Ally kiba naomba uingie mwenyeewe coz umeyataka mwenyewe.. sungura ulikuwa umesha mkamata eti umemuachia kiboya boya sasa kumkamata tena itaghalimu miaka mitano... Sisi wote Tupo kwenye Sanaa ila nguvu tunazidiana ndomana ally nilikuona mkombozi Wetu coz we ni fundi muziki.. Inakuwa je unajianguaha kwenye kumi na nane?????? Badala ya kufunga unategemea penati... Ona sasa refa kapeta... Na kufanya Kwa sasa tukubali bwana @diamondplatnum ni #KIBOKO japo alikwapua Ka aidia kangu na ndo kanakompa mijituzo.. Ila nime hands up... Ally kiba na diamond wote ni ma home boy kutoka KIGOMA ila mnyonge mnyongeni Haki yake mpeni... Hii ni kick kuna mtu yeyote mwenye snea??
Sunday, November 30, 2014
Wednesday, November 26, 2014
SOMA MAJINA YA WALIOKULA FEDHA ZA AKAUNTI YA ESCROW KATIKA RIPOTI YA PAC INAYOSOMWA LEO BUNGENI.
waliingiziwa fedha katika akaunti zao binafsi ni;
Mhe.
Andrew Chenge (Mb)
Zitto: Andrew Chenge aliingiziwa shilingi bilioni
1.6.
Zitto: Mhe. Anna Tibaijuka (Mb) na Waziri wa 62
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi shilingi
bilioni 1.6.
Zitto: Mhe.William Ngeleja (Mb) na ambaye
alikuwa Waziri wa Nishati na Madini alipewa
shilingi milioni 40.4
Zitto: Ndg. Daniel N. Yona ambaye alikuwa pia
Waziri wa Nishati na Madini alipewa shilingi milioni
40.4.
Zitto: Ndg. Paul Kimiti ambaye ni Mbunge Mstaafu
wa Jimbo la Sumbawanga
alipewa shilingi milioni 40.4
Zitto: Dr. Enos S. Bukuku ambaye alikuwa Mjumbe
wa Bodi ya TANESCO aliingiziwa shilingi milioni
161.7.
Zitto: Upande wa Majaji Prof. Eudes Ruhangisa,
aliingiziwa milioni 404.25 na J.A.K Mujulizi
aliingiziwa shilingi milioni 40.4
Zitto: kwa upande wa Watumishi wa umma,Ndg.
Philip Saliboko ambaye alikuwa mtumishi wa RITA
aliingiziwa
shilingi milioni 40.4
Zitto: Ndg. Emmanuel Daniel Ole Naiko ambaye
alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa (TIC) aliingiziwa
shilingi milioni 40.4
Zitto: Ndg. Lucy L. Appollo ambaye ni Mtumishi
wa TRA aliingiziwa shilingi milioni 80.8.
Zitto: Viongozi wa Madhehebu ya
Dini walioingiziwa fedha na Benki ya Mkombozi ni
Askofu 63
Methodius Kilaini shilingi 80.9
Zitto: Askofu Eusebius Nzigirwa shilingi milioni
40.4 na Mchungaji Alphonce Twimann Ye Simon
shilingi milioni 40.4.
Zitto: Watu walienda kugawana fedha kwenye
Benki tajwa wakiwa na mifuko ya rambo,
sandarusi,
mabox, magunia na lumbesa TegetaEscrow
Zitto: Bilioni 73.5
zilitolewa na kugawanywa kwa watu mbalimbali
kinyume cha
Sheria ya Benki Kuu na Taasisi za Fedha ya 2006
Zitto: Taarifa
ya benki (bank statements) yenye majina na
akaunti zote
zilizoingiziwa fedha zimeambatishwa.
Zitto: Kamati imebaini mawasiliano kutoka kwa
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini na
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha
Tuesday, November 25, 2014
Monday, November 24, 2014
Thursday, November 20, 2014
Monday, November 17, 2014
MTOTO ALIYEGEUKA NYOKA AZUA BALAA…!!
Mtoto mchanga mwenye umri wa miezi minne amezua kizaazaa cha aina yake, baada ya kuwapo taarifa kwamba mara kadhaa umbo lake limekuwa likigeuka na kuwa nyoka na mwili wake ukiendelea kudhoofu kutokana na kukataa kunyonya maziwa ya mama yake.
Mtoto huyo (jina lake tunalihifadhi kwa sasa), wiki iliyopita alivuta umati wa wakazi wa Kijiji cha Nkome mkoani Geita ambao walifurika ndani na nje ya Kanisa la AICT Nkome, lililopo kijiji hapo, kushuhudia maombi ambayo alikuwa akifanyiwa ili kumkomboa katika kile kilichotafsiriwa kuwa ni mateso dhidi yake.
