NI pigo tena kwa tasnia ya Bongo Muvi,
mwongozi filamu Bongo na aliyekuwa mume
wa staa wa filamu Bongo, Yvonny Cherry
‘Monalisa‘, George Tyson amefariki dunia
baada ya kupata ajali mbaya ya gari eneo la
Morogoro akitokea mkoani Dodoma. Tyson
alikuwa ameambatana na watu kadhaa
katika safari hiyo.
Friday, May 30, 2014
PIGO JINGINE BONGO MOVIE MWONGOZAJI WA MOVIE GEORGE TYSON AFARIKI DUNIA
Wednesday, May 28, 2014
MSANII RACHEL HAULE KUZIKWA KESHO
MSANII wa filamu Rachel Haule ‘Recho’
aliyefariki dunia siku ya jana atazikwa jijini
Dar es Salamm siku ya kesho badala ya
Songea kama ilivyopangwa hapo awali.
Ratiba ya kuuaga mwili wa marehemu
inabaki pale pale siku ya kesho Leaders Club
na baadae kwenda kuzikwa katika makaburi
ya Kinonondoni.
Tuesday, May 20, 2014
DIAMOND BADILIKA KABLA MAMBO HAYAJAHARIBIKA.
Kwa Staili Hii Diamond Badilika Kabla Mambo
Hayajaharibika..Kwa Mengine Hongera.
Mwaka 2014 umekuwa ni mwaka wenye
neema nyingi kwa Diamond Platnumz
kimataifa. Tangu aachie video ya remix ya
My Number One aliomshrikisha Davido,
jina la staa huyo limekuwa kubwa kiasi
cha sasa kumfanya afike sehemu ambayo
hakuna msanii wa Tanzania aliyewahi
kufika.
Kuanzia video yake kushika namba moja
kwenye vitu vikubwa vya TV kikiwemo
Trace TV, kutajwa kuwania tuzo za MTV
MAMA katika vipengele viwili na pia
kutajwa kuwania tuzo za BET kwenye
kipengele cha Best International Act:
Africa. “An international music superstar
from Tanzania is being born right before
our eyes. Hongera sana
@diamondplatnumz,” alitweet January
Makamba.
Ni kweli, supastaa wa kimataifa kutoka
Tanzania amezaliwa mbele ya macho yetu
na ni wajibu wetu kumuunga mkono
katika kila hatua anayoenda. Lakini kama
unamtakia mtu heri na mafanikio zaidi, si
lazima kumsifia muda wote. Ni vyema
kumwambia ukweli pale ambapo tunahisi
anatakiwa kuparekebisha ili asonge
mbele zaidi.
Jambo muhimu ambalo Diamond
anatakiwa kurekebisha ni katika live
performance. Naomba nikiri kuwa pamoja
na kuwa shabiki mzuri wa nyimbo nyingi
za Diamond, sijawahi kupenda
performance zake za live. Nimeshamhudia
kwa zaidi ya mara 10 akitumbuiza na zote
nimekuwa nikimuona akifanya vilevile na
sipati kile ambacho nakuwa nakitegemea.
Juzi alikuwa mmoja wa wasanii
waliotumbuiza kwenye show ya Road to
MAMA ya MTV Base iliyofanyika Club
Bilicanas akiwa pamoja na Sauti Sol na
kundi la Mi Casa Music. Bahati mbaya
ama nzuri kwake ni kwamba kutokana na
kuwa msanii mwenyeji, yeye alikuwa
msanii wa mwisho kutumbuiza. Walianza
Wakenya Sauti Sol ambao kwa mtu
aliyekuwa pale ukumbini atakubali kuwa
show yao ilishangiliwa sana
Baadaye walifuata Mi Casa Music na wao
wakadhihirisha kwanini ni kundi bora la
muziki wa house kwa sasa nchini Afrika
Kusini kwa kupiga show kali sana.
Diamond alifuata na kama kawaida wakati
anaingia alishangiliwa mno. Kama
kawaida yake, aliungana na dancers wake
wanne waliokuwa wakimpa support.
Ilikuwa show ya kawaida iliyoboa kwa
muda mfupi tu.
Ushauri wangu kwa Diamond ni kuwa
asiconcentrate sana katika kucheza na
kusahau kujiimarisha katika uimbaji wa
live. Haoneshi ujuzi wowote wa kuziimba
nyimbo zake kiustadi anapokuwa stejini.
Kwakuwa hujikuta akicheza mno na
hivyo kuchoka haraka, sauti yake
huharibika na kusikika vibaya na
huondoa kabisa ule uprofesheno wa sauti
ya msanii anayependwa na mwenye hits
nyingi. Kama angekuwa anaimba na
vyombo live show ingekuwa inapewa jeki
na muziki tofauti unaopigwa na bendi.
Atafute namna nyingine ya kiubinifu
zaidi ya uimbaji wa nyimbo zake live.
Asitumbuize nyimbo kama zinavyosikika
kwenye CD. Kama ataendelea na
performance za kutumia DJ na CD, basi
atengeneze version tofauti za beats
atakazotumia kuimba live. Madhara ya
hiki anachokifanya sasa ataonekana kama
dancer badala ya kuwa muimbaji, sifa
aliyonayo Cabo Snoop.
Kelele na shangwe anazozipata akiwa
anatumbuiza zisimdanganye kuwa
anazikonga nyoyo za mashabiki kwa
performance kali kwakuwa ukweli ni
kwamba shangwe nyingi ni kwasababu
nyimbo anazoimba ni hits na wengi
wanazifahamu. Kwa perfomance ya aina
ile kama angekuwa ni msanii asiye na
jina, wengi wasingekuwa wanarespond
hivyo.
Shabiki hapendi kwenda kumuona msanii
ambaye nyimbo zake hutumbuiza nyimbo
zake vilevile kama zinavyosikika redioni.
Kwa walioshuhudia show ya P-Square
November mwaka jana pale Leaders Club
waliona jinsi mapacha hao walivyo
wachawi wa live performance.
Pamoja na kuwa wachezaji wazuri,
hawakuwa wakicheza katika kila wimbo.
Muda mwingi walikuwa wakiimba nyimbo
zao kwa hisia na kuinteract vizuri na
watazamaji.
Kwakuwa kutajwa kwake kwenye tuzo
hizo kubwa kutampa exposure zaidi na
kupata show za kimataifa, alifanyie kazi
hilo ili kutowapa sababu wakosoaji na
kumuona kama amebebwa tu kufika
hapo.
Bongo5
Sunday, May 18, 2014
ADAMU KUAMBIANA KUZIKWA JUMANNE
Mwili wa muigizaji Adam Kuambiana ambaye pia
alikuwa director wa filamu nchini aliyefariki jana
alfajiri utaagwa kesho Jumatatu, Jumanne mwili
huo utapelekwa viwanja vya Leaders Club
ambapo mashabiki wake watapata nafasi ya
kuuaga. Atazikwa katika makaburi ya Kinondoni,
Dar e salaam hiyo hiyo Jumanne kwa mujibu wa
taarifa iliyotolewa na mkewe anayeitwa Janeth
Saturday, May 17, 2014
SHOCKED :MSANII WA FILAMU ADAMU KUAMBIANA AFARIKI DUNIA
Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa
mwigizaji Adam Kuambiana (pichani)
amefariki Dunia. Bado tunafuatilia taarifa hizi
kwa undani na tutawaletea habari kamili
punde zikiwa tayari.
Friday, May 16, 2014
MPOKI HANA AKILI KABISA .SOMA HAPA CHINI....
MPOKI HANA AKILI KABISA, AZIDI
KUWACHAFUA WATU KIBAO KWA MADAI
KUWA NI UTANI...CHEKI HAPA
Stori: JOSEPH SHALUWA
IMETHIBITIKA bila shaka yoyote kuwa
msanii aliyebahatika kuwa maarufu wa
vichekesho Bongo, Silvery Mjuni ‘Mpoki’
au Bepari la Kihaya ni mjinga yaani 0
brain kwa Kimombo, Gazeti kiongozi kwa
habari za mastaa Ijumaa limejiridhisha.
Msanii aliyebahatika kuwa maarufu wa
vichekesho Bongo, Silvery Mjuni ‘Mpoki’
au Bepari la Kihaya.
Hata hivyo, ikiwa msanii huyo ambaye
kwa fikra zake anaamini ndiye mkali
kuliko wachekeshaji wote Bongo
japokuwa Mzee Majuto ndiye namba
moja, anaweza kuwa mwerevu badala ya
kuendelea kuwa mjinga.
KWA NINI MJINGA?
Kwa mujibu wa Kamusi ya Kiswahili
Sanifu (Oxford – Toleo la Pili)
inamuelezea mjinga kuwa ni mtu asiyejua
kitu au jambo fulani.
Hata hivyo, mjinga hawezi kuendelea
kubaki katika hali hiyo baada ya
kufundishwa na kujua maana.
HABARI KAMILI
Tukio la Mpoki hivi karibuni
kuwadhalilisha watu waliofika jukwaani
kukabidhi tuzo kwa washindi katika Tuzo
za Kilimanjaro Tanzania Music Awards
(KTMA) kwenye Ukumbi wa Mlimani City
jijini Dar ni ushahidi tosha kuwa ana
tatizo la kufikiri.
Ukiachana na tukio hilo, rekodi yake ya
maisha yake ya kisanii na nje ya sanaa
inathibitisha asivyo hodari wa kutumia
ubongo wake sawasawa, vijana wa mtaani
huita zero brain (0).
Kwa uelewa wake, uchekeshaji ni
udhalilishaji ndiyo maana vipande vingi
anavyoigiza huwa anawasema watu
vibaya hata wale ambao wamemsadia
kufika alipo kisanii.
TUZO ZA KILI
Katika hali ya kawaida, kwa mtu asiye
mjinga na anayejitambua, Mpoki
asingeweza kumkejeli mtu mwenye
heshima zake kama Asha Baraka ambaye
ni Mkurugenzi wa Aset.
Silvery Mjuni ‘Mpoki’ akiwa kazini.
Asha anaweza kuwa mama yake lakini
bila haya alimwambia mbele ya hadhara
kuwa kwa alivyo na mwonekano mzuri
kwa usiku ule, asubuhi yake angeweza
kusalimiwa shikamoo (akimaanisha
angekuwa na mwonekano wa kizee kwa
kuwa hatakuwa na make up tena).
Hakuishia hapo, Mpoki alifikia hatua ya
kuingilia hadi mambo binafsi ya watu
ambayo katika hali ya kawaida hayawezi
kuwa utani, alimwambia Maimartha Jesse
kuwa licha ya kwamba ananyonyesha
lakini amepiga matiti jeki. Upuuzi mtupu!
NJE YA KILI
Ukiachana na kero alizotoa kwenye
jukwaa lile linaloheshimika, Mpoki ana
tabia ya kuwadhalilisha watu hata
anapokuwa kwenye kazi zake. Mifano ipo
mingi.
Kutokana na kile kinachoonekana
kutojielewa, Mpoki humkejeli mtu
makusudi ili kutengeneza bifu akiamini
magazeti yakimwandika ataendelea kuwa
juu.
Hivi karibuni alitoa wimbo ambao ndani
yake amewatukana baadhi ya watu
akiwemo mwandishi mmoja mashuhuri
nchini wa magazeti pendwa kwa kumuita
dada wakati akijua ni mwanaume
(anapenda misala).
Kwa akili zake fupi, aliamini paparazi
huyo angepaniki na kurushiana naye
maneno kwenye magazeti na mitandao ya
kijamii, hakufanya hivyo na mpaka sasa
yuko kimya kabisa kama hakuna kitu
kilichotokea kwa sababu ni mwerevu.
Pia jamaa huyo bila haya wala soni
aliwahi kuigiza kwa kumkejeli
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,
Reginald Mengi kwenye maigizo yao ya
Orijino Komedi.
Ikumbukwe kuwa, Televisheni ya Afrika
Mashariki (EATV) inayomilikiwa na mzee
Mengi ndiyo iliyorusha kipindi chao cha
vichekesho kwa mara ya kwanza. Kifupi
ndiye aliyemtoa baada ya kupigika kwa
muda mrefu.
Mpoki alitambulishwa kwa mara ya
kwanza na Runinga ya ITV akiwa na
Kundi la Nyota Ensemble kupigtia Kipindi
cha Mambo Hayo cha ITV ambacho ni
mali ya mzee Mengi.
WADAU WACHARUKA
Wadau wa burudani Bongo waliopata
kuzungumza na Ijumaa kwa nyakati
tofauti, walionesha hisia zao za wazi kwa
namna walivyokasirishwa na msanii huyo
mwenye mdomo mchafu na asiyepima
maneno.
Wapo waliokwenda mbali zaidi kwa
kusema kwamba ikiwa kutakuwa na
shughuli yoyote ya kiburudani na msanii
huyo akapangwa kuwa MC basi
hawatahudhuria kwa kuogopa
kudhalilishwa.
Nasra Abdillah wa Tabata jijini Dar
alisema: “Mimi nahisi kuna kitu cha zaidi
kwa Mpoki, si kwamba ni mchekeshaji,
nadhani kichwani hayupo vizuri. Mimi
nilikwenda Mlimani City siku ile, kuna
ndugu yangu alikuwa mmoja wa watoa
tuzo.
“Alipoona kila anayepanda anadhalilishwa
(ingawa kwa Mpoki ni utani) akaingiwa
hofu. Ilifika mahali akatamani kuahirisha
kwenda kutoa tuzo, tukampa moyo lakini
alipopanda mambo yakawa yaleyale,
akadhalilishwa waziwazi.
