Wednesday, November 5, 2014

RAIS KUOMBWA MSAADA WA FEDHA KUTOA MWILI WA DADA AKE MOCHWARI

Rais kuombwa Msaada wa
fedha kuutoa mwili wa dada yake
Mochwari…
Baadhi ya viongozi wakubwa duniani ikiwemo
Marais, Viongozi wa kidini na wengineo
wamekuwa na utaratibu wa kutumia huduma
za mitandao ya kijamii na simu za mkononi
kuwasiliana na watu.
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ni moja ya
marais ambao wamekuwa wakitajwa kutumia
sana mitandao ya kijamii ikiwemo Twitter.
Huenda usiamini alichokifanya Rais Uhuru
Kenyatta, stori ni kwamba baada ya
kutumiwa message na Anita Lipesa ambaye
alikwama shilingi milioni tatu na laki tano za
Kenya kwa ajili ya kutoa mwili wa dada yake
aliyefariki kutoka chumba cha kuhifadhia
maiti.
Anita amesema baada ya jitihada za
kuchangisha michango kushindikana aliamua
kumtumia ujumbe kwa Rais Kenyatta ingawa
hakuwa na tumaini lolote kujibiwa, dakika 30
baada ya kutuma message hiyo Kenyatta
alimpigia simu dada huyo ambaye hakuamini
kama Rais angeweza kufanya hivyo.
Dada huyo anasema baada ya kumwelezea
Rais kilichotokea alipata msaada wa kuutoa
mwili wa dada yake huyo na kwenda kufanya
mazishi.
Anita (mwenye t-shirt nyeusi) akiwa
na familia yake.

No comments:

Post a Comment