Ilikuwa saa 4.00 asubuhi Jumamosi, Novemba 8 mwaka huu wakati mtoto huyo alipofikishwa katika kanisa hilo na kuanza kufanyiwa maombi na sababu ya hatua hiyo ikielezwa kuwa ni kutokana na kuwa na umbo la nyoka na kwamba matendo yake yanaashiria kwamba mwenye asili ya nyoka ndani ya roho yake.
Mtoto huyo alifikishwa kanisani hapo na mama yake mzazi, Sarah Silasi wakitokea Kijiji cha Ichile, Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza, ambako alikimbia matukio yanayohusishwa na ushirikina.
Mmoja wa wazee wa kanisa hilo la AIC Nkome, Mathew Misana anasema: “Alikuwa anatoa ulimi mithili ya nyoka, mwendo wake anapolala alijizungusha kama nyoka na hata alipojikunja mwili wake ulikuwa kama unavyoona nyoka.”
Misana anasema matukio hayo na mengine kadhaa yakiwamo ya ngozi ya mtoto huyo kuwa nyeusi kama ya nyoka aina ya chatu, yaliwalazimisha ndugu na jamaa zake wakiongozwa na mama mzazi kutaka aombewe.
“Ngozi yake kuonekana kama ya mzee huku macho yake yakionekana kuwa makubwa na kichwa chake kuwa na umbo la nyoka pamoja na miguu, baada ya kuona hali hii tukaihusisha na mambo ya kishirikina na kuamua kuanza maombi,” alisisitiza.
Hata hivyo, muda mfupi baada ya maombi kuanza, taarifa za kuwapo kwa aina hiyo ya mtoto zilisambaa haraka na kusababisha umati mkubwa wa watu kujaa ndani ya kanisa hilo ambalo ni boma kwa maana kwamba ujenzi wake bado unaendelea.
“Watu wengi walijaa na wengine wakawa wanapanda juu ya miti na juu ya boma wakati mwingine matofali yalianguka. Hewa ikapungua na usalama ukawa mdogo kwani watu walisukumana wakitaka kushuhudia,” anasema Misana.
Baada ya watu kuwa wengi, uongozi wa kanisa uliomba msaada wa Polisi wa Kituo cha Nkome ambao walifika kanisani hapo na kushauri mtoto huyo aonyeshwe ili watu waweze kuridhika kwamba hakuwa amegeuka kuwa nyoka.
Uongozi wa kanisa ulifanya hivyo lakini mwonekano wa mtoto huyo ulisababisha watu kuongezeka badala ya kupungua na hapo ndipo polisi walipoelekeza mama wa mtoto huyo ambebe na kuondoka naye hadi kituoni.
Mwinjilisti wa kanisa hilo, Emmanuel Misungwi anasimulia: “Tumeshudia vitu visivyo vya kawaida wakati tunafanya maombi na wakati tunaendelea na huduma, mama wa mtoto Sarah alianguka akaanza kuongea juu ya mtoto kwa nguvu ya mapepo.”
SOURCE:MWANANCHI
Wednesday, November 12, 2014
BREAKING:RAPPER GEEZ MABOVU AFARIKI DUNIA
Mabovu ambae ni maarufu kwenye muziki wa
hiphop Tanzania, amefariki dunia kwenye
hospitali aliyokua amelazwa nyumbani kwao
Iringa alikokwenda wiki mbili zilizopita kutokea
Dar es salaam.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Iringa, Geez
amefariki jioni hii. Alienda kwao wiki moja na
nusu iliyopita ambako alianza kuugua mfululizo
mpaka mauti yalipomkuta.
Geez atazikwa kesho (Leo) jioni November 13
2014.
Saturday, November 8, 2014
SITTI ABBAS MTEVU KUJIVUA UMISS TANZANIA
Barua ya Sitti Mtemvu:
Mimi Sitti Abbas Mtemvu baada ya kutwaa taji la urembo la Miss Tanzania kumezuka shutuma mbalimbali dhidi yangu. Wameniwekea maneno mengi sana mdomoni kwamba nimesema wakati sio. Shutuma hizo zimeandikwa katika vyombo mbalimbali vya habari, blogs na mitandao ya kijamii, kiasi ambacho naweza hata kuhatarisha maisha yangu.
Sasa kwa hiari yangu tena bila kushawishiwa na mtu na kwa kulinda heshima yangu na familia yangu natamka rasmi kuvua taji la urembo la Miss Tanzania 2014. Napenda niwashukuru wale wote waliokuwa wakinipa sapoti tangu mwanzo nilipoingia katika mashindano haya katika ngazi ya taifa, na warembo wote wa Chang’ombe, Temeke pamoja na wote tuliokuwa nao katika fainali za Taifa.
Pia napenda kutuma shukrani za dhati kwa waandaji wote wa kituo cha Chang’ombe, Temeke na wajumbe wa Kamati ya Miss Tanzania kwa mafunzo mbalimbali niliyopata. Nawashukuru pia waandishi wote kwa mchango wenu, pamoja na wizara ya habari, utamaduni na michezo na Baraza la Sanaa kwa busara zenu. Leo nalivuta taji rasmi nililopewa na binadamu lakini alilonipa mwenyezi Mungu bado ninalo. Mwisho naomba radhi Watanzania wote kwa uamuzi niliouchukua.

Wednesday, November 5, 2014
RAIS KUOMBWA MSAADA WA FEDHA KUTOA MWILI WA DADA AKE MOCHWARI
fedha kuutoa mwili wa dada yake
Mochwari…
Baadhi ya viongozi wakubwa duniani ikiwemo
Marais, Viongozi wa kidini na wengineo
wamekuwa na utaratibu wa kutumia huduma
za mitandao ya kijamii na simu za mkononi
kuwasiliana na watu.
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ni moja ya
marais ambao wamekuwa wakitajwa kutumia
sana mitandao ya kijamii ikiwemo Twitter.
Huenda usiamini alichokifanya Rais Uhuru
Kenyatta, stori ni kwamba baada ya
kutumiwa message na Anita Lipesa ambaye
alikwama shilingi milioni tatu na laki tano za
Kenya kwa ajili ya kutoa mwili wa dada yake
aliyefariki kutoka chumba cha kuhifadhia
maiti.
Anita amesema baada ya jitihada za
kuchangisha michango kushindikana aliamua
kumtumia ujumbe kwa Rais Kenyatta ingawa
hakuwa na tumaini lolote kujibiwa, dakika 30
baada ya kutuma message hiyo Kenyatta
alimpigia simu dada huyo ambaye hakuamini
kama Rais angeweza kufanya hivyo.
Dada huyo anasema baada ya kumwelezea
Rais kilichotokea alipata msaada wa kuutoa
mwili wa dada yake huyo na kwenda kufanya
mazishi.
Anita (mwenye t-shirt nyeusi) akiwa
na familia yake.
BOB JUNIOR AMPA RAHA SABBY ANGEL
Kila Namna Sijawahi Kuona: Sabby Angel
Wawili wapendanapo dunia huwa
maua !...........Muigizaji mwenye mvuto wa aina
yake katika kiwanda cha filamu Tanzania Sabby
Angel amesema kuwa Mahaba anayopewa na
Bob Junior hajawahi kuyapata popote pale
kwani anamridhisha kwa kila namna kiasi cha
kufurahia maisha yake ya kimapenzi kwasasa,
yaani full raha tupu!.
Sabby amesema kuwa ametembea huku na
huko lakini kwa Bob Junior amenyoosha
mikono juuu!
Wawili hao wiki ilopita waliongozana wote
kwenda Tanga ambapo Bob Junior alikuwa na
show huko.
Sabby
Tuesday, November 4, 2014
WEMA SEPETU ACHAFUA HUKO INSTAGRAM WANAOSEMA AZAE

Monday, November 3, 2014
Huyu ndie kijana wa CCM inayesemakana Kampiga Waziri Mkuu Mstafu Mzee Warioba na Chupa ya Maji leo Ubungo
limetokea leo katika mdahalo uliondaliwa
na taasisi ya mwalimu Nyerere,Ubungo.
Katika mdahalo huo , vijana ambao mpaka
sasa hawajafahamika walisisima gafla wote
kwa pamoja wakiwa na mabango
yanayopigia debe katiba inayopendekezwa
na gafla fujo kubwa zikaibuka na watu
kuanza kupigana.
Kada wa CCM bwana Paul Makonda,
pichani, inasemekana alimpiga Mwenyekiti
wa tume ya mabadiliko ya katiba Mzee
Joseph Sinde Walioba kwa chupa ya maji.
Hili ni jambo la kwanza la aibu ya aina yake
kutokea nchini kwa kijana mdogo kumpiga
waziri mkuu wa nchi na chupa ya maji.
Tunatumai vyombo vya sheria vitachunguza
tukio hili na kuwachukulia hatu vijana wote
waliohusika katika fedheha hii.
TOA MAONI YAKO:
Subscribe to:
Posts (Atom)