moyes
ametimuliwa.
David Moyes amefutwa kazi baada
ya kushikilia usukuni wa klabu hiyo
kwa miezi kumi tu.
Klabu hiyo hapo awali ilikuwa
imekataa kuzungumzia udaku wa
magezti kuwa Moyes atafutwa kazi
kabla ya msimu kumalizika.
Moyes, mwenye umri wa miaka 50,
aliteuliwa na Ferguson kumrithi
alipostaafu mwaka jana baada ya
kuwa na klabu hiyo kwa miaka 26.
Taarifa kutoka kwa klabu hiyo
imemshukuru Moyes kwa bidii,
uaminifu na hekima aliyoonyesha
kocha huyo akiwa mkufunzi wa
Manchester United.
Moyes alichukuwa usukani wa
kuifunza Manchester United mwaka
uliopita baada ya aliyekuwa kocha
wa siku nyingi Sir. Alex Ferguson
kustaafu.
Huku zikiwa zimesalia mechi nne
pekee msimu wa ligi kukamilika
Mancheseter united inashikilia
nafasi ya saba kwenye jedwali la
msimamo wa ligi hiyo alama ishirini
na tatu nyuma ya viongozi Liverpool.
Klabu hiyo imeshindwa kufuzu
kushiriki michuano ya ligi ya
mabingwa ulaya kwa mara ya
kwanza katika kipindi cha takriban
miaka ishirini.

No comments:

Post a Comment