Monday, December 29, 2014

SG NIKUPE NINI

Msanii wa mziki SG anayefanya vizuri kwenye soko la bongo fleva ameachia nyimbo kali inayoitwa NIKUPE NINI hebu udownload hapa-

Friday, December 5, 2014

JE UNAJUA ALICHOKISEMA DIAMOND KWA ALIKIBA???..MSIKIE HAPA..!

Baada ya Diamond Platnumz kutua jijini Dar
es salaam December 2 akitokea Afrika
Kusini akiwa na tuzo zake 3 za Channel O,
alikutana na wadau, mashabiki pamoja na
waandishi pale Escape 1 kuzungumzia
ushindi wake na safari nzima ilivyokuwa.
Miongoni mwa maeneo aliyozungumzia ni
pamoja na umoja unaohitajika kwa wasanii
wa Tanzania ili waweze kuwa wengi katika
majukwaa ya kimataifa.
“Ombi langu mimi kiukweli ni moja tu,
Unajua lazima kama alivyosema
mheshimiwa hapa muziki wetu ushakuwa,
watu wanaukubali na tushaona njia kama
tunaweza so lazima sisi tujiamini wenyewe
tusikaekae sana nyuma kwasababu watu
kuna ile kuogopa cha kuona kama aah
watanipokea kweli. Na zile za aah
ntashindwa kuongea kizungu ntachekwa mi
nishachekwa sana kwenye kizungu sana,
lakini saizi naweza nikaingia hata Big
Brother na broken zangu hivyo hivyo lakini
napita hivyo hivyo nimeingia pale juzi Fally
hajaongea mi nimeongea “.
Diamond pia ameendelea kuwaomba wasanii
wenzake kutotengenezeana beef za wenyewe
kwa wenyewe, na hakusita kumtaja Ally Kiba
wakati akitoa mifano alipokuwa Nigeria na
kujiona yuko peke yake hakuna msanii
yeyote wa nyumbani zaidi yake.
“Kingine mimi nilikuwa nataka niombe
tufute zile zama zakutengenezeana matatizo
wasanii wenyewe kwa wenyewe wa Tanzania
kwasababu haiwezi kutusaidia kabisa,
alikuwa anaongea kitu mkubwa hapa,
nilivyofika Nigeria nilikuwa najiona kama
mkiwa kwasababu niko peke yangu,
nikiangalia huku simuoni hata Jaguar, huku
siwaoni wasanii wenzangu namtafuta
Dimpoz namtafuta nani, hata Ally simuoni
yaani niko peke yangu.”

Sunday, November 30, 2014

BABA LEVO AMCHANA ALLY KIBA KUWA AJINYONGE

Ally kiba naomba uingie mwenyeewe coz umeyataka mwenyewe.. sungura ulikuwa umesha mkamata eti umemuachia kiboya boya sasa kumkamata tena itaghalimu miaka mitano... Sisi wote Tupo kwenye Sanaa ila nguvu tunazidiana ndomana ally nilikuona mkombozi Wetu coz we ni fundi muziki.. Inakuwa je unajianguaha kwenye kumi na nane?????? Badala ya kufunga unategemea penati... Ona sasa refa kapeta... Na kufanya Kwa sasa tukubali bwana @diamondplatnum ni #KIBOKO japo alikwapua Ka aidia kangu na ndo kanakompa mijituzo.. Ila nime hands up... Ally kiba na diamond wote ni ma home boy kutoka KIGOMA ila mnyonge mnyongeni Haki yake mpeni... Hii ni kick kuna mtu yeyote mwenye snea??

Wednesday, November 26, 2014

SOMA MAJINA YA WALIOKULA FEDHA ZA AKAUNTI YA ESCROW KATIKA RIPOTI YA PAC INAYOSOMWA LEO BUNGENI.

Zitto: Upande wa viongozi wa kisiasa ambao
waliingiziwa fedha katika akaunti zao binafsi ni;
Mhe.
Andrew Chenge (Mb)
Zitto: Andrew Chenge aliingiziwa shilingi bilioni
1.6.
Zitto: Mhe. Anna Tibaijuka (Mb) na Waziri wa 62
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi shilingi
bilioni 1.6.
Zitto: Mhe.William Ngeleja (Mb) na ambaye
alikuwa Waziri wa Nishati na Madini alipewa
shilingi milioni 40.4
Zitto: Ndg. Daniel N. Yona ambaye alikuwa pia
Waziri wa Nishati na Madini alipewa shilingi milioni
40.4.
Zitto: Ndg. Paul Kimiti ambaye ni Mbunge Mstaafu
wa Jimbo la Sumbawanga
alipewa shilingi milioni 40.4
Zitto: Dr. Enos S. Bukuku ambaye alikuwa Mjumbe
wa Bodi ya TANESCO aliingiziwa shilingi milioni
161.7.
Zitto: Upande wa Majaji Prof. Eudes Ruhangisa,
aliingiziwa milioni 404.25 na J.A.K Mujulizi
aliingiziwa shilingi milioni 40.4
Zitto: kwa upande wa Watumishi wa umma,Ndg.
Philip Saliboko ambaye alikuwa mtumishi wa RITA
aliingiziwa
shilingi milioni 40.4
Zitto: Ndg. Emmanuel Daniel Ole Naiko ambaye
alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa (TIC) aliingiziwa
shilingi milioni 40.4
Zitto: Ndg. Lucy L. Appollo ambaye ni Mtumishi
wa TRA aliingiziwa shilingi milioni 80.8.
Zitto: Viongozi wa Madhehebu ya
Dini walioingiziwa fedha na Benki ya Mkombozi ni
Askofu 63
Methodius Kilaini shilingi 80.9
Zitto: Askofu Eusebius Nzigirwa shilingi milioni
40.4 na Mchungaji Alphonce Twimann Ye Simon
shilingi milioni 40.4.
Zitto: Watu walienda kugawana fedha kwenye
Benki tajwa wakiwa na mifuko ya rambo,
sandarusi,
mabox, magunia na lumbesa TegetaEscrow
Zitto: Bilioni 73.5
zilitolewa na kugawanywa kwa watu mbalimbali
kinyume cha
Sheria ya Benki Kuu na Taasisi za Fedha ya 2006
Zitto: Taarifa
ya benki (bank statements) yenye majina na
akaunti zote
zilizoingiziwa fedha zimeambatishwa.
Zitto: Kamati imebaini mawasiliano kutoka kwa
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini na
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha

Monday, November 17, 2014

MTOTO ALIYEGEUKA NYOKA AZUA BALAA…!!

Mtoto mchanga mwenye umri wa miezi minne amezua kizaazaa cha aina yake, baada ya kuwapo taarifa kwamba mara kadhaa umbo lake limekuwa likigeuka na kuwa nyoka na mwili wake ukiendelea kudhoofu kutokana na kukataa kunyonya maziwa ya mama yake.
Mtoto huyo (jina lake tunalihifadhi kwa sasa), wiki iliyopita alivuta umati wa wakazi wa Kijiji cha Nkome mkoani Geita ambao walifurika ndani na nje ya Kanisa la AICT Nkome, lililopo kijiji hapo, kushuhudia maombi ambayo alikuwa akifanyiwa ili kumkomboa katika kile kilichotafsiriwa kuwa ni mateso dhidi yake.

Ilikuwa saa 4.00 asubuhi Jumamosi, Novemba 8 mwaka huu wakati mtoto huyo alipofikishwa katika kanisa hilo na kuanza kufanyiwa maombi na sababu ya hatua hiyo ikielezwa kuwa ni kutokana na kuwa na umbo la nyoka na kwamba matendo yake yanaashiria kwamba mwenye asili ya nyoka ndani ya roho yake.

Mtoto huyo alifikishwa kanisani hapo na mama yake mzazi, Sarah Silasi wakitokea Kijiji cha Ichile, Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza, ambako alikimbia matukio yanayohusishwa na ushirikina.

Mmoja wa wazee wa kanisa hilo la AIC Nkome, Mathew Misana anasema: “Alikuwa anatoa ulimi mithili ya nyoka, mwendo wake anapolala alijizungusha kama nyoka na hata alipojikunja mwili wake ulikuwa kama unavyoona nyoka.”

Misana anasema matukio hayo na mengine kadhaa yakiwamo ya ngozi ya mtoto huyo kuwa nyeusi kama ya nyoka aina ya chatu, yaliwalazimisha ndugu na jamaa zake wakiongozwa na mama mzazi kutaka aombewe.

“Ngozi yake kuonekana kama ya mzee huku macho yake yakionekana kuwa makubwa na kichwa chake kuwa na umbo la nyoka pamoja na miguu, baada ya kuona hali hii tukaihusisha na mambo ya kishirikina na kuamua kuanza maombi,” alisisitiza.

Hata hivyo, muda mfupi baada ya maombi kuanza, taarifa za kuwapo kwa aina hiyo ya mtoto zilisambaa haraka na kusababisha umati mkubwa wa watu kujaa ndani ya kanisa hilo ambalo ni boma kwa maana kwamba ujenzi wake bado unaendelea.

“Watu wengi walijaa na wengine wakawa wanapanda juu ya miti na juu ya boma wakati mwingine matofali yalianguka. Hewa ikapungua na usalama ukawa mdogo kwani watu walisukumana wakitaka kushuhudia,” anasema Misana.

Baada ya watu kuwa wengi, uongozi wa kanisa uliomba msaada wa Polisi wa Kituo cha Nkome ambao walifika kanisani hapo na kushauri mtoto huyo aonyeshwe ili watu waweze kuridhika kwamba hakuwa amegeuka kuwa nyoka.

Uongozi wa kanisa ulifanya hivyo lakini mwonekano wa mtoto huyo ulisababisha watu kuongezeka badala ya kupungua na hapo ndipo polisi walipoelekeza mama wa mtoto huyo ambebe na kuondoka naye hadi kituoni.

Mwinjilisti wa kanisa hilo, Emmanuel Misungwi anasimulia: “Tumeshudia vitu visivyo vya kawaida wakati tunafanya maombi na wakati tunaendelea na huduma, mama wa mtoto Sarah alianguka akaanza kuongea juu ya mtoto kwa nguvu ya mapepo.”
SOURCE:MWANANCHI

Wednesday, November 12, 2014

BREAKING:RAPPER GEEZ MABOVU AFARIKI DUNIA

Taarifa zilizothibitishwa ni kwamba rapper Geez
Mabovu ambae ni maarufu kwenye muziki wa
hiphop Tanzania, amefariki dunia kwenye
hospitali aliyokua amelazwa nyumbani kwao
Iringa alikokwenda wiki mbili zilizopita kutokea
Dar es salaam.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Iringa, Geez
amefariki jioni hii. Alienda kwao wiki moja na
nusu iliyopita ambako alianza kuugua mfululizo
mpaka mauti yalipomkuta.
Geez atazikwa kesho (Leo) jioni November 13
2014.

Saturday, November 8, 2014

SITTI ABBAS MTEVU KUJIVUA UMISS TANZANIA

Barua ya Sitti Mtemvu:

Mimi Sitti Abbas Mtemvu baada ya kutwaa taji la urembo la Miss Tanzania kumezuka shutuma mbalimbali dhidi yangu. Wameniwekea  maneno mengi sana mdomoni kwamba nimesema wakati sio. Shutuma hizo zimeandikwa katika vyombo mbalimbali vya habari, blogs na mitandao ya kijamii, kiasi ambacho naweza hata kuhatarisha maisha yangu.

Sasa kwa hiari yangu tena bila kushawishiwa na mtu na kwa kulinda heshima yangu na familia yangu natamka rasmi kuvua taji la urembo la Miss Tanzania 2014. Napenda niwashukuru wale wote waliokuwa wakinipa sapoti tangu mwanzo nilipoingia katika mashindano haya katika ngazi ya taifa, na warembo wote wa Chang’ombe, Temeke pamoja na wote tuliokuwa nao katika fainali za Taifa.

Pia napenda kutuma shukrani za dhati kwa waandaji wote wa kituo cha Chang’ombe, Temeke na wajumbe wa Kamati ya Miss Tanzania kwa mafunzo mbalimbali niliyopata. Nawashukuru pia waandishi wote kwa mchango wenu, pamoja na wizara ya habari, utamaduni na michezo na Baraza la Sanaa kwa busara zenu. Leo nalivuta taji rasmi nililopewa na binadamu lakini alilonipa mwenyezi Mungu bado ninalo. Mwisho naomba radhi Watanzania wote kwa uamuzi niliouchukua.

Wednesday, November 5, 2014

RAIS KUOMBWA MSAADA WA FEDHA KUTOA MWILI WA DADA AKE MOCHWARI

Rais kuombwa Msaada wa
fedha kuutoa mwili wa dada yake
Mochwari…
Baadhi ya viongozi wakubwa duniani ikiwemo
Marais, Viongozi wa kidini na wengineo
wamekuwa na utaratibu wa kutumia huduma
za mitandao ya kijamii na simu za mkononi
kuwasiliana na watu.
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ni moja ya
marais ambao wamekuwa wakitajwa kutumia
sana mitandao ya kijamii ikiwemo Twitter.
Huenda usiamini alichokifanya Rais Uhuru
Kenyatta, stori ni kwamba baada ya
kutumiwa message na Anita Lipesa ambaye
alikwama shilingi milioni tatu na laki tano za
Kenya kwa ajili ya kutoa mwili wa dada yake
aliyefariki kutoka chumba cha kuhifadhia
maiti.
Anita amesema baada ya jitihada za
kuchangisha michango kushindikana aliamua
kumtumia ujumbe kwa Rais Kenyatta ingawa
hakuwa na tumaini lolote kujibiwa, dakika 30
baada ya kutuma message hiyo Kenyatta
alimpigia simu dada huyo ambaye hakuamini
kama Rais angeweza kufanya hivyo.
Dada huyo anasema baada ya kumwelezea
Rais kilichotokea alipata msaada wa kuutoa
mwili wa dada yake huyo na kwenda kufanya
mazishi.
Anita (mwenye t-shirt nyeusi) akiwa
na familia yake.

BOB JUNIOR AMPA RAHA SABBY ANGEL

Jamani Bob Junior Ananipa Raha Kwa
Kila Namna Sijawahi Kuona: Sabby Angel
Wawili wapendanapo dunia huwa
maua !...........Muigizaji mwenye mvuto wa aina
yake katika kiwanda cha filamu Tanzania Sabby
Angel amesema kuwa Mahaba anayopewa na
Bob Junior hajawahi kuyapata popote pale
kwani anamridhisha kwa kila namna kiasi cha
kufurahia maisha yake ya kimapenzi kwasasa,
yaani full raha tupu!.
Sabby amesema kuwa ametembea huku na
huko lakini kwa Bob Junior amenyoosha
mikono juuu!
Wawili hao wiki ilopita waliongozana wote
kwenda Tanga ambapo Bob Junior alikuwa na
show huko.
Sabby

Tuesday, November 4, 2014

WEMA SEPETU ACHAFUA HUKO INSTAGRAM WANAOSEMA AZAE

Okay... Lets get things straight here.... See dat doggie up there... Y'all see her....? Dat is my bebi.... since i dont have a bebi... Huyo ndo mtoto wng... Basi sasa nitapopost afu nisikie kuzaa nakublock fasta... Mshaniona sizai basi ndo mjue sizai... Akha...!! Zaa zaa... If u have a child im happy for u... Nd wish u da best... I dont... Ndo mungu alivyonipangia... So please hey.... Watakaozaa all da best... Walio na mipango ya kuzaa hongereni... Mimi sina ... Im done... Vanilla ndo bebi wangu kipenzi na nampenda kuliko.... Na wale wa subhannah llah pia nisiwaone... This is getting too personal sasa...

Monday, November 3, 2014

Huyu ndie kijana wa CCM inayesemakana Kampiga Waziri Mkuu Mstafu Mzee Warioba na Chupa ya Maji leo Ubungo

Jambo la aibu na la kufedhehesha sana
limetokea leo katika mdahalo uliondaliwa
na taasisi ya mwalimu Nyerere,Ubungo.
Katika mdahalo huo , vijana ambao mpaka
sasa hawajafahamika walisisima gafla wote
kwa pamoja wakiwa na mabango
yanayopigia debe katiba inayopendekezwa
na gafla fujo kubwa zikaibuka na watu
kuanza kupigana.
Kada wa CCM bwana Paul Makonda,
pichani, inasemekana alimpiga Mwenyekiti
wa tume ya mabadiliko ya katiba Mzee
Joseph Sinde Walioba kwa chupa ya maji.
Hili ni jambo la kwanza la aibu ya aina yake
kutokea nchini kwa kijana mdogo kumpiga
waziri mkuu wa nchi na chupa ya maji.
Tunatumai vyombo vya sheria vitachunguza
tukio hili na kuwachukulia hatu vijana wote
waliohusika katika fedheha hii.
TOA MAONI YAKO:

Thursday, October 30, 2014

WOLPER AONGEA KWA UCHUNGU KUPITIA HILI GAZETI NA KUKANUSHA HII HABARI

NAOMBA MNISHAURI KUHUSU HILI GAZETI MKIWA KMA MASHABKI ZANGU MAANA AKUNA UKWELI ...NA JE NIVEMA KWEL MAANA TUNAWAZAZI NA PIA TUNA WAPENZI SASA MTU UTAANZA KUJIELEZEA VP KWA MPENZ WAKO ILI AKUELEWE KWAMBA HZI HABAR SYO ZAKWELI...LAKN PIA ALLY KBA NINGEPENDA UANDIKE CHOCHOTE KMA NI KWENYE ACC YAKO AU UTAJBU HAPA KWANGU ..HII NI KWA UPANDE WANGU...HOPE IREN PIA KMA KAGUSWA NAE ATAANDIKA UKWEL WAKE..NIPO MWANZA KIKAZI GAZET HILI LIMENIKOSESHA RAHA SAANA ...NAOMBENI USHAUR WENU NAMSAADA PIA ATA KMA NIKESI NPO TAYAR ASANTENI KWAKUPOTEZA MUDA WENU..LKN PIA ANAEJUA KUNA MTU MTETEZ AU ANAIJUA SHERIA UMTAG..AMEN

BREAKING:MSANII MANENTO AFARIKI DUNIA

Habari zilizotufukia hivi punde zinasema kuwa muigizaji Mzee Manento amefariki dunia hapo jana. Bado tunafuatilia kwa karibu habari hizi nz chanzo ch kifo cha mzee wetu huyu.

Mzee Mnento atakumbukwa hasa kwa filamu alizocheza kiumakin na marehemu Kanumba. Hero of the church, Dar to lagos,fake pastor n.k pumzika kwa Amani

Mungu ailaze Roho ya maerehemu mahali pema peponi amina. 

Wednesday, October 29, 2014

MSANII NAY WA MITEGO NA MPENZI WAKE WAPATA MTOTO

Mchumba wa rapper Nay wa Mitego, Siwema amejifungua mtoto wa kiume jana ambapo pia ilikuwa ni siku ya kuzaliwa kwa mama wa msanii huyo.
Mtoto wa Nay akiwa na bibi yake

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Nay ameandika:Ooooooh my goooooood!!!! Leo ni cku ya kuzaliwa mama angu mzazi,,, tukiwa 2nakata cake napigiwa cm nimepata mtoto wakiume… yani kazaliwa cku 1 na bibi yake,,! Hao apo wamezaliwa leo… Asante Mungu.. Asante

DIAMOND KUTUNUKIWA PHD

DIAMOND KUTUNUKIWA PHD.!
Tarifa kutoka Idara ya Sanaa ya Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)
zinasema kuwa tarehe 8 Novemba 2014,
Kijana Nassib Abdul atatunukiwa Shahada
ya Uzamivu(Phd) na Chuo hicho kwa
kuthamini mchango wake kwenye jamii
kupitia sanaa.(Honorary PhD in Fine
&Perfoming Arts).
Alongside DIAMOND mwingine
atakayepewa Shahada hii ya Heshima
kwenye Mahafali haya ni Balozi Fulgence
Kazaura (marehemu) ambaye aliwahi kuwa
Chancellor wa UDSM miaka ya nyuma!!
Naibu Mkuu wa shule ya Sanaa na
Sayansi ya Jamii (College of Arts and
Social Sciences) Prof.H Sigala amekiri
kupokea maombi kutoka Idara ya Sanaa
za Maonesho (Department of Fine
&Perfoming Arts) ya kumtunuku Diamond
PhD.
Amesema bado haijadhibitika kama
Diamond atatunukiwa shahada hiyo hadi
bodi ya taaluma ya chuo (senate) ikae na
kupitia maombi hayo. “Senate ikikaa
inaweza kukubali au kukataa maombi
hayo, lakini kwa sasa hatuwezi kusema
lolote” alisema Prof.Sigala.
Mashabiki wa Diamond wamepokea kwa
furaha taarifa hizi na wengine wameanza
kurusha vijembe mitandaoni kujibu
mapigo ya waliomzomea Diamond kwny
tamasha la Fiesta mwaka huu.
Mdau mmoja wa karibu wa Diamond
amenukuliwa kwny ukurasa wake wa
Facebook akisema “Ningependa
kuwakaribisha Wazomeaji woooteee
wenye sauti mbaya sana waweze kufika
kwenye Viwanja vya UDSM kushuhudia
Tukio la Kihistoria kwa Mtoto huyu wa
Tandale ambaye ni BIDII NA HESHIMA
Vimemfikisha hapa.”
Ikiwa “Senate” ya UDSM itapitisha
maombi hayo, na Diamond kutunukiwa
Shahada hiyo basi atatambulika rasmi
kama DR.NASIBU ABDUL au Pengine
DR.DIAMOND PLATNUMZ au ukitaka
swaga unaweza sema DR.PLATNUMZ
BABY!
Baadhi ya watu wameonekana
kutoridhishwa na mapendekezo hayo ya
Idara ya Sanaa ya chuo kikuu cha Dar
kumtunuku Diamond PhD, huku wengine
wakinukuliwa wakisema “Ukistaajabu
Uprofesa wa JK utaona PhD ya Diamond”
SOURCE: JF

Breaking: CHIDI BENZ AFANIKIWA KUPATA DHAMANA


Hatimaye Rapa Chid Benz leo amefanikiwa
kupata dhamana na kutolewa rumande na
kurejea uraiani. Anatakiwa kufika
mahakamani Novemba 11 ambapo kesi yake
itatajwa tena.
Una lipi la kumwambia Chid Benz baada ya
kupata dhamana na kurejea uraiani?

Tuesday, October 28, 2014

Breaking: MHIMBILI WAPANDISHA GHARAMA ZA VITANDA

Kwa mujibu wa taarifa iliyosainiwa na
Mkurugenzi mtendaji wa hospitali hiyo, Dk
Marina Njelekela na kusambazwa kwenye
vyombo vya habari, Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili (MNH), imepandisha gharama ambapo
mgonjwa atakayelazwa atalazimika kulipa
Sh5,000 kwa siku.
Taarifa hiyo ilibainisha kuwa gharama mpya
ambazo zitalipwa kwa wagonjwa wote wa rufaa
zilianza kutumika Oktoba 17, mwaka huu
ambapo taarifa zaidi kutoka hospitalini hapo
zimebainisha kuwa tangu utaratibu huo uanze,
kumekuwa na tofauti kubwa na zamani kwa
sababu wagonjwa ambao hawana uwezo wa
kulipia kiasi hicho, hawalali hospitali hata kama
hali zao zingewataka kulazwa.

Monday, October 27, 2014

BREAKING :CHID BENZI KUFIKISHWA MAHAKAMANI


kufikishwa mahakamani kesho Asubuhi
MONDAY , 27TH OCT , 2014
Msanii wa muziki Chidi Benz anatarajiwa kufikishwa mahakamani siku ya kesho kujibu mashitaka kutokana na kesi ya kukamatwa na Dawa za Kulevya, tukio lililotokea Ijumaa wiki iliyopita.