“Mpoki anatakiwa kubadilika. Nampa
ushauri wa bure, ajifunze kupitia kwa
wengine. Lakini hata hivyo mimi popote
ambapo yeye atakuwa mshereheshaji,
sitakanyaga hata kwa dawa.”
Dulla wa Sinza Kwaremmy alisema:
“Sikufurahishwa na kitendo cha
kumwambia Dj Bon Love na wadogo zake
kwamba ni wabahili wa fedha na
kumshangaa Vanessa Mdee kwa
kuzungumza Kiingereza wakati yeye ni
Mpare azungumze Kiswahili, halafu
akamkejeli eti awe anafanya mazoezi ya
kuvaa viatu virefu baada ya kunusurika
kuanguka jukwaani. Ule si utani ni
udhalilishaji.”
Mdau mwingine ambaye hakutaka
kutajwa jina lake alisema:
“Sikufurahishwa kabisa alivyomwambia
Isha Mashauzi, eti ni mwanamke wa
Kikurya, si wa kuoa.
Lakini mbaya zaidi akamwambia make up
zilimfanya aonekane msichana mrembo,
lakini akiamka asubuhi atapewa shikamoo
kwa mwonekano mpya atakaokuwanao.
Ile ilikuwa too much. Kifupi Mpoki ni
mpuuzi sana.”
HUYU AWAKUMBUKA TAJI, MILLARD
NA PENNY
January Kingamkono wa Msasani Dar,
yeye alikwenda mbali zaidi na
kuwakumbuka washereheshaji wa siku
zote katika hafla hiyo, Taji Liundi, Millard
Ayo, Jokate Mwegelo, Penniel Mungilwa
‘Penny’ na wengineo.
Hapa anafafanua: “Kili walichemsha kwa
kweli. Kumkaribisha Mpoki lilikuwa wazo
zuri lakini mizaha yake ilikuwa ya kijinga
sana. Alikuwa akiwatusi na kuwakejeli
watu na si kuchekesha. Nawashauri Kili
wafikirie kuwarudisha akina Taji na
wengine waliokuwa wakifanya vizuri kwa
pamoja kama kweli wanataka hafla yao
iwe na msisimko.
“Wakumbuke Tuzo za Kili siyo free event
(onesho la bure), watu wanatoa pesa zao.
Sasa lazima wazingatie kuwa
kinachotolewa kwa watazamaji
kinalingana na hela iliyolipwa. Kifupi
Mpoki aliboa,” alisema Kingamkono.
HUYU ATAKA AOMBE RADHI
Mdau mwingine, Juma Alii wa Manzese ya
Tip Top jijini Dar alisema: “Mpoki
anatakiwa kujifunza. Kila kona sasa hivi
gumzo ni yeye. Nasikia wale mastaa
waliokejeliwa wanataka kumfungulia
kesi, ni vyema ajifunze kusoma alama za
nyakati. Ajue alikosea na aombe radhi.
“Lakini pia ni vizuri kama atajifunza
kutoka kwa washereheshaji wengine,
namna wanavyofanya kazi kwenye
matukio rasmi kama hayo.”
TAJI ASHAURI
Mkongwe katika tasnia ya utangazaji
Bongo, Taji Liundi aliona kasoro za
Mpoki. Hata hivyo, kwa kutumia busara
alitupia katika ukurasa wake ndani ya
Mtandao wa Kijamii wa Facebook
akizungumzia hafla hiyo ambapo
aliandika: “Nadhani ingekuwa vema
kutambulisha wasoma tuzo vizuri.
Kuna mtu mmoja “Mhaya Mweupe”
angestahili kuwasilisha kwa umakini
zaidi!! Pia tunasikia mazungumzo ya
watangazaji na watu nyuma ya jukwaa
kupitia mic zisizozimwa. Onesho lina
msisimko lakini nadhani “production”
imekuwa na changamoto!
Maneno hayo yalitupiwa na Taji, Mei 4,
mwaka huu muda mfupi tu wadau
wakaibuka na kulipuka. Wa kwanza
alikuwa ni Dinne Shose ambaye
aliandika:
“Yaani Taji nimeliwaza hilo nikawa
nawaambia wadogo zangu...imekuwaje?
Wapi Taji?...ma MC hawana mvuto...utani
upo lakini hauchangamshi matokeo yake
utani umezidi hadi unaboa watu...wish
Taji, Millard, Jokate na Penniel mngekuwa
ma MC.”
Mara moja, Taji akajibu: “Dinne ahsante
kwa maoni. Sisi wazoefu tutapata
majukwaa mengine. Nadhani Shadee
kajitahidi sana lakini shoo ilikuwa ndefu,
focus inaweza kupotea. Mpoki katumia
mtindo wa Kevin Hart akiwa ana-MC
BET.”
