JOHARI ATEMA
CHECHE.."SIJAWAHI ,SINA NA
WALA SIWEZI KUWA NA
UHUSIANO NA MTU MPUUZI
KAMA YULE...."NI SHIDAAA
AISEEE....!
NI mtafutano! Staa mkubwa wa sinema
za Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’
ameingia kwenye vita ya maneno na
bosi wa Mtanashati Entertainment,
Ostaz Juma Namusoma ikiwa ni siku
chache tangu jamaa huyo alipotangaza
kumuoa mwanadada huyo.
Staa mkubwa wa sinema za Bongo,
Blandina Chagula ‘Johari’.
Wakizungumza na Risasi Jumamosi kwa
nyakati tofauti, kila mmoja alitoa la
moyoni huku Johari akionekana
kukasirishwa mno na ishu hiyo.
KILICHOMPONZA JOHARI
Ilidaiwa kuwa baada ya Ostaz
kutangaza kwamba atafunga ndoa na
Johari, vyombo mbalimbali vya habari
na mitandao ya kijamii vililichukulia
jambo hilo kwa ukubwa wake kwani
mwanadada huyo hakufunguka
sawasawa.
WENGINE WADAI KULIPA KISASI
Habari zinasema baada ya ishu hiyo
kugeuka habari ya mjini ilidaiwa
kwamba labda Johari aliamua kufanya
hivyo kwa kuwa mkurugenzi mwenzake
wa RJ Film Production ‘RJ’, Vincent
Kigosi ‘Ray The Greatest’ naye alidaiwa
‘kuchepuka’ na Chuchu Hans.
Bosi wa Mtanashati Entertainment, Ostaz
Juma.
Kuenea kwa habari za Johari kuolewa
na Ostaz kulimsababishia usumbufu
mkubwa mwanadada huyo kutoka kwa
ndugu, jamaa na marafiki wakihoji
ukweli wa ishu hiyo ili kujiandaa na
cherekochereko.
MADAI YA AWALI YA OSTAZ
Katika maelezo yake ambayo yapo
kwenye rekodi zetu, Ostaz alidai kuwa
Johari anajua kila kitu kwani
walifahamiana kitambo hata kabla ya
mrembo huyo kujuana na Ray.
Hakuishia hapo, Ostaz alidai kuwa
tayari amemfungulia Johari kampuni ya
kutengeneza sinema pamoja na vifaa
vyote hivyo yupo kwenye mishemishe
za kumuoa.
JOHARI SASA
Ili kuondoa utata huo, gazeti hili
lilimtafuta Johari kwa udi na uvumba
na kutaka kujua undani wa ishu hiyo
ambayo imezua maswali mengi hasa
kwa mashabiki wake.Johari: Sijawahi,
sina na wala siwezi kuwa na uhusiano
na mtu mpuuzi kama yule (Ostaz Juma).
Mwanzoni nilidhani utani, nashangaa
imekuwa ishu kubwa.
Risasi Jumamosi: Kwani hufahamiani
na Ostaz? Mbona anasema anakujua
tangu unaishi Mburahati, Dar na enzi
ukiwa Kaole?
Johari: Ni kweli Ostaz alikuwaga
anakuja pale Kaole tulipokuwa
tunafanya mazoezi lakini si yeye
waliokuwa wanakuja ni wengi.
Risasi Jumamosi: Je, hajawahi kuleta
maombi ya kukuoa?
Johari: Hakuwahi kunitongoza ila kila
nilipokutana naye nilikuwa najua kwa
kumwangalia tu machoni. Alikuwa
anaonesha kabisa ananitaka lakini
hakuwahi kunitamkia.
“Hajawahi kuniambia anataka kunioa.
Kwanza mimi ni Mkristo. Sina ndoa
mbili. Siwezi kuolewa mke wa pili na
mpuuzi kama yeye.
Risasi Jumamosi: Je, zile picha
zilizosambaa ukiwa umepozi kimahaba
na Ostaz zilitoka wapi?
Risasi Jumamosi: Ilikuwa nje ya RJ,
nilipiga picha na watu wengi kama
Dogo Janja akiwemo na huyo Ostaz.
Nilipigwa na butwaa nilipoziona
mitandaoni eti nina uhusiano na Ostaz
huku naye akiulizwa na kudai ni kweli.
“Kwani kupiga picha na mtu ndiyo
tayari mmekuwa wapenzi au
wachumba? Labda yeye anachukulia
hivyo kwamba ukishapiga picha na
mwanamke tayari anakuwa mpenzi
wako.”
Risasi Jumamosi: Kuhusu dini, Ostaz
alisema atakubali uwe Mwislamu na
jina lako litakuwa Rahma. Je,
alishakuambia juu ya hilo?
Johari: Hajaniambia, hata hivyo, sina
mpango wa kubadili dini ili niolewe na
yeye.
Risasi Jumamosi: Vipi kuhusu Ostaz
kukufungulia kampuni na vifaa vya
kutengenezea sinema?
Johari: Mh! Achana na kampuni au
vifaa, hata simu tu hajawahi
kuninunulia, kwanza hana fedha.
Halafu ajue kabisa kwamba mimi ni
tofauti na hao wasanii wengine
wanaoishi kwa kutegemea kuhongwa.
Mimi ni super woman, siku hizi huwa
fedha kwangu ni makaratasi. Huyo
Ostaz ana fedha gani?
“Haniwezi, mimi siyo kama hao watoto
anaowadhalilisha kwa kuwapigisha
magoti na akome kabisa kutumia jina
langu kama daraja. Hakuna kitu
ninachochukia kama mtu kutaka
kutumia jina langu kujitafutia
umaarufu, ana hadhi gani ya kuwa na
mimi, akome kabisa, mimi nimesota,
ninyi Global mnajua.”
Risasi Jumamosi: Umekana kuwa na
uhusiano wa kimapenzi na Ostaz, je,
una mchumba au mpenzi?
Johari: Mimi ni mwanamke
niliyekamilika. Nina mchumba na
‘soon’ nitamtambulisha kwa mashabiki
wangu. Lakini ijulikane kuwa siyo Ostaz
kwani hawezi kuwa mchumba wangu.
Risasi Jumamosi: Au unataka kurudi
kwa Ray?
Johari: (mshtuko) hivi ni nani aliwahi
kutamka kwamba mimi na Ray ni
wapenzi. Hapana, siyo Ray.
Risasi Jumamosi: Kwani Ray ni nani
kwako?
Johari: Ray ni mkurugenzi mwenzangu
wa RJ. Nje ya kazi tuna maisha yetu
mengine.
Risasi Jumamosi: Je, ni mtu maarufu?
Johari: Nimeshasema nitawatambulisha
subirini. Unajua mimi siyo mtu wa
matangazo.
Baada ya kumsikia Johari, gazeti hili
lilimgeukia Ostaz ambaye hakupatikana,
lakini rafiki yake wa karibu alidai kuwa
Johari amechanganyikiwa kwani Ostaz
alikuwa amuoe kweli lakini hamuelewi
mwenendo wake wa sasa.
“Johari amechanganyikiwa,” alisema
rafiki huyo.
Friday, April 11, 2014
JOHARI ATEMA CHECHE" SIJAWAHI SINA NA WALA SIWEZI KUWA NA UHUSIANO NA MPUUZI MKUBWA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment