
Thursday, October 30, 2014
WOLPER AONGEA KWA UCHUNGU KUPITIA HILI GAZETI NA KUKANUSHA HII HABARI

BREAKING:MSANII MANENTO AFARIKI DUNIA
Wednesday, October 29, 2014
MSANII NAY WA MITEGO NA MPENZI WAKE WAPATA MTOTO

DIAMOND KUTUNUKIWA PHD
Breaking: CHIDI BENZ AFANIKIWA KUPATA DHAMANA
Tuesday, October 28, 2014
Breaking: MHIMBILI WAPANDISHA GHARAMA ZA VITANDA
Monday, October 27, 2014
BREAKING :CHID BENZI KUFIKISHWA MAHAKAMANI
Sunday, October 26, 2014
Friday, October 24, 2014
Breaking: CHIDI BENZI AKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA
Kuna taarifa zilitoka on millardayo.com leo
jioni kuhusu msanii wa muziki wa kizazi
kipya Chidi Benz kukamatwa na dawa za
kulevya katika uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam
akiwa anaelekea Mbeya kwenye show ya
Instagram Party ambayo inatarajiwa
kufanyika kesho.
millardayo.com iliahidi kuzifatilia hizi taarifa
kwa Polisi ili kupata uthibitisho ambapo
imefahamika ni kweli msanii huyu
amekamatwa leo mchana akiwa katika
sehemu ya kuondokea uwanjani hapo
ambapo baada ya alifanyiwa upekuzi na
kubainika amebeba dawa hizo ambapo ni
kete 14 za dawa za kulevya kwenye mfuko
wa shati lake na misokoto miwili ya bangi.
Kwenye mahojiano na millardayo.com
kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Hamisi
Selemani ambae ni kamanda wa polisi katika
viwanja vya ndege Tanzania amethibitisha
kukamatwa kwa Chidi Benz na kusema
msanii huyu alipohojiwa amekiri kweli kuwa
dawa hizo ni zake.
Amesema ‘Alikuja Airport kwa ajili ya safari
kwenda Mbeya, kete hizo 14 za dawa za
kulevya zilikua zimefungwafungwa na nailoni
na pia amekutwa na vifaa vingine
vinavyohusiana na watu wanaotumia dawa za
kulevya, kuna kigae na kijiko na yeye
mwenyewe anakiri ni vitu vyake huwa
anatumia ila anashangaa ni kwa nini
vimeweza kubaki kwenye mfuko,
tutamfikisha Mahakamani baada ya kuweza
kubaini ni dawa aina gani za kulevya’
BASATA KUMVUA TAJI MISS TANZANIA
Tuesday, October 21, 2014
Sunday, October 19, 2014
MSIKILIZE MENEJA WA T.I AKIONGEA JINSI YA KUFANYA COLLABO NA T.I

Records, Jason Geter amesema ili msanii wa Afrika aweze kupata collabo na msanii mkubwa wa Marekani, anahitajika kuwa na ushawishi katika sehemu anayokotoka ili awe na kitu cha kumuongezea pia msanii huyo anayetaka kumshirikisha. Meneja wa T.I, Joson Gete akizungumza na wadau wa muziki Dar Jason Geter Akiongea kwenye warsha iliyoandaliwa maalumu kwaajili ya wadau wa muziki nchini Ijumaa hii, Geter alitolea mfano wa jinsi T.I. alivyokubali kufanya wimbo na P-Square. Alisema alipigiwa simu na rafiki yake aliyemueleza kuwa kundi la P-Square lingetaka kumshirikisha T.I. kwenye wimbo wake lakini bahati mbaya hakuwahi kuwasikia wasanii hao. “Kiukweli nilikuwa sijawahi kuwasikia kabla, kwasababu Marekani hawachezwi kivile, nina uhakika baadhi ya watu wanawafahamu lakini watu wengi Marekani hawawafahamu kabisa P-Square,” alisema. Geter alidai baada ya kuambiwa hivyo aliamua kufanya utafiti wake mwenyewe ili kuwafahamu wasanii hao na hivyo aliingia Youtube kuwatazama. “Nilipoenda kufanya utafiti wangu, nikasema wow, hawa jamaa ni wakubwa,” aliongeza. Alidai baada ya kuona ukubwa wake, aliona kuwa P-Square wana kitu cha kumuongeza T.I. “Sababu mashabiki wengi wa P-Square wanaweza kuwa hawajawahi hata kumsikia T.I. Kwahiyo hicho ndio kitu cha kwanza kwamba utaenda kumuongezea nini msanii wangu. Msanii wangu ana msingi wa Marekani kukupa, wewe utaweza kumtambulisha kwa kitu kingine?” Aliongeza kuwa hatua ya pili inahusisha masuala ya fedha na biashara ambapo huusikiliza wimbo anaotaka kushirikishwa msanii huyo. Alisisitiza kuwa mara nyingi suala la fedha au malipo ya collabo sio kitu wanachokiweka mbele zaidi ya kuzingatia kuwa ni nini msanii wake atakipata kutokana na kushirikishwa kwenye wimbo huo. “Sawa unayo fedha, sasa hatua ya pili, kitu gani unaweza kukioffer kwake, una kitu cha kuoffer kwa msanii wangu? Je wimbo ni mzuri? Kwahiyo hivyo ndio vitu ambavyo unahitaji kuvifikiria. Na mwisho wa siku zote unatakiwa kulinda brand yako.” Kuhusu njia anayotakiwa msanii kufanikiwa katika soko la muziki wa Marekani, Jason alisema jambo la kwanza ni kuwa na ukaribu na watu kama yeye ambao wana connection na watu wengi pamoja na brands ambazo zimesimama nchini humo. Geter alidai kufanya wimbo na msanii wa Marekani peke yake, haitoshi kwa msanii wa Afrika kufanikiwa kwenye soko la Marekani. “T.I. alifanya ngoma na P-Square, lakini kiukweli, inahitaji zaidi ya hivyo kupenya soko la Marekani,” alisisitiza Geter. “Inahitaji T.I. na P-Square kwenda kwenye game ya basketball pamoja na kutembea pamoja. Inahitaji uwekezaji huo wa muda kwa msanii wa Afrika kutumia muda kukaa kwenye soko la Marekani.” Geter alisisitiza kuwa kama msanii anataka kufanikiwa Marekani, anatakiwa kutake risk kwa kuacha fedha nyingi anazopata Afrika na kukubali kupata kidogo Marekani wakati anakuza jina lake. “Kama unaingiza dola 5 Afrika, unaweza kuja Marekani na utakuwa na bahati sana ukipata sehemu sahihi ambazo unaweza ukapata hata dola moja tu. Ni kazi sana kwa watu kuwekeza muda wa aina hiyo na nguvu katika chochote kile, hiyo ndio changamoto kubwa.” Geter alisema hilo linawezekana kwa kuingia ubia na watu ambao tayari wana nguvu huko kukusaidia. Kuhusu lugha ambayo msanii anatakiwa kutumia, Geter alisema muhimu ni kufahamu kuongea Kiingereza lakini sio lazima nyimbo ziwe za lugha hiyo kwakuwa muziki unaweza kufanya vizuri hata kama ukiwa umeimbwa kwa lugha nyingine. “Lakini yote ni kuwa kile ambacho tunafanana ni rhythm. Ni ile beat inayonifanya nicheze na pia hisia ambayo inagusa moyo. So in America to get played on radio and all that stuff, yes you need to know some English but if you got that beat right, we gonna move man.”msikilize apa