Kwa mujibu wa Kamanda Geofrey Nzowa, Mkuu wa Kikosi cha kupambana na dawa za Kulevya nchini, Chidi Benz atafikishwa katika mahakama ya Kisutu ambapo atasomewa mashitaka yake kwa mara ya kwanza.
Chidi alipatikana na dawa za kulevya aina ya Heroine kete zipatazo 14 pamoja na misokoto ya Bangi katika kiwanja cha ndege cha Julius Nyerere akiwa anaelekea Mbeya kwa shughuli za kimuziki.

hemed phd ft gelly wa rhymes the one

Shilole - Namchukua (Official Video)

DOWNLOAD MWANA FA FT ALLY KIBA-KIBOKO

Elly bizzy kuhama offcial video

DOWNLOAD NEW SONG SHUKU-WE NI MZURI

BARUA YA DIAMOND (WCB ) KWA JWTZ

Friday, October 24, 2014

Breaking: CHIDI BENZI AKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA


Kuna taarifa zilitoka on millardayo.com leo
jioni kuhusu msanii wa muziki wa kizazi
kipya Chidi Benz kukamatwa na dawa za
kulevya katika uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam
akiwa anaelekea Mbeya kwenye show ya
Instagram Party ambayo inatarajiwa
kufanyika kesho.
millardayo.com iliahidi kuzifatilia hizi taarifa
kwa Polisi ili kupata uthibitisho ambapo
imefahamika ni kweli msanii huyu
amekamatwa leo mchana akiwa katika
sehemu ya kuondokea uwanjani hapo
ambapo baada ya alifanyiwa upekuzi na
kubainika amebeba dawa hizo ambapo ni
kete 14 za dawa za kulevya kwenye mfuko
wa shati lake na misokoto miwili ya bangi.
Kwenye mahojiano na millardayo.com
kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Hamisi
Selemani ambae ni kamanda wa polisi katika
viwanja vya ndege Tanzania amethibitisha
kukamatwa kwa Chidi Benz na kusema
msanii huyu alipohojiwa amekiri kweli kuwa
dawa hizo ni zake.
Amesema ‘Alikuja Airport kwa ajili ya safari
kwenda Mbeya, kete hizo 14 za dawa za
kulevya zilikua zimefungwafungwa na nailoni
na pia amekutwa na vifaa vingine
vinavyohusiana na watu wanaotumia dawa za
kulevya, kuna kigae na kijiko na yeye
mwenyewe anakiri ni vitu vyake huwa
anatumia ila anashangaa ni kwa nini
vimeweza kubaki kwenye mfuko,
tutamfikisha Mahakamani baada ya kuweza
kubaini ni dawa aina gani za kulevya’

    

BASATA KUMVUA TAJI MISS TANZANIA


BASATA Kumvua Taji Miss Tanzania 2014 Kwa
Kudanganya Umri
Sakata la lililojitokeza la mrembo wa Taifa wa
mwaka huu 'Redd's Miss Tanzania 2014', Sitti
Mtemvu kudaiwa kudanganya umri, limeingia
katika sura mpya baada ya Baraza la Sanaa
Tanzania (Basata) kueleza kuwa litamvua taji
hilo endapo itabainika kweli alichakachua umri
wake.
Katibu Mkuu wa Basata, Geoffrey Mwingereza,
aliliambia NIPASHE jana kuwa baraza hilo
linasubiri uchunguzi ukamilike na endapo
watabaini kuna udanganyifu ulifanyika
hawatakuwa na la kufanya zaidi ya kumvua taji.
Wakati Mwingereza akieleza hayo, viongozi wa
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo wanatarajia kukutana leo jijini Dar es
Salaam kwa ajili ya kujadili sakata hilo la Sitti.
Akizungumza na NIPASHE jana, Naibu Waziri wa
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo, Juma Nkamia, alisema serikali
imesikia taarifa za mkanganyiko kuhusiana na
mrembo huyo hivyo imeamua kuitisha kikao ili
kuanza kulifanyia kazi.
Nkamia alisema kamwe serikali
haiwezi kukaa kimya pale ambapo
jina la nchi linatajwa vibaya.
"Siwezi kukuambia hatua gani
zitachukuliwa, ila kesho (leo)
tutakuwa na kikao, serikali haiwezi
kukaa kimya, kuna vyombo vyake
vinalifanyia kazi," alisema Naibu
Waziri huyo.
Aliongeza kuwa yeye alikuwa nje
ya Dar es Salaam, lakini tayari
kuna maelekezo aliyoyatoa na
yameanza kufanyiwa kazi na
wizara hiyo.
Siku moja baada ya Sitti
kutangazwa mshindi wa taji hilo,
taarifa za mrembo huyo kuhusu umri wake
zilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii
zikionyesha kuwa ana miaka 25, hivyo hana sifa
za kushiriki shindano hilo hapa nchini.
Nakala ya hati ya kusafiria ya mrembo huyo
ambayo ilitolewa Februari 15, 2007 na muda
wake wa kumaliza kutumika ukiwa ni Februari
14, 2017 yenye namba AB 202696 inaonesha
Sitti ambaye pia anashikilia taji la Kitongoji cha
Chang'ombe na Kanda ya Temeke, alizaliwa
Mei 31, 1989.Pia taarifa nyingine zinazoone sha
mrembo huyo ana miaka 25 ni zilizokuwa
kwenye Taasisi ya Explore Talent, ikimtaja
kwamba anaishi Dallas, Texas, urefu wake ni
5'8, umbo lake ni la kati, asili yake ni Mwafrika
na rangi ya macho yake ni kahawia.
Juzi, Kamati ya Miss Tanzania iliyoko chini ya
Mratibu wa shindano hilo, Hashim Lundenga,
ilisema kuwa Sitti amezaliwa Mei 31, 1991 katika
wilaya ya Temeke jijini kwa mujibu wa cheti
chake cha kuzaliwa alichokionesha.
Lundenga alionesha cheti cha kuzaliwa cha Sitti
ambacho kimetolewa na Wakala wa Usajili,
Ufilisi na Udhamini (RITA) Septemba 9, mwaka
huu kikiwa na namba 1000580309 na kikimtaja
baba yake ni Abbas Mtemvu Zuberi (Mbunge-
Temeke) wakati mama ni Mariam Nassor Juma
(Diwani- Temeke).
Hata hivyo, Lundenga alisema kuwa kamati
yake inaendelea na uchunguzi kuhusiana na
taarifa hizo na endapo watabaini kuwepo na
udanganyifu watamchukulia hatua mrembo
huyo kwa kushirikiana na Basata.
Pia Lundenga na Sitti, walikanusha taarifa za
mrembo kuwa kuwa na mtoto na kusema
kwamba mwenye uthibitisho wa jambo hilo
anatakiwa aliwasilishe kwa kamati ili hatua
zichukuliwe.
Sitti aliibuka kidedea katika shindano la urembo
la taifa lililofanyika usiku wa Jumamosi ya
Oktoba 11 kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini
na kuwashinda washiriki wenzake 29 waliokuwa
wanawania taji hilo.

Sunday, October 19, 2014

MSIKILIZE MENEJA WA T.I AKIONGEA JINSI YA KUFANYA COLLABO NA T.I


Records, Jason Geter amesema ili msanii wa Afrika aweze kupata collabo na msanii mkubwa wa Marekani, anahitajika kuwa na ushawishi katika sehemu anayokotoka ili awe na kitu cha kumuongezea pia msanii huyo anayetaka kumshirikisha. Meneja wa T.I, Joson Gete akizungumza na wadau wa muziki Dar Jason Geter Akiongea kwenye warsha iliyoandaliwa maalumu kwaajili ya wadau wa muziki nchini Ijumaa hii, Geter alitolea mfano wa jinsi T.I. alivyokubali kufanya wimbo na P-Square. Alisema alipigiwa simu na rafiki yake aliyemueleza kuwa kundi la P-Square lingetaka kumshirikisha T.I. kwenye wimbo wake lakini bahati mbaya hakuwahi kuwasikia wasanii hao. “Kiukweli nilikuwa sijawahi kuwasikia kabla, kwasababu Marekani hawachezwi kivile, nina uhakika baadhi ya watu wanawafahamu lakini watu wengi Marekani hawawafahamu kabisa P-Square,” alisema. Geter alidai baada ya kuambiwa hivyo aliamua kufanya utafiti wake mwenyewe ili kuwafahamu wasanii hao na hivyo aliingia Youtube kuwatazama. “Nilipoenda kufanya utafiti wangu, nikasema wow, hawa jamaa ni wakubwa,” aliongeza. Alidai baada ya kuona ukubwa wake, aliona kuwa P-Square wana kitu cha kumuongeza T.I. “Sababu mashabiki wengi wa P-Square wanaweza kuwa hawajawahi hata kumsikia T.I. Kwahiyo hicho ndio kitu cha kwanza kwamba utaenda kumuongezea nini msanii wangu. Msanii wangu ana msingi wa Marekani kukupa, wewe utaweza kumtambulisha kwa kitu kingine?” Aliongeza kuwa hatua ya pili inahusisha masuala ya fedha na biashara ambapo huusikiliza wimbo anaotaka kushirikishwa msanii huyo. Alisisitiza kuwa mara nyingi suala la fedha au malipo ya collabo sio kitu wanachokiweka mbele zaidi ya kuzingatia kuwa ni nini msanii wake atakipata kutokana na kushirikishwa kwenye wimbo huo. “Sawa unayo fedha, sasa hatua ya pili, kitu gani unaweza kukioffer kwake, una kitu cha kuoffer kwa msanii wangu? Je wimbo ni mzuri? Kwahiyo hivyo ndio vitu ambavyo unahitaji kuvifikiria. Na mwisho wa siku zote unatakiwa kulinda brand yako.” Kuhusu njia anayotakiwa msanii kufanikiwa katika soko la muziki wa Marekani, Jason alisema jambo la kwanza ni kuwa na ukaribu na watu kama yeye ambao wana connection na watu wengi pamoja na brands ambazo zimesimama nchini humo. Geter alidai kufanya wimbo na msanii wa Marekani peke yake, haitoshi kwa msanii wa Afrika kufanikiwa kwenye soko la Marekani. “T.I. alifanya ngoma na P-Square, lakini kiukweli, inahitaji zaidi ya hivyo kupenya soko la Marekani,” alisisitiza Geter. “Inahitaji T.I. na P-Square kwenda kwenye game ya basketball pamoja na kutembea pamoja. Inahitaji uwekezaji huo wa muda kwa msanii wa Afrika kutumia muda kukaa kwenye soko la Marekani.” Geter alisisitiza kuwa kama msanii anataka kufanikiwa Marekani, anatakiwa kutake risk kwa kuacha fedha nyingi anazopata Afrika na kukubali kupata kidogo Marekani wakati anakuza jina lake. “Kama unaingiza dola 5 Afrika, unaweza kuja Marekani na utakuwa na bahati sana ukipata sehemu sahihi ambazo unaweza ukapata hata dola moja tu. Ni kazi sana kwa watu kuwekeza muda wa aina hiyo na nguvu katika chochote kile, hiyo ndio changamoto kubwa.” Geter alisema hilo linawezekana kwa kuingia ubia na watu ambao tayari wana nguvu huko kukusaidia. Kuhusu lugha ambayo msanii anatakiwa kutumia, Geter alisema muhimu ni kufahamu kuongea Kiingereza lakini sio lazima nyimbo ziwe za lugha hiyo kwakuwa muziki unaweza kufanya vizuri hata kama ukiwa umeimbwa kwa lugha nyingine. “Lakini yote ni kuwa kile ambacho tunafanana ni rhythm. Ni ile beat inayonifanya nicheze na pia hisia ambayo inagusa moyo. So in America to get played on radio and all that stuff, yes you need to know some English but if you got that beat right, we gonna move man.”msikilize apa

Thursday, October 16, 2014

KIJANA APIGISHWA MBIZI KWENYE DIMBWI

Askari wa jeshi la Wananchi
la Tanzania (JWTZ)
akimwadhibu kijana ambaye
hakuweza kufahamika jina lake
mara moja, kwa kumpigisha
mbizi kwenye dimbwi la maji
ya barabarani baada ya
kukutwa akiwa ametinga sare
za Jeshi la Wananchi huku
akipiga misele mitaani
wakati akitambua kuwa yeye
si askari ni raia wa
kawaida.
Kijana huyo alikutana na
adhabu hiyo kali kutoka kwa
mjeda huyo baada ya kumbaini
kuwa si askari halisi ya
jeshi la Tanzania wakati
alipokamatwa na kushindwa
kutoa maelezo ya kuridhisha
kuhusiana na swala zima la
kijeshi, na hapo ndipo
alipoanza kuamuliwa kuvua
mavazi hayo na kisha kuaza
kutumikia adhabu hiyo.
Tukio hilo lilitokea hivi
karibuni maeneo ya Kariakoo
jijini Dar es Salaam.
Kijana akiendelea kutumikia
adhabu ya kupiga mbizi.
Picha na Kamanda wa Matukio
Blog.Mia

DOWNLOAD WIMBO HUU WA ZACHAA FT DIAMOND

DOWNLOAD WIMBO WA MICHA PELO NILIAMUA MP3

DOWNLOAD WIMBO WA MICHA PELO FT ALLY NIPISHE MP3

DOWNLOAD WIMBO WA ELLY BIZZ mp3

DOWNLOAD WIMBO WA MASE H-MONEY MP3

Wednesday, October 15, 2014

HALIMA JAMES MDEE AFUNGUKA MAZITO



MBUNGE wa Jimbo la Kawe jijini Dar na
Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Bawacha),
Halima James Mdee ambaye aliwekwa
Mahabusu ya Gereza la Segerea, Dar kwa saa
kumi na mbili amesimulia mambo matano
mazito aliyokumbana nayo hali iliyomfanya
atokwe machozi.
Mbunge wa Jimbo la Kawe jijini Dar
na Mwenyekiti wa Baraza la
Wanawake wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo
(Bawacha), Halima James Mdee.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii
mwishomi mwa wiki iliyopita, Mdee licha ya
kuponda utendaji kazi mbovu wa serikali
kuhusu mahabusu, aliyataja mambo hayo kama
ifuatavyo:
HAUSIGELI NA KESI NDOGONDOGO
Alisema alipofika mahabusu aliwakuta
wasichana wadogo ambao baadhi yao ni
mahausigeli wakamlalamikia kwamba wamekaa
ndani kwa muda mrefu bila kesi zao kusikilizwa.
Alisema kwa uchunguzi wake alibaini kuwa
wasichana hao wa kazi za ndani, kesi zao
zilifunguliwa kwa kubambikwa na mabosi wao
pale wanapodai malipo, hivyo wao husingiziwa
wizi au kosa lolote.
UBOVU WA CHAKULA
Pia Mdee alisema chakula cha mahabusu
hakiridhishi kutokana na kupikwa bila kiwango
na kuwa na michanga, wakati mwingine hakiivi.
MAHABUSU KUKAA MUDA MREFU
BILA KESI KUSIKILIZWA
Jambo jingine alilodai kukumbana nalo Segerea
ni mahabusu kukaa kwa muda mrefu kati ya
miaka 4 hadi 7 bila kesi zao kusikilizwa kwa
kisingizio cha upelelezi kutokamilika.
MACHANGUDOA KUWASHAWISHI
MABINTI
Katika sakata lingine, Mdee alisema wanawake
wengi waliokamatwa kwa makosa ya kujiuza
usiku (machangu) wanaopelekwa mahabusu
wamekuwa wakiwashawishi wasichana wadogo,
hasa mahausigeli wanaofikishwa humo.
“Wasichana hao huwashawishi mahausigeli kiasi
kwamba wanapotoka mle mahabusu na wao
wanakwenda kujihusisha na ukahaba na
biashara ya madawa ya kulevya kwa vile baada
ya kutoka hawapewi nafasi na mabosi wao
kuendelea na kazi,” alisema Mdee.
MAHABUSU WA KIKE KUADHIBIWA
NA ASKARI WA KIUME
Jambo lingine aliloligundua Mheshimiwa Mdee
ni kitendo cha askari wa kiume kutoa adhabu
kwa maabusu wa kike badala ya kuadhibiwa na
wanawake wenzao kitendo ambacho alisema
kimekuwa kikiwadhalilisha mahabusu hao.
Hata hinyo, Mdee alimuomba Waziri wa Sheria
na Katiba, Asharose Migiro kuanzisha utaratibu
wa safari za kushtukiza magerezani na
kuzungumza na mahabusu ili kusikiliza kero zao
na kuzitatua.
Jumanne iliyopita, Mdee alifikishwa katika
gereza hilo saa 11 jioni ambako alilala hadi
kesho yake saa 1 asubuhi kwa madai ya
kufanya maandamano haramu kwenda Ikulu ya
Dar.

Friday, September 5, 2014

AJALI MBAYA IMETOKEA HUKO MUSOMA LEO HII NI AJALI MBAYA


Ajali kubwa sana imetokea huko musoma leo,ni
mabasi mawili yamegongana uso kwa uso!!! Hadi
sasa watu zaidi ya #34 wameripotiwa kufariki
dunia papo hapo!!!
Na majeruhi ni #83. Inasikitisha sana kwani
nimeshindwa kuposti hata picha za majeruhi,,

Saturday, July 26, 2014

DIAMOND ASHINDA TUZO MBILI

Wanaziita African Muzik Magazine Awards
ambapo za mwaka huu 2014 zimetolewa huko
Eisemann center Texas Marekani na
kuhudhuriwa na mastaa mbalimbali akiwemo
Diamond wa Tanzania ambae pia alikua
mmoja wa wanaowania tuzo.
Good news kwa mujibu wa meneja Babu Tale
ni kwamba Diamond ameshinda tuzo mbili
moja ya Msanii bora wa Afrika Mashariki na
nyingine ni wimbo bora wa kushirikiana ambao
ni ‘number one rmx’ alioufanya na Davido wa
Nigeria.
Stori zaidi na pichaz vitafata baadae hivyo
endelea kukaa karibu na millardayo.com mtu
wangu ili ujue kilichotokea kwenye tukio hili
ambalo limewahusisha wakali wengine kama
Davido, 2Face, Fally Ipupa, Iyanya, Flavour,
Wyre, Miriam Chemmoss na wengine ambao ni
sehemu ya watu kutoka nchi 17 za Afrika.

Sunday, July 20, 2014

DUH! DUNIA HII HATARI ONA MWENYEWE

Bora uwe na hamsini nzima kuliko mia mbovu. Vijana hawa walikua wakiiba wakakamatwa na wananchi wenye hasira kali na kuwekwa taili za gari na kuchomwa moto.