TAJI AMTOLEA UVIVU
Baada ya mjadala kuwa mkali huku
wachangiaji wengi wakipeleka lawama
zao moja kwa moja kwa Mpoki, Taji
aliamua kumtolea uvivu kwa kuandika
hisia zake kwa ukweli kuhusu ubovu wa
aliouita utani lakini kumbe ni
udhalilishaji.
Sehemu ya maandishi ya Taji
yanasomeka: “Hakuna shaka kwamba
Mpoki ni mchekeshaji mzuri. Hapo juu
nimeelezea mtindo wake wa kukejeli
alipoutoa. Ni kwa mchekeshaji mwenzake
Kevin Hart. Je, alipitiliza? Nadhani
NDIYO. Kwa Bon Luv na Ray Kigosi.
Sikumwelewa Mpoki. Nadhani Martin
Kadinda naye hakupendezwa.
“Hapo sasa kuna tofauti ya KUCHEKESHA
na KUBEZA, pia ya kuwa MC! Kasoro
nyingine niliyoiona ni kurusha watu,
Fina, Ruge... Sijui kama ilikuwa kwenye
script. Mchango wa Fina unaeleweka
kupitia OnePlus (kejeli za Mngoni kuzaa
na Mzungu hazikuwa na ladha).
“Naamini Mpoki atapokea maoni chanya
ili aweze kuji-balance akifungua mdomo.
Ajipange. Kuna kitu kinaitwa MANENO
MATUPU, kama vile kujitangaza kuwa ni
MC wa harusi angali anafanya KTMA mara
ya pili na kuaminika, masuala ya kulipwa
ontime mbele ya Kavishe???? Matani ya
“kiutu uzima” kwenye Live TV, watoto
wanaangalia!!
“Anyway, yote haya hayatakosa
kukosolewa kwa tamasha kubwa kama
lile. Nadhani hakuna mchangiaji
anayechukia KTMA. Kuomba ushauri
wasiache.
Ikiwa watu wanalewa ukumbini,
unategemea nini kama nusu ukumbi
ukiamka kumtuza, kumtukana Diamond
au kuwafuata wasanii backstage? Dah!!
Kungekuwa na bucket la maji kwa kila
mchemshaji! Ni kusema lile tangazo nalo
tata! Si Sprite vile? Naona kama watu
watamwagiana pombe??!”
MDAU MWINGINE
Edwine Ndaki alisema: “ Taji Liundi upo
sahihi, nimependa ulifanya uchambuzi na
ushauri. Kwa sisi tulio nje ya nchi
tunapongeza kwa wazo la kurusha event
live online. Mpoki next time au popote
inabidi aangalie utani gani na wapi.”
JIMMY CHOCOLATE MKATTE
“Iko haja ya ma - MC kufanyiwa rotation,
rafiki yangu Mpoki alibweteka
akamnyima Co - MC nafasi. That was
illegal.”
BINTI SHANGWE
“Kasoro kibao, MC wameboa, hakuna
mpangilio, huyu hajamaliza kuongea,
huyu kashadakia, hasa Mwarabu wa
Dubai, mtu anayetaja jina la mshindi na
MC inabidi wapokezane mic...”
KILI: HATUKUJUA KAMA ANGEHARIBU
Mmoja wa wanakamati ya maandalizi ya
tuzo hizo, kwa sharti la kutotajwa jina
lake gazetini kwa maelezo kuwa si
msemaji, alizungumzia kuhusu
udhalilishaji uliofanywa na Mpoki,
akasema hawakujua kama angefanya vile.
“Tulimwamini maana tulishawahi kufanya
naye kazi. Kilichotokea pale
kilitushangaza sana lakini isingekuwa
rahisi kumrekebisha wakati akiwa tayari
yuko jukwaani. Pengine utekelezaji wa
hilo ungesababisha tatizo jingine kubwa
zaidi. Niseme tu, tumejifunza.”
KUTOKA DAWATI LA IJUMAA
Mpoki, wewe ni staa na una heshima
kubwa kwenye jamii. Kila binadamu
amepewa akili; uwezo wa kufikiri upo
kwa kila mmoja tatizo ni pale kwenye
uamuzi wa kutumia. Ni vyema sasa
ukabadilisha staili ya maisha na uanze
kutumia akili yako ipasavyo.
Vichekesho siyo kuwadhalilisha watu,
lakini kubwa zaidi kumbuka ulipotoka,
acha kuwakejeli hadi waliokusaidia –
hata hivyo si uungwana kuwadhalilisha
watu.
Badilika ili uondoke kwenye ujinga kwa
kuchekesha vitu vyenye mantiki ili uwe
mwerevu. Inawezekana ukiamua! –
MHARIRI.
source; GPL
T.I.D NA RECHO KTK MAHABA MAZITO
YOU HEAARRDDD: T.I.D NA RECHO KATIKA
MAHABA MAZITO
Taarifa zinazotolewa na Ma snitch wa kitaani
zinadai kuwa Wasanii T.i.D na Mwanadada
Recho wako katika dimbwi zito la mahaba kwa
zaidi ya miezi mitatu sasa wamekua
wakionekana wakiwa pamoja hadi kwenye show
za T.i.D mikoani ingawa wao wenyewe
hawataki mahusiano yao yawe wazi kwa jamii,
hata mhariri wetu Gossip Cop Soudy Brown
alipojaribu kuwacheki kupitia simu zao za
mkononi wote walikanusha na T.I.D akadai
kuwa eti etiiiii amewahi kukutana na Recho
mara mbili tu.
Taarifa nyingine zinasema Recho sasa hivi
hataki hata kupiga deal zake za muziki zaidi ya
kuwa pembeni ya mzee mnyama, so mara zote
anashinda kinondoni kwa kina mzee kigogo.
YOU HEEEARRRDDDD!!!
Tuesday, May 13, 2014
NAY WA MITEGO APEWA MAKAVU NA MASHABIKI
OMA KWELI ! MASHABIKI ‘WAMPA MAKAVU
LIVE" NAY WA MITEGO BAADA YA KUDAI
KUWA NDIYE RAPPER BORA ZAIDI
TANZANIA...JIONEE HAPA
Nay wa Mitego anaamini kuwa ukimto
Profesa Jay wa zamani (anadai huyu w
sasa kachoka) yeye ndiye rapper bora
zaidi kuliko mwingine Tanzania. Laki
mashabiki wanaikubali kauli hiyo? Hel
NO!!
Octavian Kiwale
Unatafuta kick tu wewe, nadhubutu
kukuambia ukizungumzia HIP HOP hat
killer tu hujamfikia ndo ujiringanishe
Prof?//////// FID Q ndo usimwongelee
kabisa
Winnie Glory
We ney fid Q na joe makin huwafiki h
robo, mbuz tu wew ndo man unalelew
na siwema
TheBoy Junior
Na je nakula ujana ipo wapi hip hop a
bongo fleva na akisema ye ndo anaong
ukweli nash mc tumuweke wapi sasa?
Asitafte kiki wasanii wa hip hop wengi
na wanafanya vile hip hop inapaswa
kuwa. Huyu hana jipya tena tafta
Scandal utoke kama diamond na si
kwakusema we ndo hip hop hata hip h
yenyewe huijui….
Agapito Petro
Mwana fa,ngwair(r.i.p.),kala jere100,
n.k. Huwafikii hata kiduchu
Laurent Mwamlima
Ney umeishaaaa… kajititie tu Hata
MPOKI MJUNI hata mzee MGARI
humfikii kwa hip hop
Vitalis Kaizer
Hata 50 bora ya hip hop sidhani kama
umo bado sanaaaaaaa kuropoka sio hi
hop jipangee!!
Dotto Kondo
Huyu jamaa bhana,sometimes nahc
huwa akili zinamruka
Ze Jap Suprah
Chiz wewe mwambie aandike kip
sijasikia hafu tuone
Rashid Mtoi
Dogo janja mwenyewe humfikii hata
robo
HUYU DADA AFUNGUKA YA MOYONI
Huyu Dada anaishi maeneo ya kijitonyama dar aamua kuwafungukia wanaume ambao huwa wanamtoa matenga wakati wa tendo la ndoa.
Monday, May 12, 2014
HATARI SANA MTOTO ATUMIA NDUMBA KUSOMA
Mtoto mmoja ambaye jina (lake kapuni) ameweza kuonyesha uchawi hadharani kwa kuweka dawa yake juu ya dawati.
WASICHANA WALIOTEKWA NA BOKO HARAMU
Wasichana ambao kundi la Boko Haram liliwateka
nyara
Kiongozi wa kundi la Boko Haram Abubakar
Shekahu amesema kuwa atawaachilia huru
wasichana waliotekwa nyara iwapo tu wapiganaji
wa kundi hilo wanaozuiliwa na serikali ya
Nigeria wataachiliwa huru.
Katika kanda mpya iliyotolewa na kundi hilo,
kiongozi huyo, amesema kuwa wasichana hao
waliweza kusilimu katika kipindi cha wiki nne
zilizopita tangu watekwe nyara.
Kanda hiyo inaonyesha zaidi ya wanawake
miamoja wakiwa wamevalia hijabu na kuswali.
