Wednesday, October 15, 2014

HALIMA JAMES MDEE AFUNGUKA MAZITO



MBUNGE wa Jimbo la Kawe jijini Dar na
Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Bawacha),
Halima James Mdee ambaye aliwekwa
Mahabusu ya Gereza la Segerea, Dar kwa saa
kumi na mbili amesimulia mambo matano
mazito aliyokumbana nayo hali iliyomfanya
atokwe machozi.
Mbunge wa Jimbo la Kawe jijini Dar
na Mwenyekiti wa Baraza la
Wanawake wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo
(Bawacha), Halima James Mdee.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii
mwishomi mwa wiki iliyopita, Mdee licha ya
kuponda utendaji kazi mbovu wa serikali
kuhusu mahabusu, aliyataja mambo hayo kama
ifuatavyo:
HAUSIGELI NA KESI NDOGONDOGO
Alisema alipofika mahabusu aliwakuta
wasichana wadogo ambao baadhi yao ni
mahausigeli wakamlalamikia kwamba wamekaa
ndani kwa muda mrefu bila kesi zao kusikilizwa.
Alisema kwa uchunguzi wake alibaini kuwa
wasichana hao wa kazi za ndani, kesi zao
zilifunguliwa kwa kubambikwa na mabosi wao
pale wanapodai malipo, hivyo wao husingiziwa
wizi au kosa lolote.
UBOVU WA CHAKULA
Pia Mdee alisema chakula cha mahabusu
hakiridhishi kutokana na kupikwa bila kiwango
na kuwa na michanga, wakati mwingine hakiivi.
MAHABUSU KUKAA MUDA MREFU
BILA KESI KUSIKILIZWA
Jambo jingine alilodai kukumbana nalo Segerea
ni mahabusu kukaa kwa muda mrefu kati ya
miaka 4 hadi 7 bila kesi zao kusikilizwa kwa
kisingizio cha upelelezi kutokamilika.
MACHANGUDOA KUWASHAWISHI
MABINTI
Katika sakata lingine, Mdee alisema wanawake
wengi waliokamatwa kwa makosa ya kujiuza
usiku (machangu) wanaopelekwa mahabusu
wamekuwa wakiwashawishi wasichana wadogo,
hasa mahausigeli wanaofikishwa humo.
“Wasichana hao huwashawishi mahausigeli kiasi
kwamba wanapotoka mle mahabusu na wao
wanakwenda kujihusisha na ukahaba na
biashara ya madawa ya kulevya kwa vile baada
ya kutoka hawapewi nafasi na mabosi wao
kuendelea na kazi,” alisema Mdee.
MAHABUSU WA KIKE KUADHIBIWA
NA ASKARI WA KIUME
Jambo lingine aliloligundua Mheshimiwa Mdee
ni kitendo cha askari wa kiume kutoa adhabu
kwa maabusu wa kike badala ya kuadhibiwa na
wanawake wenzao kitendo ambacho alisema
kimekuwa kikiwadhalilisha mahabusu hao.
Hata hinyo, Mdee alimuomba Waziri wa Sheria
na Katiba, Asharose Migiro kuanzisha utaratibu
wa safari za kushtukiza magerezani na
kuzungumza na mahabusu ili kusikiliza kero zao
na kuzitatua.
Jumanne iliyopita, Mdee alifikishwa katika
gereza hilo saa 11 jioni ambako alilala hadi
kesho yake saa 1 asubuhi kwa madai ya
kufanya maandamano haramu kwenda Ikulu ya
Dar.

No comments:

Post a Comment