Monday, November 3, 2014

Huyu ndie kijana wa CCM inayesemakana Kampiga Waziri Mkuu Mstafu Mzee Warioba na Chupa ya Maji leo Ubungo

Jambo la aibu na la kufedhehesha sana
limetokea leo katika mdahalo uliondaliwa
na taasisi ya mwalimu Nyerere,Ubungo.
Katika mdahalo huo , vijana ambao mpaka
sasa hawajafahamika walisisima gafla wote
kwa pamoja wakiwa na mabango
yanayopigia debe katiba inayopendekezwa
na gafla fujo kubwa zikaibuka na watu
kuanza kupigana.
Kada wa CCM bwana Paul Makonda,
pichani, inasemekana alimpiga Mwenyekiti
wa tume ya mabadiliko ya katiba Mzee
Joseph Sinde Walioba kwa chupa ya maji.
Hili ni jambo la kwanza la aibu ya aina yake
kutokea nchini kwa kijana mdogo kumpiga
waziri mkuu wa nchi na chupa ya maji.
Tunatumai vyombo vya sheria vitachunguza
tukio hili na kuwachukulia hatu vijana wote
waliohusika katika fedheha hii.
TOA MAONI YAKO:

No comments:

Post a Comment