Abubaka Shekau anasema kuwa wanawake hao
ni wasichana waliotekwa nyara na kundi hilo.
Walitekwa nyara kutoka katika shule yao mjini
Chibok, Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo
Rais wa Ufaransa amejitolea kuwa mwenyeji wa
mkutano utakaotafuta njia za kupambana na
Boko Haram.
JAMANI JACQUELINE WOLPER A.K.A GAMBE ALEWA HADI KUANGUKA
Staa wa sinema za Kibongo,
Jacqueline Wolper Massawe
anadaiwa kuwa tilalila na kujikuta
akipiga mwereka kwenye shughuli ya
kibao kata cha mwigizaji mwenzake,
Vanita Omary.
Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline
Wolper Massawe baada ya kuanguka.
Kwa mujibu wa ‘shushushu’ wetu
aliyekuwa ndani ya nyumba, tukio
hilo lilijiri kwenye Ukumbi wa PG
Hall (zamani FM Club), Kinondoni
jijini Dar ambapo mastaa kibao
walihudhuria.
Ndani ya kibao kata hicho, Wolper
alicharuka kipombepombe kwa
kucheza ovyo na kukimbiakimbia
akiwa tilalila.
Katika kukimbia huko, ndipo akapiga
mwereka na kuanguka huku
akijaribu kusimama kwa
kuchechemea.
Baadhi ya wageni waalikwa walibaki
wakimshangaa na kusema kuwa
hapendezi akinywa pombe kwani
ustaarabu wote unapotea.
Mbali na pombe pia alikuwa kivutio
kwa staili ya ukataji wake wa mauno
akiwa na kivazi kilichoacha nje
mapaja yake akiwa na rafiki yake
aliyetajwa kwa jina moja la Vivi.
Katika hatua nyingine, Vanita
alijikuta akiangua kilio baada ya
wapiga ngoma wa kibao kata ‘kuwa
feki’ na kushindwa kufanya kazi
kama walivyoahidi.
Mshereheshaji akimvaa Vanita.
Kutokana na hilo, baadhi ya mastaa
kama Aunt Ezekiel na Yobnesh Yusuf
‘Batuli’ waligoma kucheza na
kukizomea kibao kata hicho ambacho
kililetwa na MC (jina linahifadhiwa)
akidai kuwa amewatoa Bagamoyo na
wana ufundi wa hali ya juu.
Mwisho wa shughuli, MC huyo
alimvaa Vanita akitaka alipwe
pamoja na kwamba wapiga ngoma
wa kibao kata hicho walishindwa
kazi hivyo kukaibuka mtiti wa aina
yake huku kila mtu akitimua zake.
Friday, May 9, 2014
MH OMMY DIMPOZ ATUKANWA NA MASHABIKI
Ilikua ni siku ya tuzo za Kilimanjaro ambapo Msanii huyo alipovaa viatu vilivyotatanisha na kujiuliza vya kike au kiume.
Thursday, May 8, 2014
ONA DIAMOND NA WEMA WALIVOMFANYIA UMAFIA JOKETI KWA KUPIGANA DENDA MBELE YAKE
WAKATI msanii wa kizazi kipya anayefanya
vizuri kwa sasa na kujizolea tuzo 7
alizokuwa anawania kupitia Kilimanjaro
Tanzania Music Awards 2014, Naseeb Abdul
'Diamond akiibuka shujaa Mlimani City jijini
Dar ambako hafla hiyo ya utoaji tuzo
ilifanyika, usiku huo ulikuwa mbaya kwa
mpenzi wake wa zamani,Jokate Mwegelo
ambaye huenda alijuta kufika mahali hapo....
Matukio ambayo yalimnyong'onyesha Jokate
ni namna ambavyo msanii huyo na mpenzi
wake Wema Sepetu walivyokuwa wakionyesha
mahaba mazito ukumbini ilihali yeye
akishuhudia....
Katika hali ya kushangaza, Diamond na Wema
kila walipokuwa wakichukua tuzo walikuwa
wakizunguka nyuma ya jukwaa ambako
alikuwepo Jokate na kuzibwaga tuzo hizo
mezani kisha kukandamiza 'Denda Live'
mbele yake kiasi cha kumfanya
mwanamitindo huyo ainame kwa Aibu....
Diamond alionekana kumpotezea vibaya
mwandani wake huyo wa zamani huku
Wema akijikosha kwa kumpa mkono wa
kejeli hali iliyomfanya Jokate akose raha
wakati wote alipokuwa akiwaona wapenzi
hao....
Matukio ambayo yalionekana kumchoma zaidi
moyoni ni jinsi Wema alivyokuwa akimvuta
Diamond na kubadilishana mate mbele yake
jambo ambalo lilitafsriwa kama ni kumfanyia
makusudi mwanamitindo huyo ambaye kipindi
cha nyuma alifanikiwa kuleta tafrani kubwa
na kuligawa vipande vipande penzi la wawili
hao kiasi cha Wema kulalamika redioni....
Hali ya Jokate kukumbwa na mfadhaiko
ilizua minong'ono kwa baadhi ya mashuhuda
kwamba Diamond na Wema waliamua kukata
kabisa mzizi wa fitina kwa Jokate na
kuudhihirishia umma kuwa ya kale ni
dhahabu...
"Maskini Jokate, ona anavyofanyiwa na
Wema,inauma sana moyoni.Unajua mwanaume
kama umewahi kulala naye hata mara moja
ukiona anafanya mahaba na mwanamke
mwingine inauma" Alisikika staa mmoja
akiteta na mwezake
Hadi hafla hiyo inamalizika,Jokate aliganda
kwenye kiti akiwa amepooza tofauti na ilivyo
kwa staa huyo anapokuwa katika matukio
makubwa kuwa na makeke
Saturday, May 3, 2014
CHEKI LIVE TUZO ZA KILIMANJARO TANZANIA
1. WIMBO BORA WENYE VIONJO VYA ASILI
YA TANZANIA - Bora Mchawi, Dar Bongo
Massive
2. MSANII BORA CHIPUKIZI ANAYEIBUKA -
Young Killer
3. WIMBO BORA WA ZOUK - Yahaya, Lady
Jaydee
4. WIMBO BORA WA AFRO POP - Number
One, Diamond Platnumz
5. WIMBO BORA WA RAGGA / DANCEHALL
- Nishai Chibwa Ft Juru
6. WIMBO BORA WA RAGGAE - Niwe na
wewe, Dabo
7.WIMBO BORA WA TAARAB - Wasiwasi
wako, Mzee Yusuf
8. KIKUNDI CHA MWAKA CHA TAARAB -
Jahazi Modern Taarab
9. MWIMBAJI BORA WA KIKE TAARAB -
Isha Ramadhani
10. MWIMBAJI BORA WA KIUME TAARAB -
Mzee Yusuf
11. WIMBO BORA WA KISWAHILI BENDI -
Ushamba mzigo, Mashujaa Band
12. MWIMBAJI BORA WA KIKE BENDI -
Luiza Mbutu
13. MWIMBAJI BORA WA KIUME BENDI -
Jose Mara
14. RAPA BORA WA MWAKA BENDI -
Furguson
15. BENDI YA MWAKA - Mashujaa Band
16. MWIMBAJI BORA WA KIKE, KIZAZI
KIPYA - Lady Jaydee
17. MWIMBAJI BORA WA KIUME, KIZAZI
KIPYA - Diamond
18. KIKUNDI CHA MWAKA CHA KIZAZI
KIPYA - Weusi
19. WIMBO BORA WA RNB - Closer,
Vanessa Mdee
20. WIMBO BORA WA HIP HOP - Nje ya
Box, Nick wa Pili Ft Joh Makini & Gnako
21. MSANII BORA WA HIP HOP - Fid Q
22. WIMBO BORA WA KUSHIRIKISHA /
KUSHIRIKIANA - Muziki Gani, Nay wa
Mitego ft Diamond
23. WIMBO BORA WA AFRIKA MASHARIKI
- Tubonge, Jose Chameleone
24. MTUNZI BORA WA MWAKA TAARAB -
Mzee Yusuf
25. MTUNZI BORA WA MWAKA BENDI -
Christian Bella
26. MTUNZI BORA WA MWAKA KIZAZI
KIPYA - Diamond
27. MTUNZI BORA WA MWAKA HIP HOP -
Fid Q
28. MTAYARISHAJI BORA WA NYIMBO WA
MWAKA TAARAB - Enrico
29. MTAYARISHAJI BORA WA NYIMBO WA
MWAKA BENDI - Amoroso
30. MTAYARISHAJI BORA WA NYIMBO WA
MWAKA KIZAZI KIPYA - Man walter
31. HALL OF FAME - Hassan Rehani
Bitchuka
32. HALL OF FAME INSTITUTION - Masoud
Masoud
33. VIDEO BORA YA MUZIKI YA MWAKA -
Number One, Diamond Platinumz
34. WIMBO BORA WA MWAKA - Number
One, Diamond Platinumz
35. MTUIMBUIZAJI BORA WA KIKE WA
MUZIKI - Isha Ramadhani
36. MTUIMBUIZAJI BORA WA KIUME WA
MUZIKI - Diamond Platinumz