Staa wa sinema za Kibongo,
Jacqueline Wolper Massawe
anadaiwa kuwa tilalila na kujikuta
akipiga mwereka kwenye shughuli ya
kibao kata cha mwigizaji mwenzake,
Vanita Omary.
Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline
Wolper Massawe baada ya kuanguka.
Kwa mujibu wa ‘shushushu’ wetu
aliyekuwa ndani ya nyumba, tukio
hilo lilijiri kwenye Ukumbi wa PG
Hall (zamani FM Club), Kinondoni
jijini Dar ambapo mastaa kibao
walihudhuria.
Ndani ya kibao kata hicho, Wolper
alicharuka kipombepombe kwa
kucheza ovyo na kukimbiakimbia
akiwa tilalila.
Katika kukimbia huko, ndipo akapiga
mwereka na kuanguka huku
akijaribu kusimama kwa
kuchechemea.
Baadhi ya wageni waalikwa walibaki
wakimshangaa na kusema kuwa
hapendezi akinywa pombe kwani
ustaarabu wote unapotea.
Mbali na pombe pia alikuwa kivutio
kwa staili ya ukataji wake wa mauno
akiwa na kivazi kilichoacha nje
mapaja yake akiwa na rafiki yake
aliyetajwa kwa jina moja la Vivi.
Katika hatua nyingine, Vanita
alijikuta akiangua kilio baada ya
wapiga ngoma wa kibao kata ‘kuwa
feki’ na kushindwa kufanya kazi
kama walivyoahidi.
Mshereheshaji akimvaa Vanita.
Kutokana na hilo, baadhi ya mastaa
kama Aunt Ezekiel na Yobnesh Yusuf
‘Batuli’ waligoma kucheza na
kukizomea kibao kata hicho ambacho
kililetwa na MC (jina linahifadhiwa)
akidai kuwa amewatoa Bagamoyo na
wana ufundi wa hali ya juu.
Mwisho wa shughuli, MC huyo
alimvaa Vanita akitaka alipwe
pamoja na kwamba wapiga ngoma
wa kibao kata hicho walishindwa
kazi hivyo kukaibuka mtiti wa aina
yake huku kila mtu akitimua zake.
Monday, May 12, 2014
JAMANI JACQUELINE WOLPER A.K.A GAMBE ALEWA HADI KUANGUKA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment