Wasichana ambao kundi la Boko Haram liliwateka
nyara
Kiongozi wa kundi la Boko Haram Abubakar
Shekahu amesema kuwa atawaachilia huru
wasichana waliotekwa nyara iwapo tu wapiganaji
wa kundi hilo wanaozuiliwa na serikali ya
Nigeria wataachiliwa huru.
Katika kanda mpya iliyotolewa na kundi hilo,
kiongozi huyo, amesema kuwa wasichana hao
waliweza kusilimu katika kipindi cha wiki nne
zilizopita tangu watekwe nyara.
Kanda hiyo inaonyesha zaidi ya wanawake
miamoja wakiwa wamevalia hijabu na kuswali.
Abubaka Shekau anasema kuwa wanawake hao
ni wasichana waliotekwa nyara na kundi hilo.
Walitekwa nyara kutoka katika shule yao mjini
Chibok, Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo
Rais wa Ufaransa amejitolea kuwa mwenyeji wa
mkutano utakaotafuta njia za kupambana na
Boko Haram.
Monday, May 12, 2014
WASICHANA WALIOTEKWA NA BOKO HARAMU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment