Tuesday, May 20, 2014

DIAMOND BADILIKA KABLA MAMBO HAYAJAHARIBIKA.

Kwa Staili Hii Diamond Badilika Kabla Mambo
Hayajaharibika..Kwa Mengine Hongera.
Mwaka 2014 umekuwa ni mwaka wenye
neema nyingi kwa Diamond Platnumz
kimataifa. Tangu aachie video ya remix ya
My Number One aliomshrikisha Davido,
jina la staa huyo limekuwa kubwa kiasi
cha sasa kumfanya afike sehemu ambayo
hakuna msanii wa Tanzania aliyewahi
kufika.
Kuanzia video yake kushika namba moja
kwenye vitu vikubwa vya TV kikiwemo
Trace TV, kutajwa kuwania tuzo za MTV
MAMA katika vipengele viwili na pia
kutajwa kuwania tuzo za BET kwenye
kipengele cha Best International Act:
Africa. “An international music superstar
from Tanzania is being born right before
our eyes. Hongera sana
@diamondplatnumz,” alitweet January
Makamba.
Ni kweli, supastaa wa kimataifa kutoka
Tanzania amezaliwa mbele ya macho yetu
na ni wajibu wetu kumuunga mkono
katika kila hatua anayoenda. Lakini kama
unamtakia mtu heri na mafanikio zaidi, si
lazima kumsifia muda wote. Ni vyema
kumwambia ukweli pale ambapo tunahisi
anatakiwa kuparekebisha ili asonge
mbele zaidi.
Jambo muhimu ambalo Diamond
anatakiwa kurekebisha ni katika live
performance. Naomba nikiri kuwa pamoja
na kuwa shabiki mzuri wa nyimbo nyingi
za Diamond, sijawahi kupenda
performance zake za live. Nimeshamhudia
kwa zaidi ya mara 10 akitumbuiza na zote
nimekuwa nikimuona akifanya vilevile na
sipati kile ambacho nakuwa nakitegemea.
Juzi alikuwa mmoja wa wasanii
waliotumbuiza kwenye show ya Road to
MAMA ya MTV Base iliyofanyika Club
Bilicanas akiwa pamoja na Sauti Sol na
kundi la Mi Casa Music. Bahati mbaya
ama nzuri kwake ni kwamba kutokana na
kuwa msanii mwenyeji, yeye alikuwa
msanii wa mwisho kutumbuiza. Walianza
Wakenya Sauti Sol ambao kwa mtu
aliyekuwa pale ukumbini atakubali kuwa
show yao ilishangiliwa sana
Baadaye walifuata Mi Casa Music na wao
wakadhihirisha kwanini ni kundi bora la
muziki wa house kwa sasa nchini Afrika
Kusini kwa kupiga show kali sana.
Diamond alifuata na kama kawaida wakati
anaingia alishangiliwa mno. Kama
kawaida yake, aliungana na dancers wake
wanne waliokuwa wakimpa support.
Ilikuwa show ya kawaida iliyoboa kwa
muda mfupi tu.
Ushauri wangu kwa Diamond ni kuwa
asiconcentrate sana katika kucheza na
kusahau kujiimarisha katika uimbaji wa
live. Haoneshi ujuzi wowote wa kuziimba
nyimbo zake kiustadi anapokuwa stejini.
Kwakuwa hujikuta akicheza mno na
hivyo kuchoka haraka, sauti yake
huharibika na kusikika vibaya na
huondoa kabisa ule uprofesheno wa sauti
ya msanii anayependwa na mwenye hits
nyingi. Kama angekuwa anaimba na
vyombo live show ingekuwa inapewa jeki
na muziki tofauti unaopigwa na bendi.
Atafute namna nyingine ya kiubinifu
zaidi ya uimbaji wa nyimbo zake live.
Asitumbuize nyimbo kama zinavyosikika
kwenye CD. Kama ataendelea na
performance za kutumia DJ na CD, basi
atengeneze version tofauti za beats
atakazotumia kuimba live. Madhara ya
hiki anachokifanya sasa ataonekana kama
dancer badala ya kuwa muimbaji, sifa
aliyonayo Cabo Snoop.
Kelele na shangwe anazozipata akiwa
anatumbuiza zisimdanganye kuwa
anazikonga nyoyo za mashabiki kwa
performance kali kwakuwa ukweli ni
kwamba shangwe nyingi ni kwasababu
nyimbo anazoimba ni hits na wengi
wanazifahamu. Kwa perfomance ya aina
ile kama angekuwa ni msanii asiye na
jina, wengi wasingekuwa wanarespond
hivyo.
Shabiki hapendi kwenda kumuona msanii
ambaye nyimbo zake hutumbuiza nyimbo
zake vilevile kama zinavyosikika redioni.
Kwa walioshuhudia show ya P-Square
November mwaka jana pale Leaders Club
waliona jinsi mapacha hao walivyo
wachawi wa live performance.
Pamoja na kuwa wachezaji wazuri,
hawakuwa wakicheza katika kila wimbo.
Muda mwingi walikuwa wakiimba nyimbo
zao kwa hisia na kuinteract vizuri na
watazamaji.
Kwakuwa kutajwa kwake kwenye tuzo
hizo kubwa kutampa exposure zaidi na
kupata show za kimataifa, alifanyie kazi
hilo ili kutowapa sababu wakosoaji na
kumuona kama amebebwa tu kufika
hapo.
Bongo5

No comments:

Post a Comment