Friday, July 18, 2014

Lol!! VIDEO YA H-BABA IMEMGHARIMU LAKI NA NUSU

Video mpya ya H-Baba
imemgharimu Laki na Nusu tu
Star mwenye vipaji vingi nchini Tanzania H-
Baba amesema ukweli kuhusiana na gharama
zilizomgharimu katika video yake mpya ya
"Tubebane" itakayotoka hivi karibuni.
H amesema haina haja ya kuongea uongo ama
kudanganya Mashabiki wake kwa swala la
gharama. Amefafanua kuwa Video Production
amepewa bure. Pia ameoneshwa kukerwa na
wasanii wengine wanaodanganya kuwa
wamefanya video kwa gharama kubwa sana
kumbe wamefanyiwa bure, amekiri kuwa video
za gharama zipo hata ukitazama zinaonekana ila
wengi ni waongo.
Kwa hiyo mashabiki wote wa H-Baba muipokee
video hiyo ya "Tubebane"

Saturday, June 21, 2014

NJEMBA YAFUMANIWA IKILA UNYUMBA NA MKE WA RAFIKI AKE

Na mwandishi Jk boy
Mume aliyejulikana kwa jina moja la Ngosha,
mkazi wa Mabibo jijini Dar, amemfumania rafiki
yake aitwaye Jazira akiwa chumbani na mkewe
Jack wakiivunja amri ya sita ya Mwenyezi
Mungu.Tukio hilo lilitokea Jumanne iliyopita saa
12 alfajiri ambapo ilidaiwa kuwa Jack alikuwa
chumbani na mwanaume huyo ambaye ni
mpangaji, wenzake wakipeana maraha.
Imedaiwa kuwa, wawili hao walikuwa wakimtegea
Ngosha akitoka kwenda katika shughuli zake,
Jazira alikuwa akizama katika chumba cha rafiki
yake na kufanya mchezo wa kikubwa.
Wapangaji wenziye na Jack wamedai kuwa, mke
huyo wa mtu ambaye ana miezi miwili tangu
aolewe kutoka mkoani Tabora, amekuwa kero
katika nyumba hiyo kwani amekuwa akipiga
kelele za kimahaba nyakati za asubuhi ambapo
watu wengi wanakuwa wakielekea kazini.
“Hata sisi wanawake tunaoishi nyumba hiyo tuna
waume zetu tunawalilia lakini kinachotusikitisha
mwenzetu anamlilia Jazira badala ya mumewe
ambaye anakuwa amekwenda kazini,” alisema
mmoja wa wapangaji wa nyumba hiyo.
Imeelezwa kuwa, siku hiyo mlinzi wa msikiti
alikwenda kumwamsha Ngosha kwenda kusogeza
gari lake ili watu wapite na alipofika katika
chumba chake, alikuta mlango wa sebuleni ukiwa
wazi lakini hakukuwa na mtu, ila chumbani kwake
kulisikika redio ikizungumza kwa sauti kubwa.
Jirani mmoja aliyedai kuchoshwa na tabia hiyo,
alimshauri mlinzi huyo kwenda kusikiliza kwenye
dirisha la chumba hicho na waliposikia sauti za
kimahaba wakakubaliana wamtonye mjumbe wa
Serikali ya Mtaa wa Kanuni, Mabibo aliyetajwa
kwa jina la Asha ambaye alifika na kusikia
‘mchezo’ ukiendelea chumbani
Wakati huohuo, Ngosha akapigiwa simu kuja
kushuhudia mchezo huo mchafu wa mkewe
alioufanyia ndani ya chumba chake.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema, alipofika
Ngosha nyumbani na kutonywa kilichotokea
alipandwa na hasira na kuangusha varangati kwa
rafiki yake lakini baadaye akatulizwa, akamtaka
Jazira amlipe shilingi milioni 1.2 ili amuachie mke
moja kwa moja.
JAZIRA ANA LAKI 2
Jazira alisema hakuwa na kiasi hicho isipokuwa
anaweza kulipa shilingi laki mbili tu, jambo
lililomfanya Ngosha kuomba msaada wa askari
mgambo na kumpeleka mgoni wake Kituo cha
Polisi cha Urafiki kwa ajili ya hatua zaidi za
kisheria.

Saturday, June 7, 2014

DIAMOND PLATNUMZ AMEHUDHURIA TUZO ZA MTV MAMA 2014

Diamond Platinumz amehudhuria tuzo za MTV MAMA2014 akiwa na kampani ya watu kadhaa kutoka Tanzania na mchumba wake Wema Abraham Sepetu, katika ukumbi wa ICC Arena, hapa Durban Afrika Kusini.
Diamond anawania tuzo mbili, Best Male na Best Collaboration (Number One Remix ft Davido).
Utaratibu ulianzia kwenye zuria jekundu aka Red Carpet na kupoz kwa ajili ya picha na waliungana na watu mbalimbali maarufu.
Kuhusu tuzo alizokuwa akiwania Diamond, Tuzo ya Best Collabo kupitia wimbo wa Number One Rmx imechukuliwa na Uhuru Ft DJ Bucks, Oskido, Professor, Yuri Da Cunha -Y-tjukutja, na tuzo ya Best Male Artist ilichukuliwa na Davido.
Hongera kwa Diamond kwa hatua kubwa kwenye muziki wa Kimataifa na kuwakilisha Tanzania Vizuri.

Friday, May 30, 2014

PIGO JINGINE BONGO MOVIE MWONGOZAJI WA MOVIE GEORGE TYSON AFARIKI DUNIA

NI pigo tena kwa tasnia ya Bongo Muvi,
mwongozi filamu Bongo na aliyekuwa mume
wa staa wa filamu Bongo, Yvonny Cherry
‘Monalisa‘, George Tyson amefariki dunia
baada ya kupata ajali mbaya ya gari eneo la
Morogoro akitokea mkoani Dodoma. Tyson
alikuwa ameambatana na watu kadhaa
katika safari hiyo.

Wednesday, May 28, 2014

MSANII RACHEL HAULE KUZIKWA KESHO

MSANII wa filamu Rachel Haule ‘Recho’
aliyefariki dunia siku ya jana atazikwa jijini
Dar es Salamm siku ya kesho badala ya
Songea kama ilivyopangwa hapo awali.
Ratiba ya kuuaga mwili wa marehemu
inabaki pale pale siku ya kesho Leaders Club
na baadae kwenda kuzikwa katika makaburi
ya Kinonondoni.