Thursday, October 16, 2014

KIJANA APIGISHWA MBIZI KWENYE DIMBWI

Askari wa jeshi la Wananchi
la Tanzania (JWTZ)
akimwadhibu kijana ambaye
hakuweza kufahamika jina lake
mara moja, kwa kumpigisha
mbizi kwenye dimbwi la maji
ya barabarani baada ya
kukutwa akiwa ametinga sare
za Jeshi la Wananchi huku
akipiga misele mitaani
wakati akitambua kuwa yeye
si askari ni raia wa
kawaida.
Kijana huyo alikutana na
adhabu hiyo kali kutoka kwa
mjeda huyo baada ya kumbaini
kuwa si askari halisi ya
jeshi la Tanzania wakati
alipokamatwa na kushindwa
kutoa maelezo ya kuridhisha
kuhusiana na swala zima la
kijeshi, na hapo ndipo
alipoanza kuamuliwa kuvua
mavazi hayo na kisha kuaza
kutumikia adhabu hiyo.
Tukio hilo lilitokea hivi
karibuni maeneo ya Kariakoo
jijini Dar es Salaam.
Kijana akiendelea kutumikia
adhabu ya kupiga mbizi.
Picha na Kamanda wa Matukio
Blog.Mia

No comments:

Post a Comment