Friday, May 16, 2014

MPOKI HANA AKILI KABISA .SOMA HAPA CHINI....

MPOKI HANA AKILI KABISA, AZIDI
KUWACHAFUA WATU KIBAO KWA MADAI
KUWA NI UTANI...CHEKI HAPA
Stori: JOSEPH SHALUWA
IMETHIBITIKA bila shaka yoyote kuwa
msanii aliyebahatika kuwa maarufu wa
vichekesho Bongo, Silvery Mjuni ‘Mpoki’
au Bepari la Kihaya ni mjinga yaani 0
brain kwa Kimombo, Gazeti kiongozi kwa
habari za mastaa Ijumaa limejiridhisha.
Msanii aliyebahatika kuwa maarufu wa
vichekesho Bongo, Silvery Mjuni ‘Mpoki’
au Bepari la Kihaya.
Hata hivyo, ikiwa msanii huyo ambaye
kwa fikra zake anaamini ndiye mkali
kuliko wachekeshaji wote Bongo
japokuwa Mzee Majuto ndiye namba
moja, anaweza kuwa mwerevu badala ya
kuendelea kuwa mjinga.
KWA NINI MJINGA?
Kwa mujibu wa Kamusi ya Kiswahili
Sanifu (Oxford – Toleo la Pili)
inamuelezea mjinga kuwa ni mtu asiyejua
kitu au jambo fulani.
Hata hivyo, mjinga hawezi kuendelea
kubaki katika hali hiyo baada ya
kufundishwa na kujua maana.
HABARI KAMILI
Tukio la Mpoki hivi karibuni
kuwadhalilisha watu waliofika jukwaani
kukabidhi tuzo kwa washindi katika Tuzo
za Kilimanjaro Tanzania Music Awards
(KTMA) kwenye Ukumbi wa Mlimani City
jijini Dar ni ushahidi tosha kuwa ana
tatizo la kufikiri.
Ukiachana na tukio hilo, rekodi yake ya
maisha yake ya kisanii na nje ya sanaa
inathibitisha asivyo hodari wa kutumia
ubongo wake sawasawa, vijana wa mtaani
huita zero brain (0).
Kwa uelewa wake, uchekeshaji ni
udhalilishaji ndiyo maana vipande vingi
anavyoigiza huwa anawasema watu
vibaya hata wale ambao wamemsadia
kufika alipo kisanii.
TUZO ZA KILI
Katika hali ya kawaida, kwa mtu asiye
mjinga na anayejitambua, Mpoki
asingeweza kumkejeli mtu mwenye
heshima zake kama Asha Baraka ambaye
ni Mkurugenzi wa Aset.
Silvery Mjuni ‘Mpoki’ akiwa kazini.
Asha anaweza kuwa mama yake lakini
bila haya alimwambia mbele ya hadhara
kuwa kwa alivyo na mwonekano mzuri
kwa usiku ule, asubuhi yake angeweza
kusalimiwa shikamoo (akimaanisha
angekuwa na mwonekano wa kizee kwa
kuwa hatakuwa na make up tena).
Hakuishia hapo, Mpoki alifikia hatua ya
kuingilia hadi mambo binafsi ya watu
ambayo katika hali ya kawaida hayawezi
kuwa utani, alimwambia Maimartha Jesse
kuwa licha ya kwamba ananyonyesha
lakini amepiga matiti jeki. Upuuzi mtupu!
NJE YA KILI
Ukiachana na kero alizotoa kwenye
jukwaa lile linaloheshimika, Mpoki ana
tabia ya kuwadhalilisha watu hata
anapokuwa kwenye kazi zake. Mifano ipo
mingi.
Kutokana na kile kinachoonekana
kutojielewa, Mpoki humkejeli mtu
makusudi ili kutengeneza bifu akiamini
magazeti yakimwandika ataendelea kuwa
juu.
Hivi karibuni alitoa wimbo ambao ndani
yake amewatukana baadhi ya watu
akiwemo mwandishi mmoja mashuhuri
nchini wa magazeti pendwa kwa kumuita
dada wakati akijua ni mwanaume
(anapenda misala).
Kwa akili zake fupi, aliamini paparazi
huyo angepaniki na kurushiana naye
maneno kwenye magazeti na mitandao ya
kijamii, hakufanya hivyo na mpaka sasa
yuko kimya kabisa kama hakuna kitu
kilichotokea kwa sababu ni mwerevu.
Pia jamaa huyo bila haya wala soni
aliwahi kuigiza kwa kumkejeli
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,
Reginald Mengi kwenye maigizo yao ya
Orijino Komedi.
Ikumbukwe kuwa, Televisheni ya Afrika
Mashariki (EATV) inayomilikiwa na mzee
Mengi ndiyo iliyorusha kipindi chao cha
vichekesho kwa mara ya kwanza. Kifupi
ndiye aliyemtoa baada ya kupigika kwa
muda mrefu.
Mpoki alitambulishwa kwa mara ya
kwanza na Runinga ya ITV akiwa na
Kundi la Nyota Ensemble kupigtia Kipindi
cha Mambo Hayo cha ITV ambacho ni
mali ya mzee Mengi.
WADAU WACHARUKA
Wadau wa burudani Bongo waliopata
kuzungumza na Ijumaa kwa nyakati
tofauti, walionesha hisia zao za wazi kwa
namna walivyokasirishwa na msanii huyo
mwenye mdomo mchafu na asiyepima
maneno.
Wapo waliokwenda mbali zaidi kwa
kusema kwamba ikiwa kutakuwa na
shughuli yoyote ya kiburudani na msanii
huyo akapangwa kuwa MC basi
hawatahudhuria kwa kuogopa
kudhalilishwa.
Nasra Abdillah wa Tabata jijini Dar
alisema: “Mimi nahisi kuna kitu cha zaidi
kwa Mpoki, si kwamba ni mchekeshaji,
nadhani kichwani hayupo vizuri. Mimi
nilikwenda Mlimani City siku ile, kuna
ndugu yangu alikuwa mmoja wa watoa
tuzo.
“Alipoona kila anayepanda anadhalilishwa
(ingawa kwa Mpoki ni utani) akaingiwa
hofu. Ilifika mahali akatamani kuahirisha
kwenda kutoa tuzo, tukampa moyo lakini
alipopanda mambo yakawa yaleyale,
akadhalilishwa waziwazi.
“Mpoki anatakiwa kubadilika. Nampa
ushauri wa bure, ajifunze kupitia kwa
wengine. Lakini hata hivyo mimi popote
ambapo yeye atakuwa mshereheshaji,
sitakanyaga hata kwa dawa.”
Dulla wa Sinza Kwaremmy alisema:
“Sikufurahishwa na kitendo cha
kumwambia Dj Bon Love na wadogo zake
kwamba ni wabahili wa fedha na
kumshangaa Vanessa Mdee kwa
kuzungumza Kiingereza wakati yeye ni
Mpare azungumze Kiswahili, halafu
akamkejeli eti awe anafanya mazoezi ya
kuvaa viatu virefu baada ya kunusurika
kuanguka jukwaani. Ule si utani ni
udhalilishaji.”
Mdau mwingine ambaye hakutaka
kutajwa jina lake alisema:
“Sikufurahishwa kabisa alivyomwambia
Isha Mashauzi, eti ni mwanamke wa
Kikurya, si wa kuoa.
Lakini mbaya zaidi akamwambia make up
zilimfanya aonekane msichana mrembo,
lakini akiamka asubuhi atapewa shikamoo
kwa mwonekano mpya atakaokuwanao.
Ile ilikuwa too much. Kifupi Mpoki ni
mpuuzi sana.”
HUYU AWAKUMBUKA TAJI, MILLARD
NA PENNY
January Kingamkono wa Msasani Dar,
yeye alikwenda mbali zaidi na
kuwakumbuka washereheshaji wa siku
zote katika hafla hiyo, Taji Liundi, Millard
Ayo, Jokate Mwegelo, Penniel Mungilwa
‘Penny’ na wengineo.
Hapa anafafanua: “Kili walichemsha kwa
kweli. Kumkaribisha Mpoki lilikuwa wazo
zuri lakini mizaha yake ilikuwa ya kijinga
sana. Alikuwa akiwatusi na kuwakejeli
watu na si kuchekesha. Nawashauri Kili
wafikirie kuwarudisha akina Taji na
wengine waliokuwa wakifanya vizuri kwa
pamoja kama kweli wanataka hafla yao
iwe na msisimko.
“Wakumbuke Tuzo za Kili siyo free event
(onesho la bure), watu wanatoa pesa zao.
Sasa lazima wazingatie kuwa
kinachotolewa kwa watazamaji
kinalingana na hela iliyolipwa. Kifupi
Mpoki aliboa,” alisema Kingamkono.
HUYU ATAKA AOMBE RADHI
Mdau mwingine, Juma Alii wa Manzese ya
Tip Top jijini Dar alisema: “Mpoki
anatakiwa kujifunza. Kila kona sasa hivi
gumzo ni yeye. Nasikia wale mastaa
waliokejeliwa wanataka kumfungulia
kesi, ni vyema ajifunze kusoma alama za
nyakati. Ajue alikosea na aombe radhi.
“Lakini pia ni vizuri kama atajifunza
kutoka kwa washereheshaji wengine,
namna wanavyofanya kazi kwenye
matukio rasmi kama hayo.”
TAJI ASHAURI
Mkongwe katika tasnia ya utangazaji
Bongo, Taji Liundi aliona kasoro za
Mpoki. Hata hivyo, kwa kutumia busara
alitupia katika ukurasa wake ndani ya
Mtandao wa Kijamii wa Facebook
akizungumzia hafla hiyo ambapo
aliandika: “Nadhani ingekuwa vema
kutambulisha wasoma tuzo vizuri.
Kuna mtu mmoja “Mhaya Mweupe”
angestahili kuwasilisha kwa umakini
zaidi!! Pia tunasikia mazungumzo ya
watangazaji na watu nyuma ya jukwaa
kupitia mic zisizozimwa. Onesho lina
msisimko lakini nadhani “production”
imekuwa na changamoto!
Maneno hayo yalitupiwa na Taji, Mei 4,
mwaka huu muda mfupi tu wadau
wakaibuka na kulipuka. Wa kwanza
alikuwa ni Dinne Shose ambaye
aliandika:
“Yaani Taji nimeliwaza hilo nikawa
nawaambia wadogo zangu...imekuwaje?
Wapi Taji?...ma MC hawana mvuto...utani
upo lakini hauchangamshi matokeo yake
utani umezidi hadi unaboa watu...wish
Taji, Millard, Jokate na Penniel mngekuwa
ma MC.”
Mara moja, Taji akajibu: “Dinne ahsante
kwa maoni. Sisi wazoefu tutapata
majukwaa mengine. Nadhani Shadee
kajitahidi sana lakini shoo ilikuwa ndefu,
focus inaweza kupotea. Mpoki katumia
mtindo wa Kevin Hart akiwa ana-MC
BET.”
TAJI AMTOLEA UVIVU
Baada ya mjadala kuwa mkali huku
wachangiaji wengi wakipeleka lawama
zao moja kwa moja kwa Mpoki, Taji
aliamua kumtolea uvivu kwa kuandika
hisia zake kwa ukweli kuhusu ubovu wa
aliouita utani lakini kumbe ni
udhalilishaji.
Sehemu ya maandishi ya Taji
yanasomeka: “Hakuna shaka kwamba
Mpoki ni mchekeshaji mzuri. Hapo juu
nimeelezea mtindo wake wa kukejeli
alipoutoa. Ni kwa mchekeshaji mwenzake
Kevin Hart. Je, alipitiliza? Nadhani
NDIYO. Kwa Bon Luv na Ray Kigosi.
Sikumwelewa Mpoki. Nadhani Martin
Kadinda naye hakupendezwa.
“Hapo sasa kuna tofauti ya KUCHEKESHA
na KUBEZA, pia ya kuwa MC! Kasoro
nyingine niliyoiona ni kurusha watu,
Fina, Ruge... Sijui kama ilikuwa kwenye
script. Mchango wa Fina unaeleweka
kupitia OnePlus (kejeli za Mngoni kuzaa
na Mzungu hazikuwa na ladha).
“Naamini Mpoki atapokea maoni chanya
ili aweze kuji-balance akifungua mdomo.
Ajipange. Kuna kitu kinaitwa MANENO
MATUPU, kama vile kujitangaza kuwa ni
MC wa harusi angali anafanya KTMA mara
ya pili na kuaminika, masuala ya kulipwa
ontime mbele ya Kavishe???? Matani ya
“kiutu uzima” kwenye Live TV, watoto
wanaangalia!!
“Anyway, yote haya hayatakosa
kukosolewa kwa tamasha kubwa kama
lile. Nadhani hakuna mchangiaji
anayechukia KTMA. Kuomba ushauri
wasiache.
Ikiwa watu wanalewa ukumbini,
unategemea nini kama nusu ukumbi
ukiamka kumtuza, kumtukana Diamond
au kuwafuata wasanii backstage? Dah!!
Kungekuwa na bucket la maji kwa kila
mchemshaji! Ni kusema lile tangazo nalo
tata! Si Sprite vile? Naona kama watu
watamwagiana pombe??!”
MDAU MWINGINE
Edwine Ndaki alisema: “ Taji Liundi upo
sahihi, nimependa ulifanya uchambuzi na
ushauri. Kwa sisi tulio nje ya nchi
tunapongeza kwa wazo la kurusha event
live online. Mpoki next time au popote
inabidi aangalie utani gani na wapi.”
JIMMY CHOCOLATE MKATTE
“Iko haja ya ma - MC kufanyiwa rotation,
rafiki yangu Mpoki alibweteka
akamnyima Co - MC nafasi. That was
illegal.”
BINTI SHANGWE
“Kasoro kibao, MC wameboa, hakuna
mpangilio, huyu hajamaliza kuongea,
huyu kashadakia, hasa Mwarabu wa
Dubai, mtu anayetaja jina la mshindi na
MC inabidi wapokezane mic...”
KILI: HATUKUJUA KAMA ANGEHARIBU
Mmoja wa wanakamati ya maandalizi ya
tuzo hizo, kwa sharti la kutotajwa jina
lake gazetini kwa maelezo kuwa si
msemaji, alizungumzia kuhusu
udhalilishaji uliofanywa na Mpoki,
akasema hawakujua kama angefanya vile.
“Tulimwamini maana tulishawahi kufanya
naye kazi. Kilichotokea pale
kilitushangaza sana lakini isingekuwa
rahisi kumrekebisha wakati akiwa tayari
yuko jukwaani. Pengine utekelezaji wa
hilo ungesababisha tatizo jingine kubwa
zaidi. Niseme tu, tumejifunza.”
KUTOKA DAWATI LA IJUMAA
Mpoki, wewe ni staa na una heshima
kubwa kwenye jamii. Kila binadamu
amepewa akili; uwezo wa kufikiri upo
kwa kila mmoja tatizo ni pale kwenye
uamuzi wa kutumia. Ni vyema sasa
ukabadilisha staili ya maisha na uanze
kutumia akili yako ipasavyo.
Vichekesho siyo kuwadhalilisha watu,
lakini kubwa zaidi kumbuka ulipotoka,
acha kuwakejeli hadi waliokusaidia –
hata hivyo si uungwana kuwadhalilisha
watu.
Badilika ili uondoke kwenye ujinga kwa
kuchekesha vitu vyenye mantiki ili uwe
mwerevu. Inawezekana ukiamua! –
MHARIRI.
source; GPL

No comments:

Post a Comment