Tarifa kutoka Idara ya Sanaa ya Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)
zinasema kuwa tarehe 8 Novemba 2014,
Kijana Nassib Abdul atatunukiwa Shahada
ya Uzamivu(Phd) na Chuo hicho kwa
kuthamini mchango wake kwenye jamii
kupitia sanaa.(Honorary PhD in Fine
&Perfoming Arts).
Alongside DIAMOND mwingine
atakayepewa Shahada hii ya Heshima
kwenye Mahafali haya ni Balozi Fulgence
Kazaura (marehemu) ambaye aliwahi kuwa
Chancellor wa UDSM miaka ya nyuma!!
Naibu Mkuu wa shule ya Sanaa na
Sayansi ya Jamii (College of Arts and
Social Sciences) Prof.H Sigala amekiri
kupokea maombi kutoka Idara ya Sanaa
za Maonesho (Department of Fine
&Perfoming Arts) ya kumtunuku Diamond
PhD.
Amesema bado haijadhibitika kama
Diamond atatunukiwa shahada hiyo hadi
bodi ya taaluma ya chuo (senate) ikae na
kupitia maombi hayo. “Senate ikikaa
inaweza kukubali au kukataa maombi
hayo, lakini kwa sasa hatuwezi kusema
lolote” alisema Prof.Sigala.
Mashabiki wa Diamond wamepokea kwa
furaha taarifa hizi na wengine wameanza
kurusha vijembe mitandaoni kujibu
mapigo ya waliomzomea Diamond kwny
tamasha la Fiesta mwaka huu.
Mdau mmoja wa karibu wa Diamond
amenukuliwa kwny ukurasa wake wa
Facebook akisema “Ningependa
kuwakaribisha Wazomeaji woooteee
wenye sauti mbaya sana waweze kufika
kwenye Viwanja vya UDSM kushuhudia
Tukio la Kihistoria kwa Mtoto huyu wa
Tandale ambaye ni BIDII NA HESHIMA
Vimemfikisha hapa.”
Ikiwa “Senate” ya UDSM itapitisha
maombi hayo, na Diamond kutunukiwa
Shahada hiyo basi atatambulika rasmi
kama DR.NASIBU ABDUL au Pengine
DR.DIAMOND PLATNUMZ au ukitaka
swaga unaweza sema DR.PLATNUMZ
BABY!
Baadhi ya watu wameonekana
kutoridhishwa na mapendekezo hayo ya
Idara ya Sanaa ya chuo kikuu cha Dar
kumtunuku Diamond PhD, huku wengine
wakinukuliwa wakisema “Ukistaajabu
Uprofesa wa JK utaona PhD ya Diamond”
SOURCE: JF
No comments:
Post a Comment