Kuna taarifa zilitoka on millardayo.com leo
jioni kuhusu msanii wa muziki wa kizazi
kipya Chidi Benz kukamatwa na dawa za
kulevya katika uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam
akiwa anaelekea Mbeya kwenye show ya
Instagram Party ambayo inatarajiwa
kufanyika kesho.
millardayo.com iliahidi kuzifatilia hizi taarifa
kwa Polisi ili kupata uthibitisho ambapo
imefahamika ni kweli msanii huyu
amekamatwa leo mchana akiwa katika
sehemu ya kuondokea uwanjani hapo
ambapo baada ya alifanyiwa upekuzi na
kubainika amebeba dawa hizo ambapo ni
kete 14 za dawa za kulevya kwenye mfuko
wa shati lake na misokoto miwili ya bangi.
Kwenye mahojiano na millardayo.com
kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Hamisi
Selemani ambae ni kamanda wa polisi katika
viwanja vya ndege Tanzania amethibitisha
kukamatwa kwa Chidi Benz na kusema
msanii huyu alipohojiwa amekiri kweli kuwa
dawa hizo ni zake.
Amesema ‘Alikuja Airport kwa ajili ya safari
kwenda Mbeya, kete hizo 14 za dawa za
kulevya zilikua zimefungwafungwa na nailoni
na pia amekutwa na vifaa vingine
vinavyohusiana na watu wanaotumia dawa za
kulevya, kuna kigae na kijiko na yeye
mwenyewe anakiri ni vitu vyake huwa
anatumia ila anashangaa ni kwa nini
vimeweza kubaki kwenye mfuko,
tutamfikisha Mahakamani baada ya kuweza
kubaini ni dawa aina gani za kulevya’
Friday, October 24, 2014
Breaking: CHIDI BENZI